Kumekucha: Iran yashambulia meli za Marekani kwa makombora makali

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,045
18,014
Iran imeshambulia kwa makombora makali meli bandia ya kivita ya Marekani katika mlango bahari wa kimkakati wa Hormuz.

Zoezi hilo lilishirikisha mashambulio makali hatua iliofanya kambi mbili za Marekani kujiweka katika hali ya tahadhari.
Jeshi la Marekani lilishutumu tabia hiyo mbaya iliotekelezwa na Iran ikiitaja kama jaribio la kutishia na kichokozi.
Zoezi hilo linajiri wakati ambapo kuna hali ya wasiwasi kati ya Tehran na Washington katika eneo la Ghuba.

The Iranian military fires a missile targeting the replica

CHANZO CHA PICHA, EPA Maelezo ya picha: Wanajeshi wa Iran walirusha makombora wakilenga meli ya Marekani
Meli hiyo ya kivita inayofanana na ile ya Marekani ambayo mara nyingi hutumiwa kubeba ndege za kivita inaonekana ikiwa imebeba ndege bandia ikiingia katika eneo la Ghuba.

Makombora baadaye yanarushwa kutoka maeneo tofauti ikiwemo mengine ambayo yanailenga meli hiyo.

A missile is fired from land

CHANZO CHA PICHA,EPA. Maelezo ya picha,
Makombora pia yalirushwa kutoka ardhini. Kombora jingine ambalo linarushwa kutoka kwa ndege aina ya helikopta linaonekana likipiga upande mmoja wa meli hiyo bandia.

Kile kilichooneshwa katika zoezi hilo yalikuwa mashambulizi kutoka angani na kupitia wanamaji, alisema kamanda wa jeshi la Iran la Revolutionary Guard Jenerali Hossein Salami akizungumza na runinga ya taifa hilo.

Iranian soldiers jump on the mock carrier

CHANZO CHA PICHA,EPA. Maelezo ya picha
Wanajeshi wa Iran waliruka kwenye meli ya Marekani
Shambulio la kombora la masafa marefu liligunduliwa hatua iliowafanya wanajeshi wa Marekani kuchukua tahadhari katika kambi zao za UAE na Qatar, lilisema jeshi la Marekani.

''Marekani hushirikiana na mataifa mengine kufanya mazoezi ya kukuza usalama wa baharini ili kuunga mkono uhuru wa meli kusafiri, huku Iran ikifanya mazoezi ya kushambulia, ili kujaribu kutishia na kuchokoza'', alisema kamanda Rebecca Rebarich, msemaji wa jeshi la wanamaji wa Marekani akiwa nchini ya Bahrain.
 
Attachments

  • _113691462_mediaitem113691461 (1).jpg
    _113691462_mediaitem113691461 (1).jpg
    50.1 KB · Views: 2
Iran imeshambulia kwa makombora makali meli bandia ya kivita ya Marekani katika mlango bahari wa kimkakati wa Hormuz.
Zoezi hilo lilishirikisha mashambulio makali hatua iliofanya kambi mbili za Marekani kujiweka katika hali ya tahadhari.
Jeshi la Marekani lilishutumu tabia hiyo mbaya iliotekelezwa na Iran ikiitaja kama jaribio la kutishia na kichokozi.
Zoezi hilo linajiri wakati ambapo kuna hali ya wasiwasi kati ya Tehran na Washington katika eneo la Ghuba.
The Iranian military fires a missile targeting the replica

CHANZO CHA PICHA,EPA
Maelezo ya picha,
Wanajeshi wa Iran walirusha makombora wakilenga meli ya Marekani
Meli hiyo ya kivita inayofanana na ile ya Marekani ambayo mara nyingi hutumiwa kubeba ndege za kivita inaonekana ikiwa imebeba ndege bandia ikiingia katika eneo la Ghuba.
Makombora baadaye yanarushwa kutoka maeneo tofauti ikiwemo mengine ambayo yanailenga meli hiyo.
A missile is fired from land

CHANZO CHA PICHA,EPA
Maelezo ya picha,
Makombora pia yalirushwa kutoka ardhini
Kombora jingine ambalo linarushwa kutoka kwa ndege aina ya helikopta linaonekana likipiga upande mmoja wa meli hiyo bandia.
Kile kilichooneshwa katika zoezi hilo yalikuwa mashambulizi kutoka angani na kupitia wanamaji, alisema kamanda wa jeshi la Iran la Revolutionary Guard Jenerali Hossein Salami akizungumza na runinga ya taifa hilo.
Iranian soldiers jump on the mock carrier

CHANZO CHA PICHA,EPA
Maelezo ya picha,
Wanajeshi wa Iran waliruka kwenye meli ya Marekani
Shambulio la kombora la masafa marefu liligunduliwa hatua iliowafanya wanajeshi wa Marekani kuchukua tahadhari katika kambi zao za UAE na Qatar, lilisema jeshi la Marekani.
''Marekani hushirikiana na mataifa mengine kufanya mazoezi ya kukuza usalama wa baharini ili kuunga mkono uhuru wa meli kusafiri, huku Iran ikifanya mazoezi ya kushambulia, ili kujaribu kutishia na kuchokoza'', alisema kamanda Rebecca Rebarich, msemaji wa jeshi la wanamaji wa Marekani akiwa nchini ya Bahrain.
Kweli ashki majunun 😲😜
Hiyo ni meli bandia ya iran ambayo walikuwa wanafanya luteka!
ww unasema kumekucha?! Kelele za mlango hazimnyimi usingizi mwenye nyumba usingizi anapata usingizi mnono😀😀
 
Hiyo ni "replica", sio halisi. Ni sawa na mimi kupiganw na "toy" then nijisifu
Aircraft carrier haiachwi kijinga namnz hiyo, inazo defence systems, detection mechanism, radar etc, sio meli za wavuvi zile, grow up
 
Yaan hayo mazoez marekan anaelewa Zaid kuliko ss huku jamii foram ambao hatuna uelewa wamambo yakijeshi nandomaan jemeral mmoja wakimarekan alioko bahrein alisema walijiweka tayar Kwa dakika kadhaa wakihof Kuna jambo linaweza kutokea baadae wakajiondoa kwenye uhatar huo
 
Hiyo ni "replica", sio halisi. Ni sawa na mimi kupiganw na "toy" then nijisifu
Aircraft carrier haiachwi kijinga namnz hiyo, inazo defence systems, detection mechanism, radar etc, sio meli za wavuvi zile, grow up
Boxers hua wanapiga ngumi vitu gani mazoezini kabla ya kuingia kwenye ring kwa mpambano?
 
Back
Top Bottom