Kuna wakati yapasa wanawake wafanye maamuzi magumu!

Mtambuzi

Platinum Member
Oct 29, 2008
8,810
15,398

Kuna wakati mwanamke hujikuta akiwa na wakati mgumu asijue la kufanya.....

Wanawake wengi hukabiliwa na matatizo yanayohusiana na mihemko, ukilinganisha na wanaume. Maradhi kama shinikizo la juu au la chini la moyo, kiarusi, kupoteza mwelekeo katika hedhi na sasa kansa. Nasema na sasa Kansa kwa sababu, huko nyuma hakuna aliyekuwa akijua kwamba, kansa kwa sehemu kubwa huchochewa na sononi za kimaisha. Hivi sasa kuna ongezeko kubwa sana la wanawake wanaougua kansa ya matiti na kizazi. Msisistizo mkubwa unawekwa kwenye kupima ili mtu aweze kuwahi kutibiwa. Lakini, hakuna anayejua chanzo kinachopelekea matatizo haya ya kansa.
Wataalamu hivi sasa wanakiri kwamba, kansa kama ile ya kizazi, uvimbe wake hukua haraka zaidi kwa wanawake ambao wanakabiliwa na sononi za kimaisha. Ugunduzi huu unamaanisha kwamba, kuna uhusiano wa karibu wa kibailojia kati ya sononi au huzuni kali na kansa. Kuna ukweli mkubwa kuhusu jambo hili hasa mtu anapopitia tafiti kadhaa zenye kuzungumzia jambo hili. Kwa mfano kuna wanaosema au kuamini kwamba, misukosuko ya kimaisha kama vile talaka au kutelekezwa kunaweza kuwasababaishia wanawake kansa.

Kansa inayotokana na misukosuko hii ya maisha, hujitokeza baadae sana kwenye maisha ya mtu, kwani hukua polepole. Hii ina maana kwamba, misuosuko ya maisha inapomtia mtu katika huzuni kali husababisha kansa, lakini pia huichochea kama ipo tayari. Dr. Anil Sood ambaye amekuwa kifanya utafiti kuhusu maradhi haya, anasema imebainika kwamba, huzuni kali husababisha kansa ya kizazi kukua na kusambaa haraka mwilini kuliko inavyofikiriwa. Hebu tujiulize wote linapokuja suala la mateso ya wanawake kwenye ndoa. Je kuna haja ya kuwasaidia wanawake hao kwa kuwaambia tu kwamba, wana haki sawa na wanaume au tuna haja ya kuwaambia pia kwamba, kukubali kwao kuishi kwenye ndoa za mateso kuna maana ya vifo vyao kabla ya muda? Leo hii kuna idadi kubwa ya wanawake wenye kansa na inaonyesha wazi kwamba, idadi inaongezeka kila siku. Ni nani anajua ni kwa kiasi gani kansa zinasababishwa na kero na misukosuko ya ndoa?

Kuna magonjwa mengi ya moyo na kisukari kwa wanawake wengi leo hii. Ukifanya utafiti mdogo tu utabaini kwamba, akina mama wenye maradhi ya moyo, kisukari, shinikizo la damu na hata kansa, ndoa zao zina au zilikuwa na misukosuko mingi. Nadhani sasa imefika muda ambapo wanawake wanapaswa kuujua ukweli mkubwa zaidi kuhusu maisha yao ya ndoa na afya zao, lakini na uhai wao kwa ujumla. Pengine wanawake wengi hawajui kwamba, kwa kuendelea kuishi kwenye ndoa zenye huzuni na sononeko, wapo hatarini kupata matatizo makubwa ya kimaradhi kama vile kansa. Hii ina maana kwamba, idadi ya wanawake wanaokufa kwa mwaka kutokana na mateso ya ndoa ni wengi sana kuliko inavyofikiriwa……

OMBI:
Naomba Mods msiihamishe hii mada kwenye jukwaa la JF Doctor kwa sababu mada hii inawahusu sana wanandoa……………
 
Mkuu umeona lakini kifio cha huyo mwanamke ni saa yaukutani lazima igonge kwa sauti.

Tunarudi kwenye thread, nakubaliana na hii thread wanawake wengi wanapta hayo maradhi sababu ndoa zao niza usumbufu sio wanaume wote wanao jua thamani ya wanawake.
 
Khaa noma!! Lakini jinsia hii kuolewa wanaita bahati, ningewashauri wasichana wazingatie sana masomo ili wajikomboe kiuchumi, kwani wanawake wengi ambao wanang'ang'ania kuishi kwenye ndoa zenye misukosuko ni wale ambao hawana uchumi (tegemezi).
 
