Nakuewa sana ulichozungumza na ndio maana nilisahihisha usemi wako kwamba bomba lilokwisha jengwa ni la Mafuta sio gas na halijawahi kutumika kupitishia gas, ila bomba la gas linategemewa kujengwa. Na hata hilo la Mafuta ni miles 800 ambazo hazitoki nje ya Alaska. ila ni kutoka machimboni kwenda pande mbili za ufukeni ambako mafuta hayo husafirishwa kwa meli. Hizo Miles 800 za bomba ziko within Alaska..tofauti nayojua mimi kati ya gas na oil ni combustion efficiency na physical form (one liquid while another gas) itokanayo na CH ratio! Lakini on economic sense pipeline ya oil inaweza kutumika kupitishia gas ndo maana nimetumia mfano huo! na pia on compression gas inaweza kuwa liquefied! Mjaribu kujiuliza kwanini mtu anafananisha the two jibu ni kwa vile logistics zake zinafanana
Halafu nikasema sababu za ujenzi wa bomba la gas ni kutokana na matumizi nchini Marekani tofauti kabisa na sababu tunazojenga sisi bomba la gas kutoka Mtwara kwenda Dar. Kutojenga bomba hilo ambalo linagharimu billions tungeweza kabisakununua mtambo mkubwa wa kuzalisha umeme pengine kutosheleza nchi nzima na umeme ukazalishwa Mtwara na kuunganishwa ktk grid ya taifa.
Na kama ya ujenzi wa bomba hili ni matumizi ya gas kwa wananchi majumbani (kama US) basi ingetakiwa ujenzi wa njia za kupitishia gas hiyo kwenda majumbani mwa watu mikoa yote kama unavyoona umeme (kuwepo na market ya kutosha kwanza) Halafu bomba hili ndio linakuwa kama grid ya taifa ktk usambazaji, hivyo bomba linapojengwa kutoka Mtwara hadi Mwanza kupitia Dar kwa malengo ya usambazaji wa Gas mikoani.
Kifupi mkuu wangu hatuna sababu ya maana kiuchumi kujenga bomba la gas kutoka Mtwara hadi dar wakati vyanzo hivyo vingeweza kabisa kuzalisha Umeme tokea Mtwara. Fikra hizi ndizo chanzo cha wananchi kuanza kudai Majimbo ama maendeleo mikoani kwa sababu gas hiyo inazinuaisha mikoa mingine wakati Mtwara wakizidi kudidimia.