Kuna kubwa la kujifunza hapa. Pumzika kwa Amani Aziza (Janet) Frisby

Makari hodari

JF-Expert Member
May 17, 2022
2,660
5,157
Ndugu zangu tuchukue tahadhari popote pale tulipo duniani. Usimuamini mtu tena, bin-Adam tumekuwa wanyama! Chuki iliyopitiliza mwisho wake ni unyama wa kiwango cha hali ya juu.

Binti mdogo, mrembo na msomi aliyekuwa akipambania anachokipenda zaidi na kuzitimiza na kuzifikia ndoto zake aliyekuwa akijulikana kwa jina la "Aziza (Janet) Frisby, mtoto wa tajiri na mshua mwenye asili ya Kitasha aliyezaaga watoto kadhaa na Mwanamama pisi ya kwenda ya kibongo mwenye kaushombe ka Kiarabu huko Arusha, ambaye aliuwawa kwa sumu huko jijini Nairobi nchini Kenya takribani wiki na siku kadhaa zimepita.

ILIKUWA HIVI...

Binti alitembelewa na marafiki zake (ma-slay queen wenzie) kwenye apartment ambayo alikuwa akiishi na nduguye wa kike jijini Nairobi.. bahati nzuri hii familia ya Frisby ina mabinti wakali kwelikweli! (Hata bwana Simba wa tandale ameshaonja mali mojawapo kutoka familia hiyo... bila kumsahau mtoto wa mheshimiwa J.K, aliyekuwa rais wa awamu ya nne chini TANZANIA, bwana Khalfan Kikwete) Nduguye aliyekuwa akiishi pamoja nae, nae ni pisi ya kwenda.

Basi kama unavyojua watoto wa kishua na ma-Slay queen wakishakutana chit-chats za hapa na pale, hugging, vicheko na kupendana kwa uongo na kweli kukaendelea... baadae binti akajiandaa akatoka na marafiki zake kwenda maeneo yao ya kujirusha na kujidai jijini Nairobi.

Baada ya kufika huko inasemekana kwenye kula na kunywa kuna mistake binti aliifanya, aliwaamini hao aliodhani ni marafiki zake akaacha kinywaji na kwenda washroom, baada ya kurudi bila hili wala lile akaendelea kuburudika na kuongeza na kuongeza kumbe inasemekana aliwekewa sumu.

Muda ukaenda, wakaagana na kurudi nyumbani (kwenye apartment aliyokuwa akiishi na Dada yake) hapohapo jijini Nairobi, ila ilikuwa ni usiku mnene kidogo... kama unavyojua washua kila mtu na room yake.

Siku ilipogeuka au kulipokucha Dada mtu hana hili wala lile akashangaa ndugu yake amechelewa sana kuamka siku ile akaona kuna haja ya kwenda kumcheki nduguye akakuta alishafariki muda mrefu sana! Inasemekana ni usiku uleule Aziza alikata kamba 😔😭

Dada mtu akahangaika kutafuta msaada kwa majirani na walinzi, kuita ambulance na kufuata taratibu zingine kutoa taarifa huku Bongo na kwingineko kwa ndugu zao duniani... Matajiri hawashindwi na jambo, basi Walipoanza ku-trace watu aliokuwa nao usiku uliopita na waliompitia nyumbani kwa bahati mbaya wote simu zao zilikuwa hazipatikani.

Inasemekana binti alikuwa akichukiwa chinichini na hao ma-slay queen wenzie aliokuwa akidhani ni marafiki zake na akawaamini. Sasa sijui ni wivu au kuna mengineyo chini ya Carpet.

All in all tuweni makini sana na watu tunaodhani ni marafiki au watu muhimu na wa dhati kwetu, hasa tunapokuwa sehemu za starehe... na Nairobi inasemekana ndio michezo yao kumalizania kwa sumu kwenye kumbi za starehe.

Kuna haja ya kuchukua tahadhari hata Bongo pia.

Poleni sana familia ya Frisby. Pumzika kwa amani Aziza/Janeth umeenda na utamu wako 😔😔😔

IMG_20231018_213025.jpg
 

Attachments

  • 20231020_061714.jpg
    20231020_061714.jpg
    180.9 KB · Views: 21
  • 20231020_061649.jpg
    20231020_061649.jpg
    181.2 KB · Views: 22
  • IMG_20231020_055927.jpg
    IMG_20231020_055927.jpg
    206.4 KB · Views: 20
Inasemekana pia ila familia yake haijakubaliana na hilo na wanaamini ni sumu. Kwann wale aliokuwa nao wote hawapatikani hewani mpaka leo?! Na hatuwezi kujua kama wapo Kenya au washapaa baada ya kukamilisha mission

Hata models wengine walipost kwamba hawaamini hayo majibu, kuna mengine chini ya Carpet
Sisi wenye shule ya forensic medicine huyo kilicho muua ni death by aspiration in sleep hakuna cha simu wala Nini alizidisha kiwango cha pombe
 
Back
Top Bottom