Pengine wanawake wengi hawajui kwamba, kwa kuendelea kuishi kwenye ndoa zenye huzuni na sononeko, wapo hatarini kupata matatizo makubwa ya kimaradhi kama vile kansa. Hii ina maana kwamba, idadi ya wanawake wanaokufa kwa mwaka kutokana na mateso ya ndoa ni wengi sana kuliko inavyofikiriwa……

Ahsante kwa maelezo yako....ukweli wanawake wanapata masaibu mengi kuliko yale ya wanaume na yote hayo yanakuwa very much involved with emotional and feelings unlike men. Ni wajibu wanawake wajue when to call it a quit however, it needs change in the whole society. Huku kwetu ukiwa umeachika/umeachana na mumeo bila watu kutaka kujua kwamba ile ndoa ilikuwa ya mateso, tayari conclusion is made for you, kuwa mwanamke ni mpuuzi kwa kuiharibu ndoa yake.

In some cases its shame to be called divorcee, imefikia kiwango kuwa mwanamke anajua fika kuwa mume wake anatembea na nani na wapi na kimada gani but choose to remain silent cause akianzisha zogo itaishia kwenye kuachana, na zaidi adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie either nyumba ndogo au mama mkwe na mawifi.

I think its time we start to change our thinking towards this woman inorder to save her!
 
MadameX adui wa mwanamke ni mwanamke mwenyewe, swala la mwanamke kuonekana kituko baada ya kuachana na mumewe kamwe halitazungumzwa na wanaume bali na wanawake wenyewe, wakimsimanga mwanamke mwenzao aliyachika, tena wakiwemo wale waliochangia kuvuruga ndoa hiyo.
Ndio maana nimesema, mwanamke ana uchaguzi, aidha kuvumilia ndoa ngumu, lakini akitarajia kufa mapema au ajiondoe ili kunusuru hali ya mambo na kujenga maisha yake upya. kila mtu amezaliwa peke yake na kulelewa peke yake, ndoa huwaunganisha watu ukubwani kila mtu akiwa na utashi wake, iweje sasa mtu ajione kuwa hawezi kumudu kuwa peke yake ilhali alizaliwa peke yake.
Sihamasishi wanandoa kuachana, lakini ninachosema hapo ni kwamba kuna wakati yapasa wanawake wafanye maamuzi magumu............
 
Last edited by a moderator:
Ahsante kwa maelezo yako....ukweli wanawake wanapata masaibu mengi kuliko yale ya wanaume na yote hayo yanakuwa very much involved with emotional and feelings unlike men. Ni wajibu wanawake wajue when to call it a quit however, it needs change in the whole society. Huku kwetu ukiwa umeachika/umeachana na mumeo bila watu kutaka kujua kwamba ile ndoa ilikuwa ya mateso, tayari conclusion is made for you, kuwa mwanamke ni mpuuzi kwa kuiharibu ndoa yake.

In some cases its shame to be called divorcee, imefikia kiwango kuwa mwanamke anajua fika kuwa mume wake anatembea na nani na wapi na kimada gani but choose to remain silent cause akianzisha zogo itaishia kwenye kuachana, na zaidi adui wa mwanamke ni mwanamke mwenzie either nyumba ndogo au mama mkwe na mawifi.

I think its time we start to change our thinking towards this woman inorder to save her!

....................
 
kweliiiiii jamani ni wakati wa serikali kuweka kanuni za ndoa wanaume wanaitaji shule ya kuishi na wake zao kwani wazazi wamegeuza kibao wanaangalia pato la kijana kuliko maisha yake hata kama wanaona mwanao anatesa mke na watoto hawasemi neno wamekuwa watumwa wa pesa kuliko watoto wao jamani
 
Siku hizi napata shida kidogo kujua kama mabinti wanavutiwa na kitu gani wakati wa kuchagua mchumba.......
Zamani najua ilikuwa wanaangalia zaidi mpenzi ambaye yuko responsible na shujaa wa familia, mwenye mapenzi kwa watoto na mengine yanayofanana na hayo, lakini siku hizi sifa kubwa inayotajwa ni fedha.....................
 
DUH hii inaogopesha jaman, kweli kuna haja ya kufanya maamuz magumu ingawa tatzo ni kuwa waathirika wakuu wa hili walio wengi hawana habari kuhusu hili na hawana namna ya kupata habar hz.
 
Siku hizi napata shida kidogo kujua kama mabinti wanavutiwa na kitu gani wakati wa kuchagua mchumba.......
Zamani najua ilikuwa wanaangalia zaidi mpenzi ambaye yuko responsible na shujaa wa familia, mwenye mapenzi kwa watoto na mengine yanayofanana na hayo, lakini siku hizi sifa kubwa inayotajwa ni fedha.....................

kweli kuna kazi Mtambuzi vipi kuhusu wazazi kuchangia kuharibu kwa kuwa watumwa hawawezi simama na kusema neno anaogopa atakatiwa maji au umeme nani atalipa
 
Mtambuzi uchunguzi wangu umebaini kansa hasa ya shingo ya uzazi inasababishwa na zinaa tu hakuna cha kuaathirika kiisaikolojia.............
 
Last edited by a moderator:
:A S cry:tobaaaaaa yailahiiiii.........
nijipange rasmi nitoe divorce maana my marriage is irretrievablly broken!!!!

Yanini magonjwa haya kama unaweza kujiweka pembeni!!!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom