Kumbe wengi hugombea Ubunge ili wawe Mawaziri, kauli za Nape na Dkt. Mollel ni ushahidi tosha

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
85,074
143,890
Ndiyo sababu wabunge wetu wanakuwa machawa na ndondocha za Rais! Kila ujinga wa serikali wao ni "Ndiyooo"!
 
Uongozi haupimwi kwa matamanio ya mtu binafsi.

Uongozi unapimwa kwa uwezo wa mtu binafsi.
 
Mleta made unasema hutaki mawaziri wawe wabunge, nakuunga mkono kwenye hilo tu, mengine kivyangu nayaona ni porojo tu.

Lakini hujasema wapatikane vipi? Maana usiruke mavi ukaingia shimo la choo.
 
Mleta made unasema hutaki mawaziri wawe wabunge, nakuunga mkono kwenye hilo tu, mengine kivyangu nayaona ni porojo tu.

Lakini hujasema wapatikane vipi? Maana usiruke mavi ukaingia shimo la choo.
Hata hilo Moja si haba 😀😀
 
Na mawaziri wenyewe ni kuridia rudia mle mle utafikiri PDF lazima iagizwe toka Marekani kwa dolla.
 
Mleta made unasema hutaki mawaziri wawe wabunge, nakuunga mkono kwenye hilo tu, mengine kivyangu nayaona ni porojo tu.

Lakini hujasema wapatikane vipi? Maana usiruke mavi ukaingia shimo la choo.
Wawe ni wa kuteuliwa kutoka popote, kama ilivyo marekani ila bunge ndilo liwazibitishe, kwa sasa mtu akishakuwa mbunge jua ni chawa wa rais.
 
Wawe ni wa kuteuliwa kutoka popote, kama ilivyo marekani ila bunge ndilo liwazibitishe, kwa sasa mtu akishakuwa mbunge jua ni chawa wa rais.
Tanzania hii mtu apelekwe n a rais akathibitishwe nani wa kumzuwia? Jamani hii ni Afrika siyo Ulaya.

Ni heri kama hivi sasa, kuchaguliwa wagombee kwa wananchi huko, wakichaguwa mabomu ni wananchi wenyewe.
 
Rais ni lazima awe na jopo lake la wasaidizi ambao ni mawaziri, anaowataka yeye. Hata kocha tu wa mpira huwezi kumchagulia wasaidizi.

Kinachotakiwa kufanyika, ambacho mimi naamini kinawezekana, ni sheria kali za kuwajibishana. Na Rais apunguziwe majukumu, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya wawe wanachaguliwa kwa kura. Na wao wawe na mabaraza yao, kama vile madiwani. Wawe magavana na sio vingine.

Rais pia apunguziwe madaraka, mpaka wakurugenzi, makatibu wakuu achaguwe yeye, hii iondolewe. Waziri husika ndiye achaguwe team yake.
 
Rais ni lazima awe na jopo lake la wasaidizi ambao ni mawaziri, anaowataka yeye. Hata kocha tu wa mpira huwezi kumchagulia wasaidizi.

Kinachotakiwa kufanyika, ambacho mimi naamini kinawezekana, ni sheria kali za kuwajibishana. Na Rais apunguziwe majukumu, wakuu wa mikoa, wakuu wa wilaya wawe wanachaguliwa kwa kura. Na wao wawe na mabaraza yao, kama vile madiwani. Wawe ma gavana na sio vingine.

Rais pia apunguziwe madaraka, mpaka wakurugenzi, makatibu wakuu achaguwewe yeye, hii iondolewe. Waziri husika ndiye achaguwe team yake.
Una hoja usikilizwe!
 
Back
Top Bottom