Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,468
- 911,174
EWURA wamewakumbatia Bulk suppliers wako takribani 5 na wengi wao wana asili ya India. Hawa wazabuni hukaa na kupanga bei ya kuuza mafuta kwa bei waitakayo na hivyo kutufukarisha lakini baadhi ya wenzetu walioko EWURA na Wizara ya Nishati wamevuna utajiri wa kutisha.
Maswali yafuatayo EWURA kamwe hawawezi kuyajibu nayo ni:-
Kwanza, EWURA watupe sababu za mafuta kuagizwa kutoka India ambao ni wachuuzi tu wa mafuta kutoka Urusi?
Pili, kwanini EWURA hawanunui mafuta moja kwa moja kutoka Urusi ambapo pipa moja la lita 100 lauzwa dola 30 chini ya bei ya dunia?
Tatu, kwanini EWURA ni walaini sanaaaaaaa kuitia hasara taifa kwa kununua mafuta bei ambayo ni juu ya bei ya soko? India inaponunua mafuta ya Urusi kwa punguzo la dola 30 hilo punguzo hawalipeleki kwa walaji bali hubaki nalo. Pia, wanaweka kodi zao sasa ukichanganya na ufisadi uliomo humo na kodi zetu bei ya mafuta kwa mlaji lazima iwe ya juu kupindukia!
Nne, kwanini wazabuni wanaoshinda zabuni hujirudiarudia makampuni yaleyale kama hayajajijengea mtandao hapo EWURA na Wizara husika?
Tano, kwanini EWURA wao wenyewe wasiagize mafuta kutoka Urusi na kupata punguzo la dola 30 kila pipa na kuachana na kodi za India na ufisadi wao?
Sita, kwanini serikali bado imeweka kodi za EWURA katika ankara za umeme wakati wanao uwezo wa kujiendesha yenyewe? Tunasema ruzuku kwa EWURA kumechangia sana kuuwa ubunifu maana wanashawishika kuweka mbele ufisadi wao na masilahi ya taifa baadaye wakijua tutawazawadia kwa kufanya hivyo kupitia ruzuku za kodi mbalimbali.
Saba, hivi ni wahindi tu ndiyo wenye uwezo wa kuagiza mafuta?
Nane, kwanini tununue mafuta kwa dola wakati Urusi wako tayari tununue mafuta kwa hela zetu za madafu? Hivi kwanini bado tunaongelea dola wakati tupo dunia ya BRICS?
Ninawakilisha.
Pia soma: Petroli na Diesel bei Juu. Dola yaelezwa kuwa sababu ya bei kupaa