kuna kanuni inatamka kuwa kauli za kufuta bungeni ni za chadema tu.

Ringo Edmund

JF-Expert Member
May 10, 2010
4,879
1,125
wanajf nimekuwa nikifuatilia sana mijadala ya bunge ila naona kauli za upinzani haswa chadema ndizo zinazoamriwa kufutwa kila wakati,na hata nje ya bunge kauli za wabunge wa ccm zinapita tu hata kama zimeingia kwenye hansard za bunge.
mnyika kutaja neno rais ni dhaifu hata kama lipo kwenye misamiati ya kawaida anatakiwa kufuta ila nchemba kuita wabunge ni wajinga na kiita bajeti ya upinzani takataka hata kama ipo kisheria.

komba aliwahi kusema kuwa serikali ikiendelea kushindwa kupeleka maendeleo kwake atawashawishi wapiga kura wake wahamie malawi na hilo liko kwenye hansard.

pamoja na kauli ya nasari kufutwa na mwenyekiti wake muda uleule bado ccm wameendelea kuishikia bango.
 
halafu me nilifikiri mnyika kaongea maajabu gani, kumbe raisi ni dhaifu? Makosa haya ambayo ccm wanayafanya wakijua wanaitetea ccm yao kiukweli inazidi kuwapotezea muelekeo kabisa, sijaona cha-uongo kilichoongelewa hapo jamani, kama kuongea ukweli nao ni kosa sawa but mnyika yuko sahihi na namuunga mkono
 
Yanamwisho haya na mwisho wake haupo mbali sana, muhimu ni kujipanga kwa Ushindi
 
Wabunge wa Chadema wanapita katika wakati mgumu kupita kiasi yaani wakiomba mwongozo wa spika hawaruhusiwi wakati wa CCM wanapewa fursa,Mwigulu aliwatukana matusi ya nguoni wapinzani hakuna kanuni ilitumika inauma sana
 
dawa yao wakipewa dakika kumi nao wantukana dakika 3,dakika 7 wanachangia,maana muongozo kwa ccm tu
 
Miongoni mwa mambo yasiyo fair ni hilo mfano jana jumatatu wakati Mwigulu anawatukana CHADEMA wabunge wa upinzani waliomba muongozo lakini mwenyekiti hakuwapa lakini wa magamba wakiomba wanapewa hata kama hawana la maana.
 
Back
Top Bottom