Kuna siri gani kwenye mpira wa miguu?

Hakuna sehemu wala andiko ndani ya vitabu vya dini linalo haramisha mpira, bali uharamu unakuja jinsi huo mpira unavyo endeshwa.

Mfano kulima sio dhabi lakini kwenye kulima kwako ukitumia mambo ya kushirikiana ili upate mavuno mengi tiyari hicho kilimo chako ni haramu lakini haimaanishi watakao nunua na kula hayo mazao yako wata pata dhambi.
 
Dini gani inakataza mpira? Kuna mstari wowote kwenye vitabu vya hizo dini unakataza? Leta ushahidi.
Dini haikatazi ila inaitwa "Laghawi" au "Upuuzi"
Ni kitendo mtu akilifanya hapati dhawabu Wala hapati dhambi ila akizidisha anaelekea ktk madhambi na madhara kwake ,
Mfano mpenzi wa mpira anaweza kumiss ibada,kuumia,kupoteza simu,kuibiwa,stress n.k just Kwa ushabiki.
 
Mpira ni biashara ya mabilioni na biashara mbalimbali kama pombe,kamari, utalii ,ndege,magari n.k
Imeandikwa Pepo imezungukwa na mambo magumu ,mfano kusoma ,kazi halali n.k
Na moto umezungukwa na mapambo na anasa nyingine za kuvutia.
Je, mpira unauweka katika kivutio gani?
 
Hiyo sio dini hiyo ni common sense. Too much of anything is harmful hata maji ni uhai ila yanaua as well. Nayo maji yamekatazwa?
 
Inaonekana Mungu wako anapenda uteseke usifurahie maisha.
 
Hiyo sio dini hiyo ni common sense. Too much of anything is harmful hata maji ni uhai ila yanaua as well. Nayo maji yamekatazwa?
Nadhani maelezo yamejitosheleza.
Unauliza swali la kitoto wakati una jibu tayari.
Nipe kipimo Cha too much na too little?
Nikupimie Kwamba too little ya mpira ni Upuuzi.
 
Dini mbalimbali zinapinga mpira wa miguu na kusema ni satanic
Mkuu hebu naomba unisaidie hapa, ni nini hasa ambacho dini zinapinga kuhusu mpira?

Je ni kuangalia mpira? Au kucheza? Au kushabikia?

Hebu tuweke sawa hapa, maana kwenye in hili umeongea kiujumla sana.
 
Nadhani maelezo yamejitosheleza.
Unauliza swali la kitoto wakati una jibu tayari.
Nipe kipimo Cha too much na too little?
Nikupimie Kwamba too little ya mpira ni Upuuzi.

I'm not even a believer ila unachoongea is just common sense tatizo lenu wafia dini kila kitu mnadhani ni dhambi.
 
Ni
Mkuu hebu naomba unisaidie hapa, ni nini hasa ambacho dini zinapinga kuhusu mpira?

Je ni kuangalia mpira? Au kucheza? Au kushabikia?

Hebu tuweke sawa hapa, maana kwenye in hili umeongea kiujumla sana.
Mpira ni ulevi kama pombe Kuna wanaolewa Kwa bia Moja na Kuna wengine mpaka kreti Moja.
Pombe pia wanatengeneza alcohol free yaani utakunywa haulewi yaani ligi za mchangani .
 
vipi kuhusu basketball, Boxing n.k?
Kwenu wajinga kila kitu kizuri ni cha shetani, mnataka kutuambia kuwa Mungu muweza wa yote ni Mungu wa vitu vibaya tu visivyovutia!?
Ujinga ni kipaji.
Lini shetani akawa na vitu vibaya? Vitu vizuri ndio milki ya shetani ukimsujudia anakupa. Hiyo mipira mingine basketball ni madhehebu tu ya ibada za sanamu, mkiambiwa ukweli mnachukia na kuishia kutukana
 
