Kumbukizi: Nyimbo za Chrismas za Jim Reeves na Abba group

Ni mwezi wa 12 tena, miaka inaenda na kupita, nyakati hizi za mwezi wa sikukuu za Christmas na mwaka mpya.. Mbali na nyumbani, kumbukizi ya nyakati njema za furaha
Na wazazi ambao wengine hawapo tena!
Na marafiki
Na majirani
Na ndugu ambao hamjaonana mwaka mzima
Na wageni toka mijini
Shangwe na furaha karibia kila nyumba, kijiwe
Ni mapishi na vinywaji kila nyumba, kualikana na kusalimiana
Kupeana zawadi mbalimbali

Kila kona ni nyimbo za Christmas za waimbaji maarufu Jim Reeves, Abba group, kwenye radio cassete za majumbani na miziki sehemu za starehe na matoroli ya kuuzia kanda hizo Na vibanda pia

Matoroli hayo yana redio cassete zenye nishati ya betri..wanapita mitaani radio zinaimba na watu wanatoka majumbani kununua kanda
Ni mwezi wa furaha na kusahau machungu mengi ya mwaka mzima, misiba na magonjwa, mahusiano na kushindwa kwenye mengine

Watoto wamejazana mitaani, wanacheza kwa furaha, wanasimuliana mengi! Hakuna smart phone za selfie.. Makamera men wanapita mitaani kuwapiga picha watu

Majumbani miti ya Christmas ile halisi inapambwa na mapambo halisi ya kutengenezwa majumbani na maua halisi ya kupandwa majumbani.. Nyumba zina mwanga, zina nuru zina furaha

Nyakati zimebadilika mno na haya yote hayapo tena! Zimebaki kumbukumbu zenye kutia simanzi mno...!

 

Attachments

  • Jim Reeves - The Merry Christmas Polka.mp3
    4.3 MB
Christmas
C is for the christ child born upon this day
giphy.gif
 
Lazima kuuzunika kupo tukikumbuka yaliyo pita pesa haikuwa sana na nafasi hili upate furaha upendo ulikuwa mwingi sana
Ni kweli kabisa pesa haikuwa kila kitu, kwenye sherehe watu walijitolea kuni, maji, mapishi sahani nk.. Leo hii kila unachogusa ni shekeli
 
Back
Top Bottom