Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,997
- Thread starter
- #21
Felister, nimependa sana mawazo yako:
Kwenye suala la kilimo Tanzania kabla ya kuchangia mawazo yango randomly nitaanza kwa kusema mambo yafuatayo ambayo niliwahi kuyaandika miaka minne iliyopita lakini sasa hivi naamini yana umuhimu wa pekee.
Kwanza, kama Taifa ni lazima tutambue kipaumbele chetu cha kiuchumi ni nini. Miaka hii minne au mitano iliyopita na ukienda hata kumi utaona kuwa dhana ya kupanga ni kuchagua haijaingia katika fikra za watawala na wanasiasa wetu na tumefikia kujaribu vitu vingi na karibu vyote tukivifanya vibaya. Je uchumi wetu utaendeshwa kwa madini (kama ilivyo Botswana na Namibia), Je uchumi utaendeshwa kwa mchanganyiko wa sekta (kama ilivyo Kenya ambapo kilimo, utalii na viwanda) vinachangia kwa kiasi kikubwa?
Tukiuliza kuhusu Uchumi wa Tanzania utaona kuwa in theory we are an agricultural economy lakini kilimo hicho siyo chenye mchango mkubwa kwenye uchumi which makes this statement a kind oxymoronic. So, la kwanza ni lazima tutambue ni nini kinapaswa kuendesha uchumi wetu.
Pili, ni lazima tutafute sera ya kuendesha injini hiyo ya uchumi wetu. Sasa hivi bado tumeweka mkazo mkubwa sana kwenye foreign capital investment (na hasa direct investments). Katika sera ya namna hiyo utaona kuwa tulichokifanya na ambacho tunajivunia kuwa ni maendeleo ni kile ninachokiita "importation of development". Kwa maana ya kwamba, maendeleo tunayaona hayana asili ya Tanzania bali tumeyaingiza kutoka ng'ambo.
Tunapofikia mahali tunaagiza vitunguu na nyanya kutoka ng'ambo, kandambili na samani toka ng'ambo na hadi kuona fahari ya kuvaa suruali na mashati toka majuu basi kile tunachoona kinapendezesha nchi yetu na mazingira yetu kwa kweli si cha kwetu. Nakumbuka (sijui kama vyote bado vipo, tuliwahi kuwa na kiwanda cha radio za national na hata betri!), sijui tungefika wapi kama tungeendeleza hayo hadi kuwa na assembly plants of other electronics na kuchukua nafasi ya sehemu kama South Korea, Taiwan, Hong Kong n.k
So, sera hapa ninayoiashiria ni kuwa kama tunataka kuinua kilimo we have to get back to agriculture for self-reliance. Katika pendekezo lako bado unaona ulazima wa kuwa na wawekezaji wa nje katika kilimo, I don't. Hata hivyo, hilo linaonekana ni la muhimu kwa sababu sisi wenyewe tumeona kilimo ni fani au ajira duni.
Tatu, chochote tunachotaka kufanya kwenye kilimo ni lazima kiwe kitu ambacho tuna faida nacho zaidi kulinganisha na nchi nyingine au sehemu nyingine duniani. Kiviwanda, hatuna faida kuliko Ujerumani, Marekani, China n.k Hivyo, kufikiria tunaweza kuingia katika viwanda vikubwa (heavy industries) na kutengeneza uchumi wenye nguvu ni gumu kweli. Ukija kwenye viwanda vyenye mwelekeo wa teknolojia ya electronics hatuna faida kubwa (comparative advantage) kulinganisha na China, India, Hong Kong, Taiwan na Japan. So, chochote tutakachofanya kitakumbana na ushindani mkubwa sana kwenye soko la kimataifa. Ninachosema ni kuwa bado tuna maeneo mawili tu au matatu na katika hayo matatu ni eneo moja tu naamini tuna comparative advantage kuliko nchi nyingine yoyote ile duniani (if I may so boldly).
Hivyo, kutoka hayo matatu yatafuata mapendekezo yangu ya kuona kilimo chetu kinavyoweza kuwa chanzo cha utajiri wa kudumu kwa mtu wa kawaida, kuchochea pato la taifa, kuingiza fedha za kigeni na kuinua hali ya maisha ya wananchi wetu. So far, bado hatujaanza hivyo.