Kumbukumbu za Muziki na Matukio

josephdeo

Member
Nov 23, 2015
95
196
• Ace hood-hustle

Mama need house,
Babe need some shoes

Hustle, hustle hard!.. hustle, hustle hard!

Hakaika kila niisikiapo nyimbo hii ni lines hizo ambazo naweza kuziimba kwa sauti ya juu. KWANINI?!!

#NYIMBOnaMATUKIO

Around 2013 kipindi hiki nilikuwa na babe fulani ambayo hatukuwa serious sana ila tulihave funny. Nilikuwa form III huku yeye akiwa na mtoto tayari pia saluni yake. Ila fresh nilikuwa naendesha hilo ndiga barida kabisa (stori ya nilimpataje itakuja nikipata nyimbo itakayo nikumbusha hilo).

Fast forward ni kuwa wakati fulani tukiwa kwenye hiyo relationship nilipigwa mzinga. Tena kikosi hicho cha mizinga kiliongozwa na mtu mzima mwenyewe Kalapina. Babe alitaka kufanya birthday party ya dogo (mtoto wake). Ila kuna baadhi ya pesa ilimpungua.

Ikatikiwa pesa na nilipewa siku moja tu kuhakikisha pesa inapatikana. Achana bhana na penzi la mashangazi yanajua Nini maana ya kucare. Ikanibidi nipambane ili jua la kesho niwe na ile pesa mkononi, taarifa nilipewa mishale ya saa kumi na mbili jioni mara nilipokuwa natoka shule.

Nikawa na masaa kumi na mbili ya kuhakikisha napata pesa vinginevyo ningenuniwa kwa takribani mwezi na siku zake kadhaa. Nami sikutaka kukaa mbali na Raha zake kwa kipindi hiko huku nikiwa na kazi nyingine ya kuomba msamaha kwa magoti. Ambition ikawa ni kupambana ili tu nipate mkwanja na kuepusha minuno.

Nafika maskani ilikuwa tayari ni saa moja jioni na hakukuwa na kibarua chochote kwa mda kama ule. Nami sikuwa na chochote na hata jumba hilo bovu nilipoliangusha kwa kaka zangu wawili nao hawakuwa na kitu. Akiba ya Bi mkubwa nayo ilikuwa haina kitu huku ikining'ong'a.

Hata nilipochungulia simuni hakukua na muamala funny thing Ni kuwa pale nyumbani ni mimi pekee ambaye nilikuwa nikiifahamu namba ya Siri ya mama kwa m-pesa. Siunajua siku ya nyani kufa miti yote uteleza. Sikuwa na namna zaidi ya kutumia akili niipate hiyo pesa.

Nini cha haraka nifanye ili nipate kibunda cha fasta ili kusolve hiyo inshu. Nikapata inshu fulani ambazo tulikuwa tukipiga kitambo mimi na bro. Kuiba mabomba yanayopeleka maji kwenye nyumba za watu na kumuuzia bosi wetu aliokuwa akifanya biashara ya usambazaji wa maji majumbani.

Katika harakazi zangu za mtu mweusi nilikuwa nimewahi kuona bomba fulani mitaa ya Bugarika likiwa halijafukiwa. Yaani lilikuwa linaelea juu juu na hayo ndio tulikuwa tukiyakata. Bro hakakubali mpango ule kwa kunisaidia, family first. Tukayasubiri masaa yasogee mpaka mida ya wanga hapo ni saa saba za usiku. Upepo unavuma mji umetulia na watu wamepumzika. Ila kwetu ulikuwa rasmi mda wa kazi.

Tukavua nguo kisha tukabakiza boksa tu na tulitakiwa kutembea umbali wa km 5 ili kufika eneo bomba lile lipo (tulitembea na boksa pekee). Eneo tuliloenda kufanya wizi huu ni Bugarika (hili ni eneo ambalo hawakuwa na mchezo kabisa linapokuja swala la wezi, walijaa wakurya wengi).

So tumefika eneo la tukio barida tuko na visu. Hatukujua kuwa ile nyumba ililindwa na mbwa karibia sita tena wale wakali. Hatukuwa tumelifahamu hilo. Tukajigawa kwa kuangalia ukubwa na pesa tutakayolipwa. Tamaa mbaya kwani licha ya kuwa tulipata ukubwa ulitosha kabisa ila tamaa ikatufanya tuongeze vipimo.

Tukajikuta tukiifikia nyumba ambayo lile bomba lilielekea. Ile tumekata na maji yameanza kumwagika kwa presha kubwa. Ikawaamsha wale waliokuwa ndani na yule mzee alipoona watu akaamrisha mbwa wake huku akipiga yowe la moto. Nadhani Usain Bolt alijifunzia kwangu mbio, nilitimua mbio ambazo sikuwahi kuzikimbia hapo awali. Kisu mkononi na nilikuwa na boksa huku weusi wangu ukinisaidia na nyuma niliisikia yowe la watu.

Mbwa wako maili kadhaa nyuma yangu huku wakifuatiwa na wananchi wenye hasira kali. Hapo sijui hata bro alikuwa wapi bali niliangaika kuyaokoa maisha yangu, nilikimbia. Mbio za mashindano kabisa mbwa zikawa zinawapa msaada wananchi na kujua nilikuwa wapi, jegrafia ya jiji la Mwanza nimilima na Mimi nikiaipandisha majabali kama nilikuwa nikicheza.

Ilikuwa hatari kamili na baada ya kupita huku na kule nikafanikiwa kuwachenga wale raia huku mbwa nikizishambulia kwa mawe. Ulikuwa usiku wa kukumbukwa kwangu ila kamwe kumbukumbu hizi zinachangizwa na namna bro alivyofika nyumbani na kipande cha bomba tulilokuwa tumelikata.

Hata hatari zile zote bado yeye aling'ang'ana na bomba lile na kufika nalo nyumbani. Kesho yake tukaliuza na nikasolve ule msala wa shangazi. Hii ni kati ya hustle ya hatari zaidi kuwahi kuifanya ambayo iliyaweka maisha yangu kwenye risky kisa pussy..
 
Dah mwamba kama kachupi unakumbuka picha la stering kachupi? Imegin mbwa wamekukaribia afu wameshika boksa katika kujikwamua wamechana ila nini we msengeee unahatar teh teh teh
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom