Kuna kitu kinakosekana kwangu, kwa kuwa nimekua bila malezi ya baba

pole sana mkuu! This issue is very serious coz am experiencing it. Sometimes hua nalia kabisa coz dingi angu yupo alive bt hajanilea na sikuwahi kumwona mpaka nafikia 20+ years. Hua inaniwia vigumu kumwita baba kwani miaka yote hiyo aliniacha na kufanya yake sasa nimekua mtu ndo anasema oooo mwanangu


Moral lesson
You better be a good parent no matter what!!!!!
 
Ni kweli mkuu. Hata mimi sikuwahi kumwona baba kwani alifariki nikiwa na miezi mitatu tu. Looking back now naona kuna mambo ambayo ningekuwa na baba pengine ningekuwa tofauti kidogo. Ni wazi kuna vitu nimekosa hasa ile model na kuwa na shujaa wa moja kwa moja katika maisha yangu. Mshauri, mlinzi na mhimili wa kisaikolojia katika ile miaka ya utoto, utineja n.k.

Pamoja na haya yote my mom was/is one of the strongest women I know. Alihakikisha kuwa nalelewa katika misingi imara, namfahamu Mungu na kutenda wema na kuwa humble hapa duniani. Na kutokana mfano wake, napenda na kuheshimu wanawake sana. Zaidi ya yote, lile pengo la kumkosa baba siku moja litazibwa kwa mimi kuwa baba na mume bora kabisa kwa wanangu na mke wangu siku nitakayoamua kuoa na kuwa na watoto. Nitahakikisha kuwa nilichokikosa mimi wao wanakipata sabini mara sabini na kuendelea!


Nakumbuka siku nyingi zilizopita tulikuwa tunafanya mitihani ya form 6 mimi na rafiki zangu watano tumekaa sehemu tunakula. Mooja wwetu akaanzisha stori kwamba hajawahi kumuona baba yake,tangu mdogo analelewa na mama yake!

Cha ajabu wote pamoja na mimi tulikuwa wa aina hio. Tuliolelewa na mama tu bila kumuona baba au kumuona wakati uko mdogo sana!

Kama ulivyomaliza,kwa experience yangu[sio kiuchumi/kielimu au kwa kukosa chochote,kwani nimepata kila nilichokuwa napata kwa mama] sitataka hata siku moja mtoto wangu amkose baba yake!
 
Kila kitu ni namna unavyokitafsiri,kujiona haujakamilika nayo ni fikra uliyojijengea kichwani.
 
Kila kitu ni namna unavyokitafsiri,kujiona haujakamilika nayo ni fikra uliyojijengea kichwani.

Huwezi kukataa au kubisha umuhimu wa wazazi wote kwenye makuzi ya mtoto, wewe lelewa na baba tu alafu useme unajiona kawaida huna tatizo, utakua na matatizo ya akili.
 
Nakumbuka siku nyingi zilizopita tulikuwa tunafanya mitihani ya form 6 mimi na rafiki zangu watano tumekaa sehemu tunakula. Mooja wwetu akaanzisha stori kwamba hajawahi kumuona baba yake,tangu mdogo analelewa na mama yake!

Cha ajabu wote pamoja na mimi tulikuwa wa aina hio. Tuliolelewa na mama tu bila kumuona baba au kumuona wakati uko mdogo sana!

Kama ulivyomaliza,kwa experience yangu[sio kiuchumi/kielimu au kwa kukosa chochote,kwani nimepata kila nilichokuwa napata kwa mama] sitataka hata siku moja mtoto wangu amkose baba yake!

Hili jambo huwa linaniumiza sana, ndio maana huwa nakua makini sana na kummpa binti mimba kisha nisimuoe,kwa sasa sina mpango wa kuoa na sifikirii hivyo..ila my mind is still evolving,siku moja naweza kuamua

Ikitokea nikaamua basi ntafanya kila kitu kuhakikisha mmtoto wangu anapata malenzi yanngu na ya mama yake.

Katika maisha yangu sijakamilika kabisa, kumkosa mama au baba katika mmaisha kuna tatizo.
 
Tupo wengi tunao pitia hali hiyo. Binafsi hadi Leo simfahamu na sijui kama yupo hai au amekufa. Haipiti siku sijamfikiria na kujenga taswira ni mtu wa namna gani,au pengine ningemuona hata kwa sekunde tu maisha yangu yangebadilika sana. Sio kwa kunipa pesa au chochote,ila kujua tu yeye ndio 'babangu' nadhani ningeanza new Chapter.
 
kobe-bryant.jpg


Realest talk .
I hear you man. And the thumb(s) up from Black Mamba aka the GOAT himself is real cool.

By the way, I like your comments here. They are always creative, funny, positive, encouraging and real. Keep it up!
 
Jamani hiyo situation hamuwezi kujua imemuathiri vipi kisaikolojia na ndio maana inamuuma na labda hamjui mazingira anayopitia mpk kufikia kusema hvy. Kwa upande wake labda anahisi kukosa malezi ya baba yake yanamsababishia kupitia anayopitia. ila kaza buti
 
kaka asikwambie mtu,mpk sa hv maisha ninayoishi mungu mwenyewe anajua, but we are the men, inabidi tukubali you never know Mipango ya Mungu.

Yeah, tunapaswa kuwa wanaume mkuu.

Kukosa kitu chochoye kwenye maisha hasa katika malezi kina madhara sana.

Mfano, mpenzi wangu wa zamani aliniomba awe ananiita kaka, akasema kwao hakuna mtoto wa kiume kwa hiyo atakua anafarijika sana kama atakua ananiita kaka.

Kww hiyo huwa ananiita kaka hata sasa baada ya kuachana na sasa huwa ananitreat kama kaka yake kabisa, tushaachana na sasa ni kaka na dada na hata akiomba jambo nimsaidie ananiomba kama kaka yake.

Alinambia kwa kukosa kijana wa kiume kwao anajihisi hajakamilika hivyo anavyoniita kaka anafarijika sana.
 
Story yako inashabiana kwa Karibu sana na yangu .
Nimelelewa na mama tangu nina miaka mitatu baada ya baba kufariki .

Tumezaliwa wawili tu wote wa kiume Leo tunamaisha yetu.

Wakati nakua nilikuwa nawaonea gere wenye baba zao.

Lakini nilipiga moyo konde Leo Mimi mtu.mzima haya mambo nishasahau.
 
Nilimkosa baba katika malezi but nimekuwa nawauliza watu walimfahamu .

Wananiambia alikuwa mtu safi sana kwa tabia na Akili kichwa .

Historia yake kitaaluma ilikuwa bomba sana na kwa tabia inasemeka katika watu wanaotoka huku kijijini kwetu hakupata kutokea mtu kama yeye.alipendwa na kila mtu.kiasi kwa siku ya msiba wake ilikuwa ni nyomi la watu hapo nyumba .

Alikuwa muuajiriwa wa udsm kama mhandisi wafanyakazi wenzie walimpenda sana .

Mambo hayo yote yalinipa uchungu sana kumkosa baba yangu.Mimi na mdogo wangu wa kiume tuli-fight sana katika Elimu bila kuchoka Leo Mimi ni muajiriwa serikali na mwenzangu daktari.

We made him our role model kwa bidii na tabia kiasi kwamba watu wanatushangaa sana today.

I miss u so much dad r.I.p may our almighty God grant u eternal life in his kingdom.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom