Kwetunikwetu
JF-Expert Member
- Dec 23, 2007
- 1,535
- 408
Njelu Kasaka na wabunge wenzake wa kundi la G55 walipingwa vikali na baadhi ya watu akiwemo hayati baba wa taifa,mwalimu Julius Nyerere kuhusu madai yao kuwepo muungano wa serikali tatu.Wengi waliwaona ni viongozi wasiofaa na pengine ni watu hatari.
Sasa kwa kuzingatia mapendekezo ya tume hii ya katiba mpya,tunaweza kusema kuwa Njelu Kasaka na kundi zima la G55 waliona mbali kuliko baba wa taifa na hata viongozi wengi wa CCM ya leo?
Madai ya serikali tatu yalianza kabla ya kundi la G55 ila ukweli kundi hili la G55 lilikuwa na msukumo na mvuto wa kipekee katika jamii juu ya jambo hili.
Haya walichotaka akina Sitta enzi hizo za G55 sasa kimetimia......urais wa Tanganyika huoooooooo! Hawa wengine wanaopigana vikumbo kwenye urais i.e. Membe, Lowasa hivi enzi zile za G55 walikuwa upande gani?