LEARNED BROTHER
JF-Expert Member
- Mar 7, 2012
- 548
- 735
Wakuu, huduma ya M-KOBA inayotolewa kupitia kampuni ya mawasiliano ya VODACOM imekuwa maarufu miongoni mwa watumiaji wake hasa makundi ya watu wenye malengo mbalimbali kama vile kusaidiana katika masuala mahsusi n.k. Hata hivyo, katika siku za karibuni kupitia makundi sogozi ya "whatsapp" imeonekana kuna shida.
Kumekuwa na uvumi kuwa pesa zilizohifadhiwa ni kama zimeibwa au kumekuwa na shida kwa wahusika kuzitoa au kupata "statement" ya salio la kundi.
Leo, nimesikiliza "voice note" ikieleza changamoto hiyo, na baadaye usiku huu nikaona tena meseji ifuatayo:-
"Jamani habari
Nasikia M-KOBA imeibiwa hela huko Vodacom
Mlio na M koba hebu checking balance zenu
Nasikia wafanyakazi wa Voda ndio wameiba,
Vikundi vinalalamika ukiuliza. Balance hupati,"
Binafsi ni mwanachama wa makundi mawili ambayo tumehifadhi pesa zetu kwenye M-KOBA. Kundi la kwanza tuna salio 15 mil, na jengine tuna salio 9 mil.
Baada ya meseji za "alert", usiku huu nimejaribu kuomba taarifa ya salio la fedha kwa makundi yote lakini sijajibiwa. Hali hiyo imenipa mashaka, na nimewashirikisha wenzangu nilionao kindini.
Aidha, nimeona ni vyema pia jambo hili nililete humu jamvini ili kupata taarifa zaidi ikiwezekana toka kwa wahusika wenyewe, au kutoa hadhari kwa wengine watakaoguswa.