Kumzomea mtu asitoe mawazo yake ni kumyima haki ya kikatiba

Mbugi

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,488
257
Hivi karibuni hususani katika harakati za kutoa ama kupata maoni ya wananchi kumejitokeza kundi mahsusi la kuzomea na kuteka uhuru wa mtu asitoe mawazo yake, binafsi nawaomba watanzania wenzangu kuacha mara moja kwani kwa kufanya hivyo tunazuia uhuru wa mtu kitu ambacho ni kinyume na katiba ya nchi, na mbaya zaidi tunaona hata viongezi wetu kama Mbowe anaunga mkono kisanii kuwa eti ni UTASHI ("MOOD") ya watu sijui kwa kutoelewa au kuelewa katiba yenyewe au wanayoajenda ya siri ya aina yake kwa katiba wanayoitaka. kumbuka kuna wakati walijitokeza watu na kulalamika wananchi walipokuwa wanambeba mh. Mrema kampeni za 1995 lakini Baba wa taifa aliwaambia watu wasishangae kwani mbona hata maiti zinabebwa. kwa dhana hii acha watu waseme kwani hapo ndipo tutakapopata pumba na unga. cha msingi kama ni uwakilishi wa kivyama kutoa maono basi kila chama kitumie fursa hii vizuri zaidi kwa kupeleka watu imara katika kuelewa.
 
Back
Top Bottom