Kumbe kulinda penzi au ndoa ni kazi!

GITWA

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
1,489
1,687
Hebu wana JF tujadili hili,mnapoanza mapenzi kila mtu anakua na matarajio yake.maana hua ameumba picha ya aina ya mwenzi anaemuitaji akilini mwake.Na mnapoanza kujuana deep huku msha du ndo mnagundua sio aina ya mpenzi uliyekua nae mawazoni.Hapo ndo unakuja ugumu wa kulinda penzi.Je utafanyaje ili ulinde penzi au utajitoa kwenye mahusiano?
 
unalindaje penzi/ndoa kama umegundua mwenza uliyenae sie yule aliyeko mawazoni?

Halafu mpaka mmeoana ndo unagundua mwenzio sie? Mmmmmmmmmh ndoa za sikuhizi hizi mmmmmmmh
 
Umeona eeeh...mi nadhan kipind cha mwanzo tu cha urafiki wa karibu au u-bf na u-gf mtu unakuwa ushapata picha huyu mtu itakuwaje nae ndani ya nyumba balaa au shwari...yoyote anaegundua ana wrong partner ndan ya ndoa basi alikurupuka..
 
Ni kweli ulichosema lakini umesahau kua binadamu ni mabigwa wa usanii anaweza kuficha tabia yake halisi kwa mda wowote mpaka apate anachotaka.
 
Hapo sikuelewi GITWA. unamaana gani unaposema "huku msha du" Kama una maana kuoana, nina imani ulikuwa na muda wa kuchumbiana. Ilitakiwa uchunguze tabia zake zote huyo mkeo mtarajiwa. Kama amebadilika mmeshaoana inatakiwa utafiti ni nini chanzo cha mabadiliko. Kumbuka ndoa ni kama bidhaa nyingine dukani. Inatakiwa Ipendezeshwe ili inunuliwe, na mpendezeshaji mkuu wa ndoa ni neno la Mwenyezi Mungu. Kaeni katika neno na utamuona mwenzako ndie haswa chaguo la kweli.

Kama ulimaanisha kuvuana nguo na kutoridhika na nyeti zake na hamjafunga pingu za maisha, hiyo ni kazi yako kutafakari na kuchukua hatua.
 
Umenena vyema mtumishi wa Mungu
 
Kabla ya ndoa hakuna haja ya kulinda penzi la mtu ambaye unaona kabisa sio chaguo sahihi ni kuchukua hatua for your own good!
 
Kama ulimaanisha kuvuana nguo na kutoridhika na nyeti zake na hamjafunga pingu za maisha, hiyo ni kazi yako kutafakari na kuchukua hatua.

na kwa onja onja kama hii watu hawatakaa waridhike na wapenzi wao... mapenzi/ndoa ni zaidi ya kufunua na kufunika
 
Hapo sikuelewi GITWA. unamaana gani unaposema "huku msha du" Kama una maana kuoana, nina imani ulikuwa na muda wa kuchumbiana. Ilitakiwa uchunguze tabia zake zote huyo mkeo mtarajiwa. Kama amebadilika mmeshaoana inatakiwa utafiti ni nini chanzo cha mabadiliko. Kumbuka ndoa ni kama bidhaa nyingine dukani. Inatakiwa Ipendezeshwe ili inunuliwe, na mpendezeshaji mkuu wa ndoa ni neno la Mwenyezi Mungu. Kaeni katika neno na utamuona mwenzako ndie haswa chaguo la kweli.
Kama ulimaanisha kuvuana nguo na kutoridhika na nyeti zake na hamjafunga pingu za maisha, hiyo ni kazi yako kutafakari na kuchukua hatua.

Umenena vyema mtumishi wa Mungu
 
tatizo watu wenyewe usanii full kwa kwenda mbele....sasa inakuwa tabu sana kujua true adentity ya mtu kama haupo makini.
ila ukweli ni kwamba lazima ujue ni vigezo gani mke/mume unataka awe navyo then from there ndio unaanza kuangalia kama interested party anavyo...na pia ni vizuri kujua kuwa huwezi kuvipata vyote hivyo ni viti unaweza kusamee na kuishi bila tabu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom