Kumbe ni Dk Mukama

Ulimakafu

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
29,046
10,693
Jana wakati wa taarifa ya habari ya ITV saa mbili usiku, walimripoti katibu mkuu wa CCM Wilson Mukama kwa kumtaja kama Dk wakati akiongea na wana CCM wa chuo kikuu Mzumbe,mi nishangaa na sikuwahi kufahamu kuwa ni daktari.Mwenye kujua tafadhali.
 
hata mimi nilishangaa sana. Awali nilifikiri wamekosea lakini waliporudia mara tatu nikajua wamemaanisha!! Mwenye Academic background yake naomba atuwekee humu!! sifa za kijinga hatuzifagilii!!
 
Wale walikuwa ni mature entry wa CCM kwa kweli sikuaona vijana wengi zaiidi ya aliyesoma risala
 
Kuna wakati VOA walikuwa wanajadiliana na Mhadhiri wa UDSM Bashiru Alli na kumwita Prof. wakati nijuavyo mimi hata PhD hana. Inawezekana kupachikana titles kirahisi kama hivi. Mwacheni Mukama aitwe Dk - suala ni je ana- behave hivyo?
 
Duuh kwa hiyo ccm wanama-Dr. wengi kuliko UDSM? Kazi ipo bado Nape nae apewe udokta wake wa kuwavua mapacha Magamba akifuzu hilo nafikri atagraduate
 
Siyo mbaya kwa huko CCM maana pia naye Prof. Maji Marefu siku zina hesabika tutakutana 2015
 
Hivyo ndo vyombo vyetu vya habari, mbona mpaka leo lowassa tbc1 wanamwita waziri mkuu mstaafu.inawezekana na hapo wameamua tu.
 
CCM wanadhani matumizi ya titles hizi ndiyo wataaminika kwa Watanzania . Ni aibu sana na hasa huko TBC sijui wako vipi tabia zao .
 
Nyerere alikuwa na honorary degrees za kutosha zaidi ya kumi (km huamini search kwny google uangalie wikipedia)...lakini hakuwa akijiita dokta km hawa mambumbu wasio hata na hadhi! alikuwa ni msomi wa ukweli wa masters of arts economics & history..achilia mbali vitabu alivyoandika yeye binafsi.! hawa wa sasa ni wajinga na wapenda anasa tu
 
kilichonichekesha jana ni pale mukama aliposema eti wanaCCM wawili au wa 3 ambao ni mafisadi hawawezi kusababisha jahazi zima lioze, yaani km yeye sio gamba vile. hahahahahaha...............
 
Hahhaha! ukienda msibani kama huwezi toa machozi basi paka hata maji machoni, au mmesahau ukiwa kwenye mkutano wa walemavu wa macho (blinds) basi nawe fumba jicho lako! mkama alikuwa anahutubia"wasomi" wa CCM so ili nae aonekane msomi ilibidi ajipachike u Dokta, so msishangae siku mkisikia ni Mchungaji, Shekhe au hata nabii hawa jamaa hubadilika kutokama na mazingira tu!
 
Inakuwaje wazee? DR Mukama anashindwaje kuwapa mapacha watatu barua ilhali jana katamka mafisadi wawili au
watatu hawawezi kusababisha jahazi kuzama.Acheni pumba mnashindwaje kujivua gamba?
Ila kama mpo serious mkimpa MAMVI barua ya kumvua gamba imekula kwenu mchana kweupe atawalipua ile mbaya
si ajabu hata Bw Mkubwa nae akatoka nduki.
 
Ukiwa ccm u-Dr unaweza kuupata kirahisi sana,ukiweza hata kumtukana Freeman Mbowe kesho unatangazwa Dr!! Shame on ccm`s!!!!!!!!!
 
hata mimi nilishangaa sana. Awali nilifikiri wamekosea lakini waliporudia mara tatu nikajua wamemaanisha!! Mwenye Academic background yake naomba atuwekee humu!! sifa za kijinga hatuzifagilii!!
Kwani wingi wa MaDr ndo suluhisho la matatizo yetu au ndio kunachochea kuongezeka kwa ufisadi?
 
Back
Top Bottom