Kumnyenyekea mwenza wako siyo ubwege ni chachandu ya ndoa

IamBrianLeeSnr

JF-Expert Member
Nov 10, 2022
2,011
4,165
C091A972-CF0F-4F50-8350-EEA2C89455D3.jpeg

Mada ya leo inawagusa walio katika ndoa na wale wanaotarajia kuingia. Unapoingia kwenye ndoa kitu cha kwanza ni kufikiria jinsi ya kuilinda kwa gharama yoyote. Kuingia kwenye ndoa na kutoka baada ya muda mfupi ni kujitafutia gundu lisilo na sababu.

Tunapogeukia suala la ulinzi wa ndoa yako sasa, hivi utashindwa kweli kumnyenyekea mpenzi wako? Unatashindwa kumvumilia mpenzi wako eti kwa sababu utajihisi wewe ni mtumwa wa mapenzi? Mathalani mkeo anaumwa na kwa bahati mbaya hamna msichana wa kazi, je utashindwa kumsaidia kazi kama kupika, kufua, kuosha vyombo na kazi nyinginezo kwa sababu tu wewe ni mwanaume? Hii siyo sawa jamani.

Unyenyekevu
Watu wamekuwa wakilitafsiri tofauti neno hilo wakidhani eti kumnyenyekea mtu ni kuonesha ubwege uliopitiliza. Jamani kama mlikuwa hamjui, kumnyenyekea mumeo, mkeo ni moja ya chachandu ya ndoa. Bila kunyenyekeana hakuna mahaba na mahaba yanapokosekana ndoa haiwezi kuwepo.

Hivi usipomnyenyekea laazizi wako unataka ukamnyenyekee nani? Mumeo/mkeo ndiyo wa kumnyenyekea siku zote za uhai wako. Ndoa kubembelezana bwana, mpenzio akija na mawazo yake, mtu amemuudhi kazini hapo ndipo mahali haswa anapopaswa kumnyenyekea na kumrudisha katika hali nzuri.

Wewe ndiye unapaswa kumsahaulisha kabisa mambo yote yaliyotokea kazini. Mpokee kwa upole, mwambie pole, mkaribishe chumbani kisha mvue nguo zake na umpeleke bafuni mwenyewe. Anza kumwogesha bila kuzungumza naye maneno mengi.

Baada ya hapo mkaushe kwa taulo kisha mrudishe chumbani, mtolee nguo za usiku kisha mpeleke mezani kwa chakula. Baada ya hapo sasa mkiwa sebuleni mnaangalia TV muulize kwa upole: “Dear vipi, mbona leo naona siyo kawaida yako? Umechokachoka...kuna nini mpenzi wangu?”

Nakuhakikishia kwamba, kwa kauli kama hiyo hata kama alikuwa na tatizo kubwa anaweza kukujibu; “Ah kuna mtu aliniudhi kidogo ofisini lakini baada ya kufika hapa nyumbani najisikia amani sasa,” tena wakati anakuambia hivyo unaweza kushangaa hata uso wake unaanza kukunjuka. Hiyo ndiyo ndoa jamani.

Kuvumiliana pia muhimu
Maisha ya ndoa yanahitaji uvumilivu wa hali ya juu la sivyo siku mbili tu unaweza kuomba talaka kama siyo mwanaume kumkimbia mke. Ndoa ina mambo mengi sana, kutunza familia, kupeana haki za ndoa, kusaidiana na kuvumiliana katika vipindi vya dhiki na faraja na mengineyo.

Ukarimu, uaminifu, upendo wa kweli ni kati ya chachu za kudumisha ndoa na kwa kufanya hivyo haiwezi kuwa na migogoro isiyokuwa na lazima.

Unapooa au kuolewa lazima ufahamu kuwa unakuwa umejenga undugu baina ya familia yako na ya mwenzio. Katika kuishi kwenu huko utakutana na matabaka mengi, watu hutofautiana tabia.

Mfano wewe mwanamke umeolewa, mumeo akaleta ndugu, yaani wifi zako. Unatakiwa kuwasoma tabia ili uweze kuendana nao.

Ili kufanikiwa katika hili unapaswa kuwa na busara, uvumilivu, unyenyekevu na kuonyesha kuwajali, hii inaweza kukusaidia sana kwani watakapokutendea mambo ya ajabu nawe ukaanza kuwaropokea, utakuwa unajiingiza kwenye migogoro ambayo mwisho wake huweza kuwa mbaya zaidi kwako kuliko kwao.

Kumbuka Mungu ametuumba kila mtu na udhaifu wake, ndiyo maana unaona wanandoa wengi wanajikuta wakizikimbia ndoa zao kwa kutendwa na wandani ama ndugu wa wandani wao, wakati mwingine mume anaweza kuwa hajui, unayepaswa kumweleza ni wewe na unapomweleza lazima uzingatie heshima na busara ambayo haitaonyesha umedharau ukoo wao.

Siyo unaanza kusema; “Nyoo! Umeniletea ukoo wenu hapa, chakula hakitoshi! Nitawafukuza!” Kwa kauli hiyo utaonekana limbukeni, kaa naye chini zungumza naye kwa ukarimu, mweleze ni jambo gani linakunyima uhuru.

Usimfiche, mwambie; “Mume wangu, kuna jambo wifi amenitendea sijui kama anaona ni kosa lakini mie naona amenikosea, mweleze asirudie tena,” tena hakikisha wakati unamweleza hayo mpo peke yenu chumbani na huenda ni baada ya kumpa haki yake. Upo hapo?

Huo ndiyo uvumilivu ninaouzungumzia, siku zote wewe ndiye unayetakiwa kuwa na uchungu na ndoa yako. Kabla ya kuzungumza jambo lolote fikiria mara mbili, halitasababisha matatizo kwako? Ukipata matatizo au kuachika huyo wifi yako atakuwepo? Jibu ni hapana!

Kaa chini, fikiria kwa makini kabla ya kuamua jambo lolote linalohusu ndoa yako. Kumbuka kuwa kuingia kwenye ndoa ni kazi ngumu lakini kazi ngumu zaidi ni kuhakikisha unailinda.

Kwa leo nilitaka kuzungumzia hayo tu nikiamini kwamba ukiyazingatia wewe uliye katika ndoa yatakuwa ni yenye manufaa makubwa kwako.
 
Muda wa kumnyenyekea mwanamke ni wakati unataka au unahamu na kitumbua chake ukitafune na kukilamba lamba! 😂😂😂
Hatari sana mzee! Ndio maana na wao wamekua wanatupiga chenga sana na vizinga vya kutosha, Ile siku unapewa mzigo wanakua washajua hapa kuna kuachwa kwenye mataa au kung’ang’aniwa 😂😂😂
 
Siku mkinikuta namnyenyekea mwanamke mniite mbwa.
Mwanamke akizingua Ni kuzabwa makofi Hadi akili zimkae sawa.

Hawa viumbe Ni mawakala wa shetani ukianza kucheka cheka nao itakula kwako aisee!
Punguza temper jamaa vitu vimebadilika nowadays hawapigwi kizembe hao utajikua umepelekwa kwenye dawati la jinsia huku ukiomba msamaha
 
Back
Top Bottom