Kuna nchi nyingine ambayo inawajengea/inawapa nyumba viongozi wake wakuu wakitoka madarakani?

Fundi Mchundo

Platinum Member
Nov 9, 2007
8,943
6,863
Ningependa kujua kama kuna nchi nyingine ambayo inawajengea/inawapa nyumba viongozi wake wakuu wakitoka madarakani?

Na inawapa magari mapya ambayo kila baada ya miaka mitano wanapewa mengine mapya ( sijui tamati ya yale ya awali). Uhuru amepewa nyumba?

Amandla...
 
Huo utaratibu upo nchi nyingi.
Usichokijua kingine ni kwamba Raisi mstaafu bongo hii anapewa monthly 80% his pensionable salary.
Anapewa entertainment allowance. Two personal secretaries, Four messengers, office space, two drivers, moja wake mwingine mke wake.
Home workers to 34 including dobi, mtu wa bustani, full medical cover, full furnished office inatengewa pesa ya uchakavu kila mwaka.

Raisi mstaafu anapewa gari nne sio moja, VXR Land Cruiser yeye na mke wake kila baada ga miaka minne. Mpya kwenye karatasi zake.
Mwinyi anawake wawili kila mmoja anapewa gari na mpambe and other perks including Mafuta, vipuri na matengenezo under tax payers expenses.

Unapoambiwa keki ya taifa uwe unajua ni ya wateule.
 
Huo utaratibu upo nchi nyingi. Kenya upo. Hata Obama alipewa nyumba baada ya kustaafu. Viongozi ndio wanafaidi kodi mzee.

Rais mtaafu wa Kenya anapewa house allowance na sio nyumba. Ila anajengewa ofisi. Angalia hapa: http://kenyalaw.org/kl/fileadmin/pdfdownloads/Acts/PresidentialRetirementBenefitsAct_No11of2003.pdf
Pension and other benefits of retired Presidents
A retired President shall, during his lifetime, be entitled to— (a) a lump sum payment on retirement, calculated as a sum equal toone year’s salary for each term served as President; (b) a monthly pension equal to eighty percent of the monthly salarycurrently paid to the President; (c) an entertainment allowance of two hundred thousand shillings permonth; (d) a housing allowance of three hundred thousand shillings per monthto cater for both an urban and a rural dwelling; (e) suitable office space, not exceeding one thousand square metres,with appropriate furniture, furnishings, office machines, equipmentand office supplies, to be provided and maintained by theGovernment;
two new cars of the retired President’s choice, replaceable everythree years, each car having an engine capacity not exceeding threethousand cubic centimetres; (g) two four-wheel drive motor vehicles of the retired President’s choice,replaceable every three years, each vehicle having an enginecapacity of three thousand, four hundred cubic centimetres; (h) a fuel allowance of two hundred thousand shillings per month; (i) an allowance of three hundred thousand shillings per month forelectricity, water and telephone facilities; (j) full medical and hospital cover, providing for local and overseastreatment, with a reputable insurance company for the retiredPresident and his spouse and his children under the age of eighteenyears; (k) the additional benefits set out in the Schedule.

Rais wa Marekani hapewi nyumba. Obama baada ya urais alihamia kwenye nyumba ya kupanga Washington. Trump anaishi kwenye nyumba take Mar-a-Lago. George W alihamia kwenye nyumba yake Texas.

Mafao ya Rais mstaafu wa Marekani ni kama ifuatavyo:
  • Office Space and Staffing Allowances: Starting six months after a President leaves office, the General Services Administration (GSA) provides funding to establish, furnish, and staff an official office anywhere in the U.S.
  • Travel Expenses: Chief Executives and up to two staff members are reimbursed for up to $1 million in costs annually. Spouses of former Presidents also are eligible for up to $500,000 per year for security and official travel.
  • Health Benefits: Provided that they had been enrolled in the Federal Employees Health Benefits program for at least five years, former Presidents are eligible for health annuities, similar to all federal employees. (Jimmy Carter is ineligible because he only served a single term and did not hold another federal position.)
  • Funerals: Presidents are guaranteed a ceremony with full honors and the option to be buried at Arlington National Cemetery.
  • Secret Service Protection: Presidents are eligible for lifetime protection. The related costs are classified.
Hata Maktaba ya Rais wa Marekani hazijengwi na serikali.

Utaona hamna anayepewa nyumba maana sidhani kama kuna rais asiyekuwa na makazi yake mwenyewe. Kujengewa ofisi sawa. Lakini hili la nyumba kwa kweli sioni sababu yake.

Amandla...
 
