Kumbe nomino "chai" tumetohoa toka India

Lucchese DeCavalcante

JF-Expert Member
Jan 10, 2009
5,471
734
Hivi karibuni nimekuwa nikifuatilia tamthilia mwanana ya India a Love Story kikautana na neno "chai" likitumika sana nikagundua kumbe hata sie waswahili tumetohoa toka kwa wenzetu wa India... Soma zaidi kuhusu Chai Masala
 
Hata wao walitohoa kutoka kwenye kichina (Tcha)
 
no language is complete by itself...juzi jumamosi nimesikia tumetohoa juice na kuita juisi kwenye kiingereza na kwamba kitu hicho hicho unaweza kutohoa kiarabu chake ukaita sharubati kumanisha juisi.
 
Hivi karibuni nimekuwa nikifuatilia tamthilia mwanana ya India a Love Story kikautana na neno "chai" likitumika sana nikagundua kumbe hata sie waswahili tumetohoa toka kwa wenzetu wa India... Soma zaidi kuhusu Chai Masala
Mbona maneno mengi tu tumetohoa kutoa India...!

Mfano wa baadhi ya maneno ni kama: Chapati, Biriani na mengine mengi.
 
Lugha mara nyingi zinaingiliana kwa sababu moja ama nyingine....neno chai linatumika na wahindi =chai,waarabu =shai,waturuki =tsai,wagiriki=tsai nadhani itakuwa ni kizungu ukuti tukitafuta nani kachukua kwa mwenziwe.
 
Wachina ndio walio tohoa na si Wahindi.

Ndio, inawezekana. Maana nchi zenyewe ni majirani.
Hata hivyo tafiti nyingi za kisayansi kuhusu Tea (Camellia sinensis) zinaelemea zaidi kwa Uchina kama "origin" of Tea.

Hata hivyo cha muhimu ni kukubali kuwa lugha yoyote lazima itachukua maneno kutoka kwenye lugha zingine. Na haimaanishi kwamba lugha inapokuwa ina maneno ya kuazima basi si ya muhimu, na kwamba labda ile lugha ambayo ndio asili ya maneno mengine ya lugha zingine basi ni bora zaidi. Kwa jamii yetu ya kiTZ pamoja na kwamba lugha yetu ya kiswahili ni changa na ni mchanyato wa lugha zingine, bado ni lugha bora kwa jamii yetu. Kama ambavyo kifilipino ni bora kwa wafilipino kuliko lugha zingine.
 
hakuna lugha isiyotohoa maneno kutoka lugha nyingine

NENO cHAI LINA ASILI YA KICHINA
 
Ndio, inawezekana. Maana nchi zenyewe ni majirani.
Hata hivyo tafiti nyingi za kisayansi kuhusu Tea (Camellia sinensis) zinaelemea zaidi kwa Uchina kama "origin" of Tea.

Hata hivyo cha muhimu ni kukubali kuwa lugha yoyote lazima itachukua maneno kutoka kwenye lugha zingine. Na haimaanishi kwamba lugha inapokuwa ina maneno ya kuazima basi si ya muhimu, na kwamba labda ile lugha ambayo ndio asili ya maneno mengine ya lugha zingine basi ni bora zaidi. Kwa jamii yetu ya kiTZ pamoja na kwamba lugha yetu ya kiswahili ni changa na ni mchanyato wa lugha zingine, bado ni lugha bora kwa jamii yetu. Kama ambavyo kifilipino ni bora kwa wafilipino kuliko lugha zingine.
Ni kweli maneno yako...!

Kuna HII thread HAPA
, unatakiwa kuorodhesha maneno ambayo unahisi yameongezwa au kutoholewa kutoka kwenye Lugha nyingine na kuingizwa kwenye Lugha ya Kiswahili, hayo maneno aidha yawe yametoka kwenye Lugha ya kimataifa au Lugha za Asili ya makabila yetu ya kiafrika.
 
Back
Top Bottom