Kuna bomu kubwa linatengenezwa mkoani Kigoma, viongozi ombeni msaada?

SUTAGI-

JF-Expert Member
Nov 9, 2018
269
511
Utangulizi.

Rambaramba maarufu kama Kamchape ni vitendo ambavyo vinashika kasi taratibu lakini kwa uhakika sana ndani ya mkoa wa Kigoma soon or later vitalipuka kama bomu na kusababisha maafa makubwa sana.

Ni vikundi vya waganga wa jadi ambao hujihusisha na upigaji wa ramli zenye kusudi la kubaini, kufichua wachawi na washirikina na hatimaye kuharibu uchawi huo. Mkoani Kigoma vikundi hivyo vinafahamika kama KAMCHAPE.

Zoezi la KAMCHAPE lilianza mapema mwaka huu, ambapo waganga hao walipokelewa wilayani Uvinza wakitokea mkoani Katavi. Tangu wameingia mkoani hapa wamezunguka maeneo mbalimbali ya mkoa wakipokelewa na kuhifadhiwa na baadhi ya wenyeji wa vijiji hivyo ikiwa ni pamoja na kupata sapoti toka kwa baadhi ya viongozi wa maeneo husika.

Tetesi za chanzo cha zoezi hilo.

Inasemekana ni agizo kutoka juu kwamba baada ya kiongozi wa juu wa nchi kufanya ziara ya kikazi mkoani Kigoma mwaka jana alikutana na vitimbwi vya wachawi.

Baada ya kufanyiwa ushenzi huo aliagiza kufanyika kwa oparesheni hiyo ya KAMCHAPE. Haijulikana agizo hilo lilitolewa kwa nani na lini japokuwa watu wengi hapa mkoani watakwambia zeozi la KAMCHAPE haliwezi kukoma kwa kuwa linazo Baraka zote toka juu.

Jitihada zilizofanyika kukomesha vitendo hivyo.

Hadi sasa zimekuwepo jitihada mbalimbali zinazofanywa na serikali kupitia viongozi wake wa wilaya na mkoa, Taasisi za kidini na watu mbalimbali katika kukabiliana na janga hilo. Nitaainisha baadhi ya jitihada hizo.

Mwezi julai 2023, Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Salum Kalli aliwaomba viongozi wa Dini pamoja viongozi wa Serikali za mitaa kwa kushirikiana na kamati ya ulinzi na usalama kukemea vitendo vya ramli chonganishi zinazofanywa na waganga wanaojiita KAMCHAPE kwani vinasababisha uvunjifu wa amani kwenye jamii. Mkuu huyo wa wilaya alibainisha kuwa watu watakaobainika kujihusisha na vitendo hivyo watakamatwa na kufunguliwa mashtaka.

Jeshi la polisi mkoani Kigoma limefanya elimu katika maeneo mbalimbali kuhusu madhara ya zoezi la KAMCHAPE na kwa vipindi tofauti wameweza kukabiliana na kuwakamata baadhi ya wananchi waliojihusisha na vitendo hivyo katika vijiji vya Bitale, Ilagala, Kazuramimba, n.k.

Viongozi wa Dini wamekuwa wakiwaasa waumini wao kutokujihusisha na vitendo hivyo vya ramli ambavyo vipo kinyume na misingi ya imani katika dini zao.

Elimu kupitia vituo vya radio imekuwa ikitolewa pia ili kuwaelimisha wananchi kuhusu vitendo hivyo.

Pamoja na jitihada zote hizo zinazoendelea kufanyika, bado tatizo ni kubwa sana kiasi cha kusababisha madhara kwa baadhi ya wananchi wanaotuhumiwa kuwa ni wachawi na wale wanaokataa zoezi hilo.

Madhara yaliyotokana na zoezi la KAMCHAPE mkoni Kigoma.

1. Vifo: Hadi sasa kuna zaidi ya vifo vinne vilivosababishwa na zoezi hilo, Juni, 2023 kijana Nassib Abdalla wa kijiji cha Ilagala aliuwawa katika vurugu zilizotokea kati ya wanaounga na wasiounga zoezi hilo. (R.IP)

Mwezi Oktoba 2023, vilitokea vifo vya watu watatu (3) kijijini Kazuramimba pia katika vurugu kati ya wanaounga na wasiounga zoezi hilo. (R.IP)

2. Uharibifu wa mali – Katika vurugu zilizotokea vijiji vya Kazuramimba na Ilagara hadi kusababisha vifo hivyo viliambatana na uharibifu mkubwa wa nyumba za watu na magari. Mathalani magari 5 ya polisi yaliharibiwa vibaya sana na wananchi wenye hasira kali.

Katika kijiji cha Munzeze, Mheshimiwa Diwani wa kata hiyo iliyopo ndani ya Jimbo la Buhingwe, jimbo analotokea Makamu wa Rais wa Tanzania ndg. Philip Mpango alibomolewa nyumba yake na wananchi wenye hasira kali baada ya kukataa huduma hiyo ya kamchape isifanyike kwake. Katika vijiji vya Kalenge, Kidahwe, Bitale, Matyazo, Nyamugari, Nyachenda, Munyegera n.k watu wamethirika sana wamefyekewa mazao yao shambani.

3. Saikolojia za watu walioathirika na zoezi la kamchape ziko hatarini kukumbwa na matatizo ya akili pia mahusiano katika jamii hizo yamekuwa mabaya na chuki iliyojengwa itaathiri vizazi vijavyo.

4. Uharibifu wa miundombinu ya barabara kama kuchoma matairi barabarani na kuzuia usafirishaji wakati wananchi wakijaribu kuwadhibiti Polisi.

Udhaifu katika kudhibiti vitendo KAMCHAPE.

Kuna udhaifu na hofu kubwa sana katika kudhibiti vitendo hivi kwanza ni kutokana na viongozi katika ngazi za vijiji na kata kushindwa kabisa kuwadhibiti KAMCHAPE, pia upo ushahidi wa baadhi ya viongozi kupata mgao kutokana na shughuli hiyo. Ili KAMCHAPE aje kwako utashinikizwa utoe wastani wa shilingi 5000 au zaidi na wakishagundua kuna uchawi utaambiwa ulipie gharama za kuutoa ambazo si chini ya laki moja.

Hiyo ni fursa kwa baadhi ya viongozi wetu wasiokuwa waadilifu ambayo inahamasisha vitendo hivyo kuendelea

Baadhi ya Polisi wanadai kuwa wanatamani sana kudhibiti zoezi hilo isipokuwa kuna watu walio juu yao ambao wanapenda kuona zoezi hilo likiendelea.

Viongozi wa kisiasa wa mkoa wetu wanasubiri maafa makubwa yakitokea ndiyo wapaze sauti, hadi sasa hakuna Mbunge wa jimbo lolote mkoani Kigoma aliyesimama kukemea vitendo hivyo vya kishenzi.

Ninatumia jukwaa hili pia kumjulisha Rais wa nchi Mheshimiwa Samia Suluhu kuwa anahusishwa na chanzo cha zoezi hili na hali iliyopo sasa mkoani Kigoma ni mbaya, wananchi wananyanyaswa kwa imani za kishirikiana hivyo ni muhimu kwake kutoa kauli ya kukemea au kuhalalisha (kama kweli alitoa agizo hilo) jambo hilo.

Namjulisha homeboy Mheshimiwa Dr. Philip Mpango kuwa asisubiri hali iwe kama ya kanda ya ziwa ya mauwaji ya vikongwe na albino ndiyo atoe kauli ya kukemea vitendo hivyo. Ni muhimu aguswe na vifo vya watu hao ambao tayari wamepoteza maisha kwa sababu tu ya zoezi hilo la KAMCHAPE.

Nina uhakika vyombo vyetu vya ulinzi na usalama vipo active isipokuwa vinachagua matukio yapi ya kuwa active na yapi vifanye kazi kwa mazoea. Katika hili bado hakuna nguvu zozote za dhati zilizowekezwa kupambana na tatizo hili. Mtandao huo ukiachwa utamea na madhara yake yataathiri kila koo ndani ya mkoa wa Kigoma.

Wiki kadhaa zilizopita viongozi wa mkoa walijitetea na kusema kuwa wanalifanyia kazi suala hilo la KAMCHAPE na kwamba wapo watu waliojihusisha na vitendo hivyo wamekamatwa. Ni kweli watu wamekamatwa lakini baada ya hao watu kakamatwa zoezi hilo ni kama limeongezewa nguvu zaidi. Fanyeni ufuatiliaji na tathmini ya zoezi hilo, Je, limekuwa na faida iliyokususudiwa au la?

Nashauri mkuu wa mkoa kama kweli unayo nia ya dhati ya kudhibiti suala hili, weka utaratibu wa kupokea taarifa ya vitenddo hivyo kila siku asubuhi kutoka kila wilaya na wakuu wa wilaya wapokee taarifa kutoka kila kijiji kila siku. Ukifanya hivyo utagundua kuwa zoezi hili limekuwa kubwa kiasi cha kuomba msaada wa ziada katika kukabiliana na vitendo hivyo.

