Serikali imejifunza nini maafa haya ya mvua?

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,113
KATUNI(595).jpg

Toa Maoni ya katuni


Mvua zilizonyesha juzi na jana katika Jiji la Dar es Salaam, zimesababisha maafa makubwa vikiwemo vifo vya watu 13, kuharibu makazi na miundombimu.

Wakazi kadhaa katika baadhi ya maeneo wamelazimika kuyakimbia makazi yao na kupatiwa hifadhi katika maeneo ya shule kutokana na nyumba zao kuzingirwa na maji na nyingine kuzama.
Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), imesema kuwa mvua hizo ni kubwa na hazijawahi kunyesha nchini tangu mwaka 1956.

Kwa mujibu wa taarifa ya Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Dk. Agnes Kijazi, mvua za juzi zilikuwa milimita 156 wakati zilizonyesha jana zilikuwa milimita 60 na kufanya jumla ya milimita 216. Mamlaka hiyo pia imesema kuwa mvua hizo zitaendelea kunyesha hadi leo.

Baadhi ya shughuli katika jiji la Dar es Salaam jana zilisimama kufuatia mvua kubwa iliyonyesha kuanzia juzi usiku hadi jana mchana na kusababisha vifo vya watu wanane na wengine watano walioripotiwa kufariki katika mvua za juzi.

Hali ni mbaya kutokana na kukatika kwa mawasiliano kiasi kwamba wakazi wengi wa Jiji jana walishindwa kwenda katika maeneo ya kazi biashara kutokana na madaraja kukatika.


Aidha, ananchi kushindwa kuvuka kutoka sehemu moja kwenda nyingine, lakini pia maeneo mbalimbali ya jiji yalijaa maji na kusababisha barabara kufungwa.
Wananchi kadhaa walipoteza maisha yao kutokana na kusombwa na maji pamoja na kunaswa na umeme huku wengine wananchi walipoteza mali zao.


Wakati watu wakifariki katika mafuriko ya Dar es Salaam, watu wanne wamekufa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha wilayani Bunda mkoani Mara.

Atahari za mvua pia zimesababisha abiria zaidi ya 1,500 kukwama kwenye kituo cha reli mkoani Dodoma kutokana na kuharibika kwa njia ya reli kati ya Dodoma na Morogoro.
Abiria walikuwa walikuwa katika treni ya kutoka Tabora na Kigoma kwenda Dar es Salaam, lakini walikwama Dodoma, kufuatia kituo cha reli cha Gurwe wilayani Mpwapwa kuharibika kutokana na mafuriko.


Kadhalika, zaidi ya abiria 5,000 waliokuwa wanasafiri kutoka eneo la Kisiwani kwenda maeneo mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, wamekwama kuendelea na safari, kutokana na daraja la eneo la Mzimbo katika kijiji cha Nkonga Ijunyi, Kata ya Kisiwani wilayani Same kusombwa na maji.

Kimsingi, haya ni maafa ambayo yametokana na kutotochukuliwa kwa hatua, ambazo tunaamini kuwa kama zingechukuliwa mapema, hali hiyo isingeweza kutokea.
Kwa muda mrefu, serikali imekuwa ikishindwa kuchukua hatua mapema za kukabiliana na maafa kama haya, licha ya baadhi ya wanasiasa na watendaji kutoa kauli na matamko bila kutekelezwa.


Uwezekano wa kunyesha kwa mvua kubwa za vuli na zenye athari ulielezwa na TMA miezi kadhaa iliyopita, lakini hatua madhubuti hazikuchukuliwa kwa ajili ya kukabiliana na hali hiyo.

Hali hiyo inaonyesha kwamba mipango na mikakati ya kukabuliana na maafa ni ya kutilia mashaka kutokana na kutokuwepo na utekelezaji.
Kwa mfano, serikali ilishindwa nini kuwaondoa kwa nguvu watu wote wanaoishi katika maeneo ya mabondeni, ambao juzi na jana ndio waliojikuta wakiwa waathirika wakubwa wa mvua hizo?


Tunashindwa kuelewa sababu za serikali kwa miaka nenda rudi kutokuwaondoa watu wote wanaoishi maeneo hatarishi na kuwapatia maeneo menngine yenye usalama.

Watu hao wamekuwa wakijenga na kuyaendeleza makazi yao huku mamlaka husika za serikali hususani halmashauri zetu zikiona bila kuchukua hatua za kuwaondoa.

Lakini vile vile, inaonekana kwamba kuna udhaifu katika ukarabati wa miundombinu kama barabara, reli, nguzo za umeme, madaraja mara kwa mara na matokeo yake ni kuwa zinapotokea mvua zenye mafuriko, miundombinu hiyo inaathirika kwa kiasi kikubwa.

Ni kwa nini basi hatua za kukarabati miundombinu hiyo hakikuchukuliwa baada ya taarifa za utabiri kuonyesha kuwa kutakuwa na nvua kubwa zenye athari?

Tunaamini kwamba maafa hayo yatakuwa ni changamoto kwa serikali kujitathmini na kujipanga upya ili kuhakikisha kwamba hali hiyo haitatokeas tena.

Sio vizuri kusubiiri maafa yatokee ndipo serikali ianze kuchukua hatua za kuwatengea waathirika makazi ya muda kama ilivyofanya jana.



CHANZO: NIPASHE

 
Sidhani kama serikali imejifunza kitu kwani tutaona pindi hali itakapokuwa shwari watu watarudi huko kwao mabondeni na serikali kuendelea kunyamazia pia inasikitisha sana kwa serikali kuwa kimya mpaka mpaka maafa kukamilika yani wakufa kumaliza kufa wakupoteza mali kumaliza kuzipoteza ndo wakajitokeza kujifanya wameguswa kwa hili Mungu ndo atawalipia kwani mlituhadaa mnatuongoza kumbe kumbe mnatummaliza kimya kimya japo tuliwakataa mliingia madarakani kwa nguvu
 
Sio kila kitu serikali, wananchi nao wamejifunza nini?.
 
Back
Top Bottom