Ukubali usikubali mpira ni ibada ya sanamu viwanja vinajaa pomoni kuliko nyumba za ibada ya Mungu. Mpira umekuwa ni kiungo muhimu kuunganisha watu mbalimbali kuliko dini zilizozoeleka. Kila kona watu watu wanaongelea mpira. Mpaka wanawake wameingizwa huko tena wanaucheza katika haiba ya kiume kiasi cha kuwa kama wanaume huku wakiachana na haiba ya kike ambayo ni asili yao. Hata kuolewa kwao ni shughuli pevu, watafanyaje mapenzi wakiwa na haiba ya kiume kama si kuwa wapenzi wa jinsia moja? Mpira unatumika kupitisha ajenda mbaya za kishetani na hili lipo wazi linaonekana kuwepo kwa bendera ya kuunga mkono kampeni za mapenzi ya jinsia moja kwenye mchezo wa mpira.

Mkuu! Nadhani inabidi ukae chini uanze kutafakari upya. Punguza kidogo mihemuko.

Hakuna sehemu ambayo shetani hapitishi agenda zake. Nakeambia hivi, haipo na haitakuwepo. Na maandiko yanathibitisha hilo.

Achana na mpira kwanza, twende makanisani kwetu ambako ndiko tunakutana mara kwa mara kumwabudu Mungu. Je, unafikiri huko shetani anakuogopa? Kwamba hafiki? Yupo na anaendelea kupenyeza agenda zake.

Huoni makanisa yanavyoshambuliwa? Huoni mafundisho ya uongo yanavyopyenyezwa makanisani?

Hata kwenye mpira, ambako kuna mkusanyiko wa watu wengi, shetani hawezi kukuacha salama. Maana mtaji wake wa kwanza ni watu.

Yaani kila sehemu yenye mkusanyiko wa watu huo ni mtaji wa shetani kuanzia. Wewe huoni huko ofisini kwako kukoje? Utakuta yanaongelewa masuala ya ngono tu mda mwingi.

Yaani hata wale watu wanakusanyika kufanya kazi ngumu vipi, kama kubeba zege nk, wakishapumzika tu unaona story za ngono na starehe nyingine zinapita. Shetani hawaachi watu wapumue.

So, Ibilisi yupo kila sehemu. Mpira ni sehemu ya mkusanyiko kama ilivyo mikusanyiko mingine. So ibilisi ni dhahili agenda zake zitapitia hapo pia.

Ambacho kinatakiwa ni kwa kila mtu kuwa na uelewa binafsi wa kushinda hoja nyingine za shetani. Mimi ninachokitaka ni mpira wenyewe, yaani zile dakika 90 za kuupiga mpira. Na sio mambo mengine ambayo yako associated na mpira.

Na ninavyoandika hivi, simaaishi namtukuza ibilisi shetani. Hapana. Naonyesha mbinu zake na namna ya kuendelea kumpinga.

Ubarikiwe.
 
Ni
Mpira ni ulevi kama pombe Kuna wanaolewa Kwa bia Moja na Kuna wengine mpaka kreti Moja.
Pombe pia wanatengeneza alcohol free yaani utakunywa haulewi yaani ligi za mchangani .
Sawa, sasa nambie nini exactly kinazuiliwa au kinapingwa na hizo dini?
 
Kama unaaamini kua Mpira ni ibada ya Kishetani kwanini upo kwenye Jukwaa La Sports hapa Nenda Jukwaa La Dini huko.
natembelea majukwa yote kusawazisha mambo. Naona wafuasi wa dini mpya ya mpira mnanitolea povu kwa kuwachana na hiyo ibada ya sanamu iliyowateka mpaka mnaingiziwa ajenda zisizofaa mtakubali tu mtake msitake
 
Msiwe wabishi enyi mashabiki wa mpira muwe wachunguzi wa mambo kutaka kujua ukweli. Kasomeni HOW THEY STOLE A GAME
 
Back
Top Bottom