Fred Mpendazoe
Member
- Aug 21, 2016
- 33
- 504
Mwaka 1992 nilipokuwa nimemaliza masomo yangu Chuo kikuu cha Leeds Uingereza, nilienda nyumbani na nilimtembelea rafiki yangu huko kijijini ambae nae alikuwa amemaliza masomo yake huko Urussi. Baada ya kukaa kama saa moja hivi niliona hali ambayo ilinishangaza sana. Rafiki yangu huyu mara kwa mara katika maongezi alikuwa akichanganya lugha.
Mara aongee kirussi wakati wazazi wake hata Kiswahili kilikuwa cha shida. Mara aongee kingereza. Baadae ndugu zake na wazazi wake waliniuliza, mbona wewe unaongea kiswahili tu wakati na wewe umesoma ulaya kama wenzako ? Mimi nilinyamaza tu kwani hata mimi hali hiyo ilikuwa imenisikitisha sana.
Rafiki yangu huyu aliajiriwa kwenye Kiwanda cha bia huko Mwanza. Mimi niliajiriwa Kampuni ya Sukari kilombero. Baada ya muda mfupi nikaambiwa kwamba alitelemshwa cheo kutoka Mhandisi wa Kiwanda hadi Mhandisi wa kawaida na nafasi yake ilichukuliwa na kijana aliyekuwa na diploma ya kutoka Chuo cha Uhandisi Dar es salaam.
Nilipofuatilia niliambiwa kwamba hakuonyesha uwezo kama aliyemaliza mafunzo ya digrii, isipokuwa alikuwa na majigambo makubwa. Alijisikia sana na kuonyesha dharau kwa watanzania waliosoma Tanzania. Alitaka atambuliwe kama alisoma nje ya nchi Urussi na aliona fahari sana kuongea kirussi hata amabapo hapakustahili aongee kirussi.
Nilielezwa, alipoajiliwa, kwenye vikao alitaka aonekane amesoma Urussi. Mara kwa mara ajifanya kama amesahau hivyo anazungumza kirussi badala ya Kiswahili au kiingereza. Lakini kibaya zaidi uwezo wa kazi ukawa mdogo sana. Akashushwa cheo. Baadae akafukuzwa kazi.
Mkasa huu wa kweli naufananisha na watanzania ambao wanaona fahari sana kuongea kiingereza na wangependa hata Bunge letu litumie kiingereza badala ya lugha ya taifa ya Kiswahili. Siku moja niliona kwenye mitandao ya kijamii eti Breaking news: “Mwanasheria wa UKAWA awazidi mawakili wa serikali katika kujibu hoja kwa kiingereza”.
Siku nyingine nikaona tena Breaking news: Kwenye mkutano wa UN Tanzania haijawakilishwa na inaonekana UN wanatumia kiingereza siyo kiswahili..” Pia kuna vikatuni vya kijinga tu vimewekwa kwenye mitandao. Katika katuni hizo na breaking news hizo, ujumbe unaonekana ni kwamba watanzania hawa kuhawaoni fahari ya Lugha yetu ya Taifa ya Kiswahili bali wanatukuza lugha ya kiingereza. Inasikitisha na ni aibu.
Nadhani wakati umefika, tuone fahari kwa viongozi wa kitaifa kutumia lugha ya Kiswahili wanapotembelewa na viongozi wa nchi za ulaya na marekani hapa nchini. Na wanapokwenda nje ya nchi wahutubie Kiswahili kwa sababu imekubalika kwenye UN na AU kiswahili kitumike. Nchi nyingi za Afrika zimeanza kujiandaa na hali hii.
Tanzania ndiyo chimbuko la Kiswahili lakini baadhi ya watanzania hawaoni fahari na lugha ya Kiswahili ambayo nchi nyingine za Afrika na ulaya na marekani wanatamani kuielewa kwa ufasaha.
Zipo nchi hazishabikii lugha ya kiingereza au lugha za kigeni na pia zimepiga hatua kimaendeleo. Mfano China, Korea, Japani, Urussi na Ujerumani.
Nchi hizi zinaheshimu lugha zake za asili, na wanapokwenda kwenye mikuatano ya kimataifa wanatumia lugha zao. Na wanaona fahari kufanya hivyo. Lakini hapa Tanzania kumbe wapo watu amabo kifikra bado wanatawaliwa na wakoloni. Wanaona fahari sana kuongea kiingereza. Na watamani hata Bunge litumie kiingereza na ofisi za serikali zitumuie kiingereza na hata hafla za kitaifa kitumike kiingereza.
Tatizo walilonao baadhi ya watanzania hawa ni fikra zilizokuwa zimepandikizwa wakati wa mkoloni kwamba ukijua kuongea kiingereza basi unaonekana msomi na umeendelea. Huo ni ulimbukeni kama aliokuwa nao yule rafiki yangu. Alijionyesha amesoma kwa kuongea kirussi mahali pasipostahili akadharau hata lugha yake, lakini baadae ikaonekana hata uwezo hakuwa nao.
Kwa mtu lugha ni mhimu katika kuwasiliana lakini mhimu sana kwa mtu ni kuwa na hekima, maarifa, ujuzi na busara katika kufanya maamuzi na uwezo wa kusimamia maamuzi hayo. Na kwa nchi ni hivyo pia. Nchi itapiga hatua kimaendeleo kama ina rasilimali watu wenye maarifa, ujuzi, viongozi wenye hekima na waliojitoa na wenye kufuatilia maamuzi yaani uongozi bora. Tanzania imeanza kusika duniani nkote kwa uongozi mahiri unaoonyeshwa na Raisi Magufuli. Ni kweli.