Kumfunga Maria jela miaka 22 kisa nyama ya swala ni matokeo ya kuwa na wanasheria waliokosa hekima na busara

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
24,044
71,289
Mijizi ya CAG mnaiacha inadunda mtaani mnakuja kumfunga Mwanamke ambaye hata hakujua ni nyama ya nini, mwanamke ambaye hata huyo swala hasingeweza kumkamata, mwanamke ambaye pengine yeye na Familia yake wanalala chini, mlo mmoja, kaletewa nyama ya mbuzi auze kumbe ni ni swala, yeye ni mkemia mpaka ajue huyu ni Swala?

Miaka 22 kwa nyama yenye thaman ya laki tisa?

Kwamba kupitia hiyo nyama, angekuwa tajiri kama walivyo majizi yenu ya CAG?

Upumbavu, ufedhuli, ujinga, ukosefu wa Hekima na Busara aliouonesha huyu Hakimu unaadhihirisha aina ya Wanasheria uchwara tulionao hapa Nchini.

1699276588668.jpg
 
Kifungu cha 326 sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kimewapa chumba mahakimu na majaji kutumia busara wanapotoa hukumu na kisha kuzingatia ,hali ya maisha ya mtuhumiwa, Ukubwa wa kosa,afya ya mtuhumiwa, kujirudia kwenye ukosaji na kuwahukumu wakosaji conditional dischage. Au masharti ya kutokutenda kosa kwa kipindi fulani.

Ukiangalia hali ya maisha na afya ya huyu mama hata kama alikuwa mkosaji na kweli alikamatwa na nyama ya Swala. Alitakiwa kuhukumiwa conditional discharge ili ajifunze na sio kifungo cha jela miaka 22 kwa kukutwa tu na kilo 22 za nyama ya Swala.
 
Kifungu cha 326 sheria ya mwenendo wa makosa ya jinai kimewapa chumba mahakimu na majaji kutumia busara wanapotua huku na kisha kuzingatia...
Hawa ni aina ya mahakimu ambao Sheria haipo kichwan, ni wapuuzi wanaotembea na tukanuni twaao kichwan,, Sina shaka ukifatilia hukumu za huyu mpuuzi, utagundua zote zinafanana.

Hivi Kwa hali ya kawaida, mwanamke alochoka kama huyu, hata km kakukutwa na nyama ya Swala, ni wakumfunga miaka 22?

Kwa mwanamke, kitendo tu cha kusota mahabusu kipindi chote cha kesi, kimetosha kumfundisha
 
Nikikumbuka kisa cha yule mdogo wake Rostam Aziz (Akram Azizi) na yale mabunduki yake lukuki ya ujangili! Halafu mwisho wa siku kesi ikaisha kwa CCM kupewa kituo cha habari cha Channel 10!

Na pia yule mbunge wa kanda ya Ziwa aliyekamatwa red handed na nyara za serikali! Na yeye mwisho wa siku akaachiliwa! Halafu unakuja kuwaona Watanzania maskini wanafungwa miaka kibao jela kwa sababu tu ya kukamatwa na nyama za porini, unaona kabisa hii nchi ina matatizo makubwa katika mifumo yake ya kisheria.

Yaani sheria zake nyingi zipo kwa ajili ya kuwabana/kuwakandamiza watu masikini. Ila siyo matajiri na vigogo wa chama na serikali.
 
Mijizi ya CAG mnaiacha inadunda mtaani mnakuja kumfunga Mwanamke ambaye hata hakujua ni nyama ya nini, mwanamke ambaye hata huyo swala hasingeweza kumkamata...
Ukiangalia kwa makini saana, mfungwa wa Africa ni mtu masikini asiyekuwa na mwelekeo wa maisha., ila wale kina Mubaba, Fisadi, Mtawala hata aiibe serikali nzima na kuiuza daima hana hatia.

Imagine mtu kakamatwa na kipande tu cha nyama ya swala anakula miaka 22, wakati huo huo kuna mijamaa mijike kwa midume yamepiga billion za kutosha mpaka kesho inaendelea kula mema ya Nchi na hakuna wakuyagusa. Kelele tu kelele tu kelele tu mwisho wa siku kimyaaaaaa kama usiku wa giza.

Eti kuna mihimili mitatu, Serikali, Mahakama na Bunge., Ujinga tu.
 
Hatafungwa kifungo hicho. Ila lazima umma utangaziwe maamuzi ya mahakama. Huyu atakwenda kukaa mahabusu kama wiki tu kisha atatoka ili next time awe makini na wanyama pori

Sheria ni lazima ziwe kali ili kuwalinda wanyana pori sababu tukicheka na hawa raia wadogo wanaozunguka mbunga miaka 10 ijayo wakiwekeza maisha yao kwa hao wanyama hamtaamini namna namna watawatokomeza pia usisahau swala la magonjwa ya mlipuko kutokana na kula nyama ambazo hazijathibishwa ubora wake.

Kwa kifupi tusiwe wepesi sana wa kuleta hisia katika maswala ya kisheria. Huu mchezo wa kuleta hisia ndio chanzo cha rushwa na utendaji mbovu wa mamlaka za serikali sababu wanainchi ndio mstari wa mbele kuwatetea wakosaji sababu wanatia huruma wakitiwa mbaroni.
 
Back
Top Bottom