Dr. Chapa Kiuno
JF-Expert Member
- Sep 11, 2009
- 443
- 18
Wadau, leo asubuhi wakati natokea nyumbani kuja kazini katika daladala niliyopanda kulikuwa na ugomvi kati ya kondakta na mwanafunzi. Ugomvi huu ulihusu kitendo cha mwanafunzi kugoma kusimama ampishe mtu mkubwa akae n hiyo ilifuatia baada ya mwanafunzi yule kumuahidi akiwa chini kuwa angelipa nauli ya mtu mzima hivyo asimzuie kupanda n mambo yalibadilika mwanafunzi yule wa kike wa Kisutu galz kugoma kunyanyuka kwenye kiti n pia kulipa pesa ya mtu mzima. Ugomvi ukaanza huku konda akimtaka asimame ili ampishe mtu mzima lakini binti yule akagoma.
Je, kuna sheria inayosema mwanafunzi AKAE au ASIMAME?
Nisaidieni kwa hilo.
Je, kuna sheria inayosema mwanafunzi AKAE au ASIMAME?
Nisaidieni kwa hilo.