Kuna faida gani kuwa Mtanzania?

Bitabo,
Faida zipo nyingi kuliko Hasara za kuwa Mtanzania, Kikubwa tuna faida ya kuwa waoga na kuwasujudia na kuwaogopa watawala na viongozi, na huku Uongozi ni dhamana ni sisi tumewaweka kwa ridhaa yetu, faida nyingine asilimia kubwa yetu hatujui Haki zetu za msingi na ndio maana tunatishwa na watawala wetu, faida nyingine wataalamu wetu hawaheshimiwi na kutumiwa ipasavyo, wanishia kutafuta ustaarabu nje ya nchi, faida nyingine Viongozi wana kauli mbiu Bora Kinywa Kiende Kinywani, mengine SIJUI
Faida nyingine kubwa tuna Katiba Nzuri sana ya toka enzi ya mkoloni ambayo imetuvusha miaka 50 bila kumwaga damu ila inazidi kuwekewa viraka na kumpa rais madaraka makubwa.
Tukija kwenye Hasara, tuna Madini mengi, utamaduni mwingi, tuna Amani na Uhuru
Nawakilisha


Kuna faida gani kuwa Mtanzania??
 
Kuna faida gani kuwa Mtanzania??

Swali zuri sana, ingawa kuna watu watakuja na majibu ya rejareja na wengine watajibu kwa jazba.

Binafsi sioni faida yoyote, kwa mfani mdogo nina jirani yangu hapa Dar ni raia wa uingereza anapata kila kitu kunizidi mimi mwenye nchi hata kwa mahitaji ya msingi kama maji, hewa safi, usalama, n.k

Yeye ana kipato kizuri wakati elimu na ujuzi namzidi, access to duty free shops, traffic barabarani wananisumbua mimi zaidi kuliko yeye, tusipolipa bili za maji dawasco, mimi nakatiwa huduma ya maji jirani yangu anapewa extension, benki mimi nanyimwa mkopo huku yeye akiomba anapewa, tukienda TIC yeye anapewa incentive nyingi kuliko mimi, vitalu vya madini kule Mererani sisi wachimbaji wadogo wadogo wazawa tulipokonywa akapewa yeye, ni rahisi yeye kuonana na RC/waziri hata Rais kuliko mimi, wakati mwingine kuonana kwao ni kwa kunywa tu kahawa lakini mimi ni kwa malalamiko ya msingi nk nk nk)
 
Faida ya kuwa mtanzania ni kuwa tayari kuwa punda au shamba la bibi. Faida ya utanzania ni ukondoo na kuishi kwa matumaini chini ya imani ya amani wakati wezi wachache na familia zao wakihomola huku wewe ukivujwa na dhiki za kutengenezwa na wao. Rejea wapemba walivyochuuzwa na Seif Sharrif Hamad wakamwaga damu ili awe nyumba ndogo ya CCM. Hata Lowassa pamoja na uchafu wake, kama Kikwete, bado ana watumwa na mateka wa kufua nepi zake za kisiasa. This is Tanzania which practically means Danganyika. I am just a philosopher.
 
faida wewe huzioni?,, au ungezaliwa burundi sidhani mpaka muda huu ukoo wako ungekuwa na watu hata 5. usimjaribu Mungu wako aliyekuweka ukazaliwa Tanzania
 
sWALI LA KIJINGA!
MUNGU ametuumba watanzania;jambo la muhimu ni kujiuliza jinsi ya kuisaidia nchi yetu isonge mbele!
huo ni mtazamo wako na usimwite mwenzako mjinga sababu mitazamo inatofautiana hata wew ulichoandika mwingine anaweza kukiona cha kijinga kama ujapendezewa na mada ni bora uka log off.
 
Back
Top Bottom