Kuna umuhimu wakujua jinsia ya mtoto ukiwa mjamzito

Akili Unazo!

JF-Expert Member
Feb 18, 2009
3,930
4,893
Wakuu kuna hii tabia ambayo sijui kama ni utandawazi au tunakiuka mila na desturi za Kitanzania.

naomaba mnisaidie hivi kuna umuhimu wowote wa kujua jinsia ya mtoto ukiwa mjamzito?
 
Hii mimi naona haina umuhimu wowote zaidi tu ya kuongeza mtafaruku tu katika nyumba nyingi.

Sasa ukikuta ni wa kike na wewe ulitaka wa kiume utafanyaje hapo?

Ni mtizamo tu.
 
Kuna hospitali moja hapa mkoaniTanga waliiambia familia fulani jinsia ya mtoto wao aliyeko tumboni, amini usiamini, siku ya kujifungua alizaliwa mtoto wa tofauti na taarifa ya daktari!

Wale wazazi walipigwa na butwaa sana, maana walishafanya maandalizi ya jinsia waliyoambiwa!

Sasa madhara mengine mabaya zaidi yanaweza kuwa ni ya kisaikolojia, ambayo yanaweza kuwaathiri mtoto pamoja na wazazi!
 
Mimi binafsi sioni umuhimu wake. Tunajuwa kuwa mtoto ni zawadi toka kwa muumba. Na naamini kabisa kuwa zawadi nzuri ni ile inayokuwa suprise kwako.
 
Kuna hospitali moja hapa mkoaniTanga waliiambia familia fulani jinsia ya mtoto wao aliyeko tumboni, amini usiamini, siku ya kujifungua alizaliwa mtoto wa tofauti na taarifa ya daktari!

Wale wazazi walipigwa na butwaa sana, maana walishafanya maandalizi ya jinsia waliyoambiwa!

Sasa madhara mengine mabaya zaidi yanaweza kuwa ni ya kisaikolojia, ambayo yanaweza kuwaathiri mtoto pamoja na wazazi!

Inawezekana huyo daktari hakuwa makini, alitakiwa kutoa tahadhari kwamba matokeo yanaweza kuwa tofauti. Mara nyingi kinachoangaliwa ni dalili za male genetalia za foetus. Kama zipo, watasema chance kubwa ni mtoto wa kiume, kama hazionekani watasema chance kubwa ni mtoto wa kike.

Huwa inatokea mara kadhaa hizo male genitali zikawawepo lakini zisionekane kwenye kipimo na hivyo kupelekea mpimaji kudhani mtoto wa kike atazaliwa.

Sijui kwanini watu wanakuwa na haraka kutaka kujua, binafsi naona inapendeza kusbiri mpaka mtoto azaliwe.
 
Inawezekana huyo daktari hakuwa makini, alitakiwa kutoa tahadhari kwamba matokeo yanaweza kuwa tofauti. Mara nyingi kinachoangaliwa ni dalili za male genetalia za foetus. Kama zipo, watasema chance kubwa ni mtoto wa kiume, kama hazionekani watasema chance kubwa ni mtoto wa kike. Huwa inatokea mara kadhaa hizo male genitali zikawawepo lakini zisionekane kwenye kipimo na hivyo kupelekea mpimaji kudhani mtoto wa kike atazaliwa.

Sijui kwanini watu wanakuwa na haraka kutaka kujua, binafsi naona inapendeza kusbiri mpaka mtoto azaliwe.

Nashukuru sana kwa michango yenu niliweka hii mada kutokana na mwanaJF mmoja kutoa thread inayosema kuwa ana mimba ya mapacha.

Wengi wamempa hongera na kumshauri aende na kufuata ushauri wa Dr.Jamani tuwe tunashauriana pale ambapo kuna madhara.

Sasa kwa hili jibu la ndugu yangu SMU hatuoni kuwa ndugu yetu aliyekwisha tangaza kuwa ana twins ikijatokea hana hao watoto itakuwaje?
 
Watoto ni zawadi.Je ni ustaarabu kutafuta kujua utaletewa zawadi gani?..hadi ukafunuefunue, upekue ili tu ujue hili box lililofungwa vizuri au vibaya, ndani kuna nini? Haileti tena ile raha maana tayari unajua kilichomo, na si ajabu kilichomo wewe unacho na ulitaka kitu kingine! Haya mambo ya kujua tumboni kuna nini yamepelekea kwa mfano huko India na kwingineko watu kutoa mimba za watoto ambao hawawataki.

Mimba za watoto wa kike zimepata dhahama sana kwenye hili.Kuna wenye kuhalalisha kujua ili ati wajiandae! Kwani huko nyuma watu walifanyaje? Kama ni nguo, vitoto vichanga vyote vina mahitaji almost sawa - unaweza kununua nguo unisex kwa maana ya rangi ambazo ni neutral hadi utakapojifungua ndio uanza sasa kutofautisha kwa rangi na style.

Kwenye mapacha, wakati mwingine ni madaktari wanakuambia kuwa una mapacha kwa maana kuna viashiria na pia mimba za mapacha zinahitaji uangalizi zaidi.Hivyo hata bila wewe kutaka kujua kuna nini tumboni, utaambiwa.
 
mh... mie napenda kuchungulia, haya mambo huanza kuangalia kama mtoto yu salama na hali ya mama ni healthy, ila inafika sehemu sonologist anakuuliza vipi tuangalie zaidi, and it gets exciting... so i have liked the idea na ninaenjoy kuangalia

Its better, reduces surprises na ikitokea majibu tofauti, unamshukuru mungu
 
Mie hata sitaki wanambia labda kiafya kama mimba iko salama, mtoto amekaa vizuri basi lakini kujua hayo mengine haina haja
 
Mh! mie napenda kuchungulia, haya mambo huanza kuangalia kama mtoto yu salama na hali ya mama ni healthy, ila inafika sehemu sonologist anakuuliza vipi tuangalie zaidi, and it gets exciting, so I have liked the idea na ninaenjoy kuangalia.

Its better, reduces surprises na ikitokea majibu tofauti, unamshukuru mungu

Nimekupa thanks kwa bahati mbaya ;)am kidding MTM
 
Mi naona hakuna haja kwani kufanya hivyo kwaweza sababisha kuingia katika mambo ya kuanza kutoa mimba kama mtoto aliye tumboni ni wa jinsi usoitaka, kwani kutoa mimba kumekatazwa sana katika dini zetu.
 
Haina maana kujua ama kutojua, kujua si vibaya kama watu wanpenda kujua, ni sawa na vyumba vya kujifungulia, siku hizi na wanume wanaingia kushuhudia wake zao wakijifungua wakati zamani haikuwa hivyo, ni mabadiliko tuya nyakati

Muhimu mpokee mwanao kwa moyo shukrani. Mabadiliko mengine hayazuiliki, itafika mahali, utake usitake utaambiwa. so get prepared na mabadiliko
 
Haina maana kujua ama kutojua, kujua si vibaya kama watu wanpenda kujua, ni sawa na vyumba vya kujifungulia, siku hizi na wanume wanaingia kushuhudia wake zao wakijifungua wakati zamani haikuwa hivyo, ni mabadiliko tuya nyakati

Muhimu mpokee mwanao kwa moyo shukrani. Mabadiliko mengine hayazuiliki, itafika mahali, utake usitake utaambiwa. So get prepared na mabadiliko

Wakati wa mabadiliko ukifika tutaupokea tu mgombea ubunge ila mie siendi kwenye utra sound eti nijui nina mtoto gani ..
I don't feel like
 
Wakati wa mabadiliko ukifika tutaupokea tu mgombea ubunge ila mie siendi kwenye utra sound eti nijui nina mtoto gani ..
I don't feel like

Binafsi nalichukulia kama utashi binafsi. Nina 3 boys na tangu mtoto wa 2 tulikuwa tunafanya ultrasound na kuambiwa sex ya mtoto. Tulitamani sana kupata mtoto wa kike lakini hatukubahatika. Kitendo cha kupata majibu mapema kulitusaidia sana kujiandaa kwani wife alikuwa na hamu sana ya baby girl. Kwa hiyo alijiandaa mapema kupokea boys wake. Kwa upande wangu sioni ubaya wowote.
 
Hongera sana dark city hope unafurahia watoto na familia yako kwani mtoto ni mtoto. Na hao madume wakianza mavurugu na michezo hadi raha ..;)
 
hongera sana dark city hope unafurahiA watoto na familia yako kwani mtoto ni mtoto
Na hao madume wakianza mavurugu na michezo hadi raha ..;)

FL1 kwa kweli tunafurahia sana. Vurugu iko juu lakini ndiyo faraja yetu. Ni kweli kwamba tunamiss pink nyumbani. Kuna wakati wife anataka kuchanganyikiwa, hadi ananunua nguo za kike na kuwapatia ndugu zake wenye girls. Hata hivyo tunamshukuru Mungu kwa kuwa boys wanaendelea vizuri. Tunawafundisha kufanya kazi zote za home. Ukizingatia baba yao ni mtu wa home kwa sana.

Tukirudi kwenye hoja; kitendo cha kujua mapema kilitusaidia sana kujiandaa na kimeendelea kutupa nguvu. Na kubwa zaidi kuondoa mawazo na kutupilia mbali ushauri wa baadhi ya ndugu na washikaji kwamba tujaribu tena ili kupata baby girl. Lakini kama mtu hawezi kuhimili msongo na kukabiliana majibu hana sababu ya kufanya ultra sound labda kwa sababu za kitabibu!
 
Wakuu kuna hii tabia ambayo sijui kama ni utandawazi au tunakiuka mila na desturi za Kitanzania.

naomaba mnisaidie hivi kuna umuhimu wowote wa kujua jinsia ya mtoto ukiwa mjamzito?
Hatukiuki mila tekinolojia imesaidia leo twaweza juwa jinsia ya mtoto kabla hajazaliwa.Enzi zile za zamani ambapo tekinolijia ilikuwa finyu hata ambao si wtz hawakuweza kujua jinsia ya mtoto.
Hivyo hakuna ubaya kujua jinsia ya mtoto kabla hajazaliwa.
 
Mimi naona haina umuhimu hata kidogo kwa sababu huwezi badilisha jinsia ukijua mtoto wako si wajinsia ambayo ulikuwa unataka. Halafu watoto ni zawadi toka kwa Mungu inapendeza ukiwa hujui mpk akitoka.
 
Back
Top Bottom