Hitimisho

Nimeandika haya baada ya kushuhudia Mama aliyetuhumiwa kuwa ni mchawi katika kijiji mojawapo hapa wilayani Kasulu chini ya umati wa watu zaidi ya Mia moja akiwa kwake na familia yake akinyolewa nywere zake zote kichwani, akachanjwa chale kifuani na utosini akupakwa dawa na hao KAMCHAPE lakini worse enough mama huyo alipelekwa chemba kwa zoezi la kunyolewa nywere sehemu zake za siri.

Nilisikitika sana lakini sikuwa na namna yoyote maana hao watu wana imani kali sana na wanamuamini KAMCHAPE kuliko maelezo yoyote uyajuayo. Nikiwa bado kijijini hapo zoezi hilo liliendelea na kufika kwa Mzee mmoja ambaye alituhumiwa na KAMCHAPE kuwa ana uume wa kichawi na kwamba ameshafanya mapenzi na kila mwanamke katika kijiji hicho.

Baada ya kuona hayo nilipiga simu Polisi wilayani Kasulu lakini ushirikiano wao ulikuwa mdogo, ni kama zoezi hilo wamelizoea na wanalichukulia kawaida sana japokuwa kwa macho yangu nimeiona chuki kubwa ikipandwa Kigoma! Ni kubwa sana sana zaidi ya mauaji ya vikongwe na albino kule kanda ya ziwa.

Muda wa kuchukua hatua zaidi ya zile zilizopo zinahitajika haraka sana.
 
Kanisa la Chanzo Halisi limezuru Kigoma na viongozi wake wote

Msiogope!

Kamchape Atachapwa yeye
Imani waliyonayo wananchi kwa KAMCHAPE ni kubwa sana.. tunakoelekea siku wakipewa amri ya kuua watuhumiwa wa uchawi watafanya hivyo bila hofu
 
Unaambiwa hao kinakamchape watasaidia kutatua tatizo la umeme
Hata wawaambie watawaletee chakula mezani wananchi wa mkoa huo waliowengi wataacha kwenda kazini wakisubiri hizo neema.
 
Wachawi ni watu wapumbavu sana waache washughulikiwe

Sent from my SM-A013G using JamiiForums mobile app
 
Hao kamchape ningefurahi km wangekuja na huku daslam watu wanaroga sana
 
Pumbafuuu Sana kamchape ni wajinga Fulani wanaleta fujo na chuki... Hata Siku Moja Shetani Hawezi kumtoa Shetani Maana Shetani Ni Baba wa ushetani.. Kigoma Akili Hamna. Wanawachezea mazingaombwe
 
Biblia takatifu inaamini uchawi "mchawi auwawe". Kamchape fanyeni kazi yenu, wachawi ni mashetani. Anaepinga ni yule ambae hajaathirika kichawi. Kuna kiongozi akiwa anahutubia moshi ukatokea wa ajabu!! Ni hao washenzi! "Washindwe na walegee".
 
Kwani tofauti ya bomb kubwa na bomb dogo ni ipi,ninavyo fikiri kitazanwacho ni athari 🤔
 
Biblia takatifu inaamini uchawi "mchawi auwawe". Kamchape fanyeni kazi yenu, wachawi ni mashetani. Anaepinga ni yule ambae hajaathirika kichawi. Kuna kiongozi akiwa anahutubia moshi ukatokea wa ajabu!! Ni hao washenzi! "Washindwe na walegee".
Ndiyo hiyohiyo imesema hukumu ni ya Mungu na si mwanadamu?
 
Elimu elimu elimu vs utamaduni utamaduni.

Inaonekana elimu imeshindwa kuondoa utamaduni wa haya mambo ya imani potovu.
 
Kigoma na kagera ni mikoa yakimkakati kuna mwingiliano mkubwa wa watu wengi wao wahamiaji kutoka burundi,congo drc from kigoma ila bukoba kuna hii mixed race banyankore haya mixed rwanda kwaiyo usishangae ivyo vitu ndio maana wakuu wa mikoa na wilaya katika sehemu. Hizo lazima wawe wanajeshi
 
Viongozi wa Kanisa,wachangamkie hiyo fursa kwa kupanda makanisa mengi huko ili kumvunia Mungu mavuno mengi.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom