Kumbe kuoa ni kugumu hivi? Aisee mniombee niko hoi bin taabani

Bilionaire kekeman

Senior Member
Nov 26, 2022
142
823
Hivi nyie wana mliokaa kwenye ndoa zaidi ya miaka kumi mmefanyeje aisee? Yaani sio poa wakuu yaani niko hoi bin taabani ndiyo kwanza ndoa yangu ina wiki mbili tu aisee najihisi kuchoka na kukata tamaa wakuu.

Majukumu yamenizidi, nakosa uhuru wa kuamua mambo yangu eti lazima mshirikishane wote kwenye nyumba yaani hapa nipo hoi bin taabani fanyeni wana wajamii forum mninusuru mambo sio poa niko chupli chupli mambo yamekwama wakuu.

Ndiyo kwanza nina miaka 27 yaani naona mambo yamenielemea majukumu yanakuwa mengi sana na wakuu naombeni msaada wenu.
 
Ulitumwa na nani!?,umewahi kuishi mwezi mmoja au miwili mfululizo na uliyemuoa kabla hamjaoana!?, Au mlikuwa mnaviziana mpewe baraka za kijinga na jamii?,

Tatizo la ndoa linaanzia pale mnapopanga kuoana kwa kuiridhisha jamii na mbwembwe nyingi. Ila ukiishi na mtu bila masharti na mikakati mingi ya ndoa au msukumo kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki mnaishi vizuri tu tena kwa muda usiojulikana.

Ila mkianza mipango ya ndoa ikawa mingi ndo tatizo linapoanzia. Miaka 27 ulikuwa unawahi nini!?.., kama unaishi kijijini ni sawa hata ukiwa na miaka 23 tu.

Ila kama ni msomi na upo town 27 unajitafutia matatizo. Muda sio mrefu utaanza kulaumu wazazi, ndugu na jamaa, baadae serikali mwisho kabisa utaanza kuilaumu CCM, nawaona humu kila lawama ni kwa CCM🤣
 
Hivi nyie wana mliokaa kwenye ndoa zaidi ya miaka kumi mmefanyeje aisee? Yaani sio poa wakuu yaani niko hoi bin taabani ndiyo kwanza ndoa yangu ina wiki mbili tu aisee najihisi kuchoka na kukata tamaa wakuu

Majukumu yamenizidi,nakosa uhuru wa kuamua mambo yangu eti lazima mshirikishane wote kwenye nyumba k.......m......m......k yaani hapa nipo hoi bin taabani fanyeni wana wajamii forum mninusuru mambo sio poa niko chupli chupli mambo yamekwama wakuuu

Ndiyo kwanza nina miaka 27 yaani naona mambo yamenielemea majukumu yanakuwa mengi sana na wakuu naombeni msaada wenu naenda kujichoma moto wakuu

Ukiona hivyo ujue ulioa kufuata mkumbo, hukujua lolote kuhusu ndoa unaishia kulalama na kutisha wenzio!!

Mpeleke mkeo kwa kaka yako kwanza ili ujipange upya!!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom