Kuna haja ya Mzamiru kuanza kila mechi

Soloma TV Online

Senior Member
Jun 26, 2023
104
291
Baada ya ingizo lake tu matundu yaliyokuwa yametobokatoboka aliweza kuyaziba ipasavyo na kupelekea Simba kuwa imara kabla ya ingizo lake.

png_20230817_182353_0000.jpg
 
Jamaa leo asingeingia kuna mawili mechi ingeisha droo au Simba angepasuka.

Uzuri wa Mzamiru huwaga anacheza chini na kuwasaidia sana mabeki na mara nyingi huwaga anaficha mapungufu ya safu ya ulinzi.

Ukitizama leo, Simba walipoteza mipira mingi karibia na box lao na vile vile Kapombe na Zimbwe walikuwa wanapanda sana, wanacha magape na mtu wakuziba hayo magepu kwa leo alikuwa hamna kwa kipindi cha kwanza,Ngoma mzito sio mwepesi na mzuri ktk kukaba kama Mzamiru, Kennedy na Che bado hawa helewana na inaonekana hawapeani majukumu ktk kukaba.

Ndio maana kipindi cha kwanza Mtibwa walipata nafsi mbili na kuzigeuza kuwa magoli na bado walipata nafasi kama mbili ambazo kama wange tulia wangepata magoli. Kipindi cha pili Mzamiru aliingia kurekebisha yote.So kwangu mimi Man of the match Mzamiru bila yy hii mechi ingekuwa droo.

Ukitizama kwa makini Mzamiru siku akipata majeruhi Simba watapata tabu sana,sijui kama wana kiungo mkabaji mwingine mzuri kwenye uwezo wa kukapata kama Mzamiru. Kocha inabidi achague kati ya Mzamiru, Ngoma na Chama au Mzamiru, Kanoute na Chama ila akijaribu kufanya kama alicho kifanya leo mtapoteana ndugu zangu. Ngoma mzuri wakati timu ikiwa na mpira ila kwenye kukaba hata Kanoute anamzidi.
 
TATIZO KUBWA sana na Simba ni.

1. Kukosekana kwa Kiungo Mkabaji
Kutaigharimu sana Simba
Viungo wake wote Ni 8.
Kanute8.
Mzamiru 8
NGOMA 8,10.


2.. Kukosekana MBADALA/ mtu wa kumchallange Inonga na Malone.
Wakiwa na ADHABU ama Majeraha.
 
UAJIULIZA ANAYEFANYA USAJILI WA MAWINGA ANAAKILI TIMAMU KWELI?????????

Mawinga. 2023
1. Peter Banda.
2. Jimyson Mwinuke.
3. KIBU Denis.
4.Said Ntibazonkiza.
5. CLOTUS Chama 10-11.
6. Aubin Kramo.
7. Essomba Onana.
8. Luis Miquesson.
10. Moses phili. 10+ 11

Hili KOSA lilifanyika 2020.
Mawinga walikuwa kumi, ukiunganisha idadi Yao mchango WAO MAGOLi hayafiki hata 10.

1 Bernald Morison.
2. Perfect CHIKWENDE.
3. Hassan Dilunga.
4. Ibrahim Ajibu.10--⁷
5.peter Banda.
6.pape sackho
7. Dunkan Nyoni
8. Valentine Muhilu.
9. KIBU Denis.
10. RALY BWALYA 8-10--11.

UNAJIULIZA HUU USAJILI UNAFANYWA NA MTU MWENYE AKILI TIMAMU KWELI.
 
Mpaka sasa sioni haja yoyote ya mzamiru said selemba kuanzia nje.

Kanoute na ngoma ni viungo ambao hawana attributes za kukaba na hata kwenye 1 v 1 sio wazuri uki compare na mzamiru.

Ila binafsi kanoute na ngoma naenda na kanoute kwasababu yupo sharp na mwepesi.

Mzamiru yuko vizuri sana both offensive na defensive,hiki kitu ndicho kimewasaidia sana simba jana.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mpaka sasa sioni haja yoyote ya mzamiru said selemba kuanzia nje.

Kanoute na ngoma ni viungo ambao hawana attributes za kukaba na hata kwenye 1 v 1 sio wazuri uki compare na mzamiru.

Ila binafsi kanoute na ngoma naenda na kanoute kwasababu yupo sharp na mwepesi.

Mzamiru yuko vizuri sana both offensive na defensive,hiki kitu ndicho kimewasaidia sana simba jana.


Sent using Jamii Forums mobile app
Unaenda na Kanute unamuacha Fabrice Ngoma?

Wewe ni mshabiki wa Simba?
 
Bodi ya wakurungezi ya Simba, ikiongonzwa na Try Again na Murtaza Magungu , itakuwa Kuna shida mahali!
Haiwezekani msimu wa tatu huu! Wanafanya usajili usioeleweka!

Yaani ni kama vile sio watu wa mpira na hawatafuti ushauri kwa watu wa mpira!
Tatizo kubwa a Simba kwa misimu hii mitatu ilikuwa kiungo wa Chini( mkata umeme hasa)- au holding midifilder
Viongozi usajili wao wa mwaka huu hawakuangalia eneo hilo- Mzamiru na Kanoute ni viungo wakutembea!

wamesahau pia kwenye beki wa kati mwenye kiwango wa kumsadia Che na Inonga, sio huyu Kennedy!

upande wa Shabalala! Pia hakuna mbadala!

Wao aklii Yao yote ni washambuliaji tu!

Yetu macho na masikio
 
Back
Top Bottom