Kuhani
JF-Expert Member
- Apr 2, 2008
- 2,944
- 64
... unajua tena kuna imani mbili hapa za mtaani...
1. Mtu ni UTU..
2. Mtu ni fedha!..
Kwa hiyo unaweza kujua kwa nini tuliukimbia Ujamaa.. Utu bila kitu mfukoni hutamaniki....
Swadakta. Ujamaa una utu, ubepari una fedha. Kama alivyosema Bubu AK kasema, kwamba kwenye ubepari kuna " kulipwa mshahara mkubwa."
Kwa hiyo yabidi mtu achague utu au fedha. Bubu nadhani amekimbilia kwa Mzee Brown (wadau wa Uingereza utawajua, wanapenda thread za Premier League). Sasa kama umechagua kukimbilia kwenye Ubepari utasemaje "kwa maoni yangu mazuri ya ujamaa ni mengi mno kuliko mazuri ya ubepari..." ?
Pointi yangu, Mkandara, ni kwamba unaweza kukosoa mfumo ambao unaishi ndani yake. Lakini kusema mfumo nilioukimbia ni bora kuliko mfumo nilioukimbilia ni kutaka kumtukana baniani mbaya wakati unajua utarudi kumuomba kiatu chake. Sorta like Mchungaji Mtikila na Rostam Aziz! Ndio maana nauliza ndugu zangu kama Bubu AK, kwamba mtu yeyote aliyekimbia the good 'ol socialist Tanzania kwenda "pasipo na utu" na "kwa makatili" wa kipebari, kilichowakimbiza kwa mabepari ni nini? Bubu AK anakwepa hilo swali.