Ningependa kujua kama kuna nchi nyingine ambayo inawajengea/inawapa nyumba viongozi wake wakuu wakitoka madarakani?

Na inawapa magari mapya ambayo kila baada ya miaka mitano wanapewa mengine mapya ( sijui tamati ya yale ya awali). Uhuru amepewa nyumba?

Amandla...
Kwi Kwi Kwi
 
Huo utaratibu upo nchi nyingi. Kenya upo. Hata Obama pia alipewa nyumba.
Usichokijua kingine ni kwamba Raisi mstaafu bongo hii anapewa monthly 80% his pensionable salary.
Anapewa entertainment allowance. Two personal secretaries, Four messengers, office space, two drivers, moja wake mwingine mke wake.
Home workers to 34 including dobi, mtu wa bustani, full medical cover, full furnished office inatengewa pesa ya uchakavu kila mwaka.
Raisi mstaafu anapewa gari nne sio moja, Mwinyi anawake wawili kila mmoja anapewa gari na mpambe and other perks including Mafuta, vipuri na matengenezo under tax payers expenses.

Unapoambiwa keki ya taifa uwe unajua ni ya wateule.
Sio kweli. Rais mstaafu wa Kenya hapewi nyumba bali anapewa posho ya nyumba. Rais mstaafu wa Marekani hapewi nyumba bali anahamia kwake. Obama alipanga nyumba Washington ili asimuhamishe binti yake.
Nadhani ni sisi tu ndio tunaowajengea nyumba. Nasikia kuna mabadiliko na wigo limepanuka zaidi la wanaostahili nyumba.

Amandla...
 
Kwa mwananchi mwenye akili hawezi kukubali kwamba kulipa kodi ni uzalendo wakati pesa yake inatumika kunufaisha wachache kwenye nchi ambayo shule hazina walimu, madawati na matundu ya vyoo.

Kama wanapata huduma zote hizo bure kazi ya mshahara na posho kwa rais aliyepo madarakani ni ipi wakati akistaafu anahudumiwa bure? Na kazi ya pensheni ya 80% ya mstaafu ni ipi ikiwa bado anaendelea kuhudumiwa bure? Africa ni bara linalosumbuliwa na ujinga mkubwa sana sana unaotengenezwa na walafi waliopo madarakani.

Mwananchi mwenye kipato kisichofika milioni 10 kwa mwaka anajenga nyumba na kusomesha lakini rais anayepata mamilioni kwa mwezi hawezi kujenga nyumba yake na kujigharamia mavazi, chakula na usafiri. Hapo unakuta akiwa madarakani anaanzisha au kuendeleza biashara zake kubwa lakini bado wananchi wanabebeshwa mzigo wa kuhudumia. Ni dhambi mbaya sana hiyo.

Afrika inahitaji ukombozi.
 
Ningependa kujua kama kuna nchi nyingine ambayo inawajengea/inawapa nyumba viongozi wake wakuu wakitoka madarakani?

Na inawapa magari mapya ambayo kila baada ya miaka mitano wanapewa mengine mapya ( sijui tamati ya yale ya awali). Uhuru amepewa nyumba?

Amandla...
Aisee sijui nimefurahi tu kukuona..ila hapa US siyo tu magazine na ulinzi na vingine na wanapewa perks mbalimbali. Maktaba za Rais huanzishwa jimbo analotoka na zinaendeshwa na serikali chini ya National Archives. Ila labda sisi tunawapa mengi...ila ndiyo shukrani yetu??
 
Hili linahitaji MJADALA mpana wenye AFYA kwa maslahi ya nchi yetu..ni lazima tujiulize
Ni halali kisheria?
Ni halali kijamii?
Kwa hali ya UCHUMI wetu ni SAWA?
Mishahara na stahili zingine wapatozo+ kulelewa kipindi wakiwa madarakani,inastahili kuendelea KUJENGEWA?
 
Huo utaratibu upo nchi nyingi. Kenya upo. Hata Obama pia alipewa nyumba.
Usichokijua kingine ni kwamba Raisi mstaafu bongo hii anapewa monthly 80% his pensionable salary.
Anapewa entertainment allowance. Two personal secretaries, Four messengers, office space, two drivers, moja wake mwingine mke wake.
Home workers to 34 including dobi, mtu wa bustani, full medical cover, full furnished office inatengewa pesa ya uchakavu kila mwaka.
Raisi mstaafu anapewa gari nne sio moja, Mwinyi anawake wawili kila mmoja anapewa gari na mpambe and other perks including Mafuta, vipuri na matengenezo under tax payers expenses.

