Joseph lebai
JF-Expert Member
- Jul 19, 2017
- 8,452
- 8,607
Na wewe ni mmojawapo! Tufanyeje?
Nilijiuliza sana jambo hilo tangu nikiwa mtoto mdogo. Baadaye niliacha mwenyewe kuangalia maiti baada ya kuona hakuna anayekubali kuacha kukodolea mimacho maiti isiyoona wala kuhisi chochote. Nakuunga mkono, sioni maana yoyote ya kuhangaika na mwili mfu zaidi ya kuuzikaKuna faida gani labda ya Kimantiki Watu Kulazimisha (Kung'ang'ania) Kumuangalia Marehemu akiwa 'Jenezani' tena ameshalala Usingizi wake wa Milele na kwamba hata ukipita Kumuaga kwa kumsogelea au kumgusa na kulia kila aina ya kilio wala hawezi kukujua sana sana utakuwa ni kama vile unapaka tu Rangi upepo?
Haya Waaga 'Marehemu' hebu nijibuni.
Sawa kabisa!Urithi wa mila na desturi kutoka magharibi, kwa wazungu vilitiathiri sana ndio maana waafrika mfumo wetu wa kuzika ilikua mtu akifa tunahama hilo eneo na kwenda mbali maana tuliamini kifo ni laana na jamii nyingine mtu akifa hakuna kuaga walikua wanaufunga mwili na wanachaguliwa wanaume wa shoka wanaubeba na kwenda nao mbali na kuchimba shimo huko na kuufukia kimila na kurudi nyumbani tena haikuepo masanduku haya ya sasa.
Tukirudi kwenye mila zetu waafrika tutaishi muda mrefu sana na tutakua na furaha
Mfu hauoni huo mkono unaoaga, hayupo! Uwe unaaga na kuwapungia mkono waliohai, si wafu - ni mavumbi hayo.kuna haja gani kuwapungia mkono wa kwa kheri watu wanaposafiri, maana hoja yako ina maana kuwa kuaga ni jambo baya kwa wale tulionao kila siku maishani mwetu..
Hapo sasa!Unamuaga anaesafiri kwa sababu nae atakuaga na mtaelewana, maiti ataelewa kama umemuaga,? Na ukumbuke pale haelewi chochote kile maana hana ufahamu na uhai sasa kuna sababu gani ya kumuaga tena?
Ile ni kusherehesha tu kuaga mwili wa marhemu sio ibada hata neno la kuaga inatokana na kuagiza na unaweza ukamuaga au ukamuagiza mtu alie macho, sio alielala, sasa utaagaje kitu kisicho na uhai?.Huu mnakasha ni mpana kwa kuwaza karibu huwezi kuujadili, inajulikana mwanadamu anazaliwa, anaishi, na atakufa sasa kama ameshazaliwa, ameishi, kwa nini akifa ndio tuseme tunaaga wakati tulijua kufa kupo na akifa hatorudi na hatutomwona tena
Hii ndio inanikera kabisa. Wanaotakiwa kumuaga binti ni wana ndugu tu, sasa utakuta mtu anachangisha kila atakaekutana nae. Nakumbuka miaka ya nyuma mzazi anafanya shughuli hii nyumbani au kama ni kwenye ukumbi basi wahusika ni wanafamilia tu.Na vipi kuhusu Sendoff
Limekaa kisaikolojia zaidi, hakuna mtu anaumia kama ambaye hajashuhudia maziko ya mpendwa wake.
Sijui nimeeleweka hapo kwenye 'kushuhudia'.
Ipo hivi pale hatuagi bali tunaenda kushuhudia tu, mwamba ndio kalala hapa kimya na soon tunamzika. Kwaheri.
Hata marehemu huwa anapungiwa mikono akiwa kwenye jeneza lililofunikwa, je huwa anaona?kuna haja gani kuwapungia mkono wa kwa kheri watu wanaposafiri, maana hoja yako ina maana kuwa kuaga ni jambo baya kwa wale tulionao kila siku maishani mwetu..
nilishaacha kitambo suala la kuaga mwili labda tu inapolazimika kwa sababu ambazo siwezi kuepuka ndio nafanya hivyoUnamuaga anaesafiri kwa sababu nae atakuaga na mtaelewana, maiti ataelewa kama umemuaga,? Na ukumbuke pale haelewi chochote kile maana hana ufahamu na uhai sasa kuna sababu gani ya kumuaga tena?
Inasikitisha mno!Sisi tunakua shapu kuhudumia msiba tena tunachanga pesa nyingi, kuliko kujitoa kuchanga pesa mtu akiugua sijui inakuaje hapo
Binafsi, sionagi ulazima ila ni jambo la hiari sana kuliko ulazimaKuna faida gani labda ya Kimantiki Watu Kulazimisha (Kung'ang'ania) Kumuangalia Marehemu akiwa 'Jenezani' tena ameshalala Usingizi wake wa Milele na kwamba hata ukipita Kumuaga kwa kumsogelea au kumgusa na kulia kila aina ya kilio wala hawezi kukujua sana sana utakuwa ni kama vile unapaka tu Rangi upepo?
Haya Waaga 'Marehemu' hebu nijibuni.