mtoto mdogo sana
JF-Expert Member
- Apr 16, 2020
- 460
- 1,338
Habarini za uzima. Mimi sijambo pia. Kama afya yako haiko katika utimilifu basi Mwenyezi Mungu akujaalie nafuu ya mapema ujisikie kupona.
Moja kwa moja kwenye mada.
Baada ya maisha yangu kuchukua sura mpya kwa Mwaka mmoja sasa, jana nimepata nafasi ya kujitathmini kujua iwapo niko sawasawa na jamii inayoishi kawaida.
Kwa uchache tu ni kuwa kutokana na changamoto za maisha zilizonikumba kuanzia wakati nikiwa mdogo sana, kuna Mambo hata mimi nilikuwa sijifahamu. Kuna baadhi ya matendo niliyokuwa nikiyafanya zamani nikijiaminisha kuwa hali ya kukosa mahitaji na kuishi mazingira hatarishi ndiyo iliyochangia kufanya baadhi ya maamuzi.
Kwa mfano, ilifika wakati fulani nikiwa mtaani, nikishikwa na njaa na sina ramani kabisa ya kupata chochote au popote pa kwenda kula nilikuwa nakaa chini naandaa mpango wa kwenda kuiba. Mimi na wenzangu (wa mtaani). Sasa ilifika wakati nikatoka katika hali ya kuwa mtoto wa mtaani. Nikapata bahati ya kwenda kusoma shule. nikiwa shule sikuwahi kuiba, ila nilikuwa mtu mwenye hofu na kujishtukia siku zote. Kila muda nilijiuliza rohoni iwapo wizi ni tabia yangu au ilitokea tu kutokana na kukosa chakula. Hali ya uchangamfu na kuongea na watu iliniondoka mara moja kila wakati mawazo hayo yalipokuja.
Ule ukimya na kutozungumza na watu mara nyingi, ukizingatia pia nilikuwa na akili darasani basi nikapata sifa ya mtoto mwenye busara, mkimya, mtulivu, kipanga na mengine mazuri. Wakati wote sifa zote hizo hazikuwahi kunifanya nijisamehe hatia ile ya kuwahi kujihusisha na wizi (Japo wizi ulikuwa ni small scale 😁😁) Kwa mimi nilivyo, najijua kabisa sio mkimya, ila nikiamua, nakua mkimya na nakuwa mkimya kabisa tena sio ukimya wala ustaarabu wa kuigiza, nakuwa kweli mstaarabu. Ila nikiingia mazingira ambayo yatanitaka niongee, nizungumze sana basi utanishangaa... maneno yatanitoka kama vile nimezaliwa pwani. naongea kwelikweli.
Basi watu ambao niko nao karibu nadhani wanashindwa kunielewa kwa kuwa mimi attitude zangu ni periodically. Wasionizoea huwa wananilaumu baadhi ya wakati kuwa nawanyamazia, lakini sio, tatizo sijajua mimi ni wa aina gani. mcheshi au mkimya. Sijui
Akili yangu huwa inazunguka kwa spidi sana nikiwa kwenye hali ya utulivu ila kama nikiwa na watu, huwa inabidi nikae nao kulingana na wanavoamini uwa pace ya akili na maamuzi ya mtu wa aina yangu inapaswa kuwa.
Sasa kuna wakati tena najishtukia kuwa hivi naigiza maisha au naishi maisha yangu? Kama ni maisha yangu, mimi ni mtu wa aina gani? mkorofi au mstaarabu, maana yote najua nayaweza.
Hili jambo linanikosesha sana kujiamini.
Yaani najijua kabisa sina tamaa wala nia ya kuiba chochote ila mtu anapozungumzia wizi yaani mimi huwa sina amani. Natafunwa sana na hatia fulani rohoni.
Mbaya zaidi sasa, mtu akinituhumu, au akihisi pengine naweza kumuibia au kudokoa kitu. Yaani hapo siwezi kujisamehe nafsi yangu. nitatengeneza theory nyingi sana nikivaa viatu vya wanaonitazama nijue wananionaje, nikizungumza, navoishi, navotembea. Basi ilimradi tu, sina amani. Nilishawahi kupata kazi sehemu... nilifanya kazi kwa mapenzi yote, kwa kuipenda na kujituma, hata ikanibidi kufanya muda wa ziada. Ila mawazo ya kuiacha kazi husika yalianza siku ambapo ofisi fulani ilitokea uharibifu na mtu akawa ame-misplace kitu. Mimi nikawa mmoja kati ya waliohojiwa - For good. Nakumbuka nilikuwa nikikaa peke yangu nalia mno. Mimi huwa nalia sana mara nyingi usiku nikilala. Basi nilikaa kwa maumivu hayo, kwa hatia ya jambo nisilofanya, nina tatizo la madonda ya tumbo.... yakazidi nikawa hata kuamka asubuhi kwenda kazini ni tabu.
Ile hatia ilipelekea niiache kazi yenyewe nikaishi maisha mengine.
Sijui wengine huwa wakoje ila mimi binafsi, sijawahi kuhua ni wa namna gani. Niliwahi kuambiwa na mtu "wewe mtoto mdogo sana you are very sensitive" nadhani alikuwa sahihi.
Hivi nyie wengine huwa mnawezaje kuishi maisha mengine ya kawaida bila kufuatwa na majinamizi ya maisha mliyoishi zamani?
Nawasilisha