Kupendwa na kila mtu

royna

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
479
335
Inawezekana kupendwa na kila mtu?na inabidi mtu afanyeje ili apendwe na kila mtu? msaada wa maoni wana MMU. Upendo huu sizungumzii ule wa romance hapana, naongelea kule kukubalika kwa kawaida.
 
Inawezekana kupendwa na kila mtu?na inabidi mtu afanyeje ili apendwe na kila mtu? msaada wa maoni wana MMU. Upendo huu sizungumzii ule wa romance hapana, naongelea kule kukubalika kwa kawaida.[/QU
NGUMU SANA KWA DUNIA HII ILA UNAWEZA KUPENDWA NA WENGI NA WAKATI HUO TEGEMEA KUNA AMBAO WATAANZA KUKUCHUKIA.........
 
Kwenye hii sayari ya tatu hata uwe mtenda mema vipi lazima maadui wataibuka tu.
Ukitegemea kupendwa jua tegemea na kuchukiwa pia

kitakachokuwa chema machoni pangu chaweza kuwa chukizo machoni pako!

Binadamu hatulingani so nivigumu sana kupokea upendo kwa 100% kutoka kwa watu wote.

Fanya mambo yaliyo mema kwa Mungu wako, kwako na jamii inayokuzunguka bila kujali nini utapata kwao, ukitegemea upendo kwa binadamu waweza ambulia umauti....!

Ndivyo binadamu walivyo!!!!!
 
^^
Binadamu hatuna jema,
Ukiwapenda anajipendekeza,
Ukifanya mambo yako anajipendelea,
Ukifa mzee alichelewa kufa,
Ukifa mdogo, angekuwa rais huyu,
Ukioa mapema yatamshinda,
Ukichelewa kuoa, jamaa -------,
Uwe mpole anaringa,
Uwe mwongeaji muongo,
Ushinde jf hana kazi ya kufanya,
Uadimike jf amefichwa,
NDIO ASILI YETU BINADAMU.
..
Fanya lililo sahihi na Usimwogope yeyote au Kumdharau yeyote
^^
 
Mie napendwa sana na watoto.....
Napenda sana kucheza nao ila baadhi ya mda hata watoto ambao sina mazoea nao napata hi zao na tabasamu...

^^
Farkina naomba nikuulize swali dogo, vipi unapenda na mimea yenye maua?
(kuna ka utafiti fulani nafanya kuhusu watu wanaopendwa sana na watoto wadogo hususani 0 years to 10 years , utanisaidia ukinijibu)
^^
 
Last edited by a moderator:
^^
Farkina naomba nikuulize swali dogo, vipi unapenda na mimea yenye maua?
(kuna ka utafiti fulani nafanya kuhusu watu wanaopendwa sana na watoto wadogo hususani 0 years to 10 years , utanisaidia ukinijibu)
^^

Yeah na nkipita njiani kama kuna maua mazuri lazma nichume...
 
Last edited by a moderator:
Jinsi unavyopiga hatua ya kimaisha maadui eanaongezeka..do maadui ni kipimo cha mafanikio...
 
Sidhani kama inawezekana. Tofauti zetu za kimaumbo na kimtazamo vina changia hilo. Pia ni changamoto za kimaisha usipokubalika na wote.
 
^^
Farkina naomba nikuulize swali dogo, vipi unapenda na mimea yenye maua?
(kuna ka utafiti fulani nafanya kuhusu watu wanaopendwa sana na watoto wadogo hususani 0 years to 10 years , utanisaidia ukinijibu)
^^

hata mie naclick sana na watoto,nawapenda,i feel free and loved around them too, na maua napenda sana,vp Himidini?
 
Last edited by a moderator:

Similar Discussions

Back
Top Bottom