Unapoambiwa keki ya taifa uwe unajua ni ya wateule.
Hii nzuri
 
Sio kweli. Rais mstaafu wa Kenya hapewi nyumba bali anapewa posho ya nyumba. Rais mstaafu wa Marekani hapewi nyumba bali anahamia kwake. Obama alipanga nyumba Washington ili asimuhamishe binti yake.
Nadhani ni sisi tu ndio tunaowajengea nyumba. Nasikia kuna mabadiliko na wigo limepanuka zaidi la wanaostahili nyumba.

Amandla...
Utamu ni kwamba, unahamasishwa kuongeza "mke" ili maruprup yaongezeke. Halafu unakuja na stories za "KatibaMpya"!! Nani akuelewe! Wanaxema wenyewe "over my dead body". Kwa misingi hiyo, wakiongeza ya wastaafu wa kawaida, wanaona itakua unawapunguzia ya kwao, na wanaongezeka kipindi hadi kipindi. Changanya na ya wakuu wengine ktk mihimili mingine ndo ujue kw nn Afrika tunaishi kw mikopo na misaada. Nchi maskini bajeti yote inaishia kwny matumizi na mafao ...! Wala hawaoni haya
 
Aisee sijui nimefurahi tu kukuona..ila hapa US siyo tu magazine na ulinzi na vingine na wanapewa perks mbalimbali. Maktaba za Rais huanzishwa jimbo analotoka na zinaendeshwa na serikali chini ya National Archives. Ila labda sisi tunawapa mengi...ila ndiyo shukrani yetu??
Ni vile tunaiga mazuri hadi kupitiliza na kuelekea kuharibu sasa
 
Ningependa kujua kama kuna nchi nyingine ambayo inawajengea/inawapa nyumba viongozi wake wakuu wakitoka madarakani?

Na inawapa magari mapya ambayo kila baada ya miaka mitano wanapewa mengine mapya ( sijui tamati ya yale ya awali). Uhuru amepewa nyumba?

Amandla...
Ony in Tanzania, huku Matundu ya vyoo tunaomba msaada nje
 
Sio kweli. Rais mstaafu wa Kenya hapewi nyumba bali anapewa posho ya nyumba. Rais mstaafu wa Marekani hapewi nyumba bali anahamia kwake. Obama alipanga nyumba Washington ili asimuhamishe binti yake.
Nadhani ni sisi tu ndio tunaowajengea nyumba. Nasikia kuna mabadiliko na wigo limepanuka zaidi la wanaostahili nyumba.

Amandla...
Na wenza wa Marais na viongozi wakuu wanalipwa mpaka wafe. Nashauri na watoto waingizwe kwenye list ya nyumba na malipo ya mwezi
 
Ningependa kujua kama kuna nchi nyingine ambayo inawajengea/inawapa nyumba viongozi wake wakuu wakitoka madarakani?

Na inawapa magari mapya ambayo kila baada ya miaka mitano wanapewa mengine mapya ( sijui tamati ya yale ya awali). Uhuru amepewa nyumba?

Hawakuwa na mishahara?
Hawakuwa na mishahara
 
Aisee sijui nimefurahi tu kukuona..ila hapa US siyo tu magazine na ulinzi na vingine na wanapewa perks mbalimbali. Maktaba za Rais huanzishwa jimbo analotoka na zinaendeshwa na serikali chini ya National Archives. Ila labda sisi tunawapa mengi...ila ndiyo shukrani yetu??
Asante MMK. Its been a minute toka tumeonana.
Swali langu ni kwa nini tuwashukuru kwa kuwapa nyumba? Hivi kweli kwa ile posho na marupurupu wanayopewa wanashindwa kujijengea nyumba kama wanaona ina umuhimu? Ni selfishness ya hali ya juu na wigo wa wanaoona nao ni haki yao kujengewa nyumba ya kifahari unapanuka. Mimi nitashangaa sana nikisikia kuwa Rais wetu wa sasa hana nyumba na alikuwa anapanga kabla ya kuwa VP. Kwa nini tunakazania kuwaongezea utajiri watu ambao ni matajiri wa kutupa? Hatuna mahitaji mengine zaidi ya hayo?
Wamarekani marais wanajenga maktaba ambayo inakuwa kumbukumbu yao na inaendeleza mambo ambayo anaona yana umuhimu kwa jamii, k.m. Carter Centre. Wanawarudishia fadhila kwa wananchi waliowapa heshima ya urais. Sisi wanaona kuwa walitutendea favour hivyo tunapaswa kuwashukuru kwa kuwa viongozi wetu. Hii haijakaa vizuri hata kidogo.

Amandla...
 
Back
Top Bottom