- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Hivi ni kweli kuwa kuna watu ambao hutoa nafsi zao ndani ya miili yao (Astral Projection)?
- Tunachokijua
- Kutoka ndani ya mwili (Astral Projection) ni tukio la kiimani ambapo inaelezwa kuwa mtu anatengana na mwili wake kifikra au kiroho, hali hii humfanya mtu kwenda popote duniani kimawazo. Katika tukio hili inaelezwa kuwa roho ya inakuwa imetengana na mwili wa nyama kiimani/ kifikra.
Kutoka ndani ya mwili (Astral Projection) kumekuwa kukifanywa katika tamaduni na dini kadhaa ulimwenguni, style Caster wanabainisha kwamba jambo hili limeanza tangu jamii za kale za Misri lakini pia lilijitokeza kwenye dini ya Kiislam na pia linaendelea kufanyika katika dini nyingine bara la Asia.
Aidha, kwa upande wa Waislam inaelezwa kuwa katika Quran Mtume Muhammad alisafiri kwa mtindo huu kutoka Makka hadi Yerusalemu, na kisha Yerusalemu kwenda mbinguni tukio ambalo Waislam huliita Isra Wal Miraj. Zaidi ya hayo, inaelezwa kuwa Astral Projection inafanywa kwa kiasi kikubwa katika jamii na dini ya Wahindu na Mabuddha barani Asia.
Je ni kweli mtu anaweza kutoka nje ya mwili wake?
Jamiiforums imepitia machapisho ya tafiti mbalimbali tumebaini kwamba zipo nadharia (Imani) kadhaa zinazoamini kuwa ni kweli mtu anaweza kutoka nje ya mwili wake. Wataalamu wa masuala ya ndoto na imani wanaeleza kwamba kwamba mtu anao uwezo wa kuamua kwa makusudi kutoka nje ya mwili wake, na kusafiri na kwenda mbali, mahali popote anapotaka na kurudi ikiwa atafatuata taratibu maalum.
Wataalamu wa Astral Projection wanasema kitendo hicho ni salama na mtu yeyote anaweza kufanya, kinachohitajika ni kuwapo kwa utulivu wa akili wa hali ya juu na uwezo kuulazimisha ubongo ukae katika hali ya kutowaza kitu chochote kwa muda fulani, na kuhakikisha hakuna wasiwasi au hofu yoyote moyoni.
Ili kutoka nje ya mwili wako wataalamu wanashauri kufuata hatua zifuatazo:
- Oga Na Vaa Nguo Safi Zisizo Bana na uende sehemu yenye utulivu isiyo na kelele ya aina yoyote
- Lala Chali Mgongo Ukiwa Umenyooka vema huku umefumba macho.
- Ukipata vishawishi kujigeuza au kujitingisha usivizingatie wala Usijishike wala kujitingisha.
- Usitingishe Macho Wala Kuchezesha Mwili Wako.
- Subiri Na Uconcerntrate Kwenye Pumzi (Hapa unakuwa unaudanganya ubongo kuwa mwili unaota)
- Ukiweza kujizuia Kujigeuza Geuza Au Kujikuna Ubongo Utajua Umelala na Utaruhusu Mwili kuachia kinga ya Paralysis au Ganzi Salama Ya Mwili Mzima ambayo Huwa Inakinga Miili Yetu Kutokujiumiza Wakati wa Kuota Mfano: sleep walking(unaota huku unatembea)
Hivyo, japokuwa wataalamu wamefafanua kwamba jambo hili linawezekana katika ulimwengu wa kiimani na kifikra, jamiiforums suala la kutoka nje ya mwili utalichukulia kama nadharia ya kiimani kwa sababu mawazo yote yanayofafanua jambo hili hayawezi kuthibitika kisayansi.