Sesten Zakazaka
JF-Expert Member
- Sep 10, 2017
- 10,561
- 19,062
Huko porini wanapokutana katika makabiliano ya silaha kati ya askari wa wanyama pori na majangili wa nyara za serikali hua hakuna mateka. Ama afe/wafe askari au afe/wafe majangili. Hua ni vita kamili, kubwa, kali na yakikatili sana.
Nimefanya mazungumzo na watu mbalimbali ikiwemo wazee wenye uzoefu wa mambo ya porini na uwindaji na wanaeleza hadithi za kusisimua kama sio kutisha za maisha ya wawindaji hasa wawindaji haramu kwa jina maarufu majangili. Watu hawa ndio sababu ya kumalizika kwa wanyama wetu wakubwa kama vile tembo na faru licha ya ulinzi wa kila aina unaowekwa na mamlaka husika.
Kwa maelezo ya wengi ni kwamba majangili huwa ni walozi na washirikina sana na wanapoingia porini kuwinda tembo au faru au hata simba kiongozi wao wa msafara hua ni mtu mwenye utaalamu wa dawa za jadi maarufu kwa jina la "Fundi". Huyu ndio hutoa melekezo, miongozo na miiko ya uindaji kabda, wakati na baada ya safari.
Inasemekana porini kumejaa miujiza na mauzauza ikiwemo wanyama wakubwa wenyewe kama tembo, faru, simba n.k ni kama vile wanavitu sio vya kawaida ambapo bila kugangwa mwindaji hawezi dumu porini hata kwa muda mchache kwani atararuriwa na kuliwa na wanyama wakali.
Wanasema mnyama kama tembo anahisia kali sana za kuweza kumtambua mtu aliyekwenda kwa ajili ya kumdhuru na akikuwahi anakumaliza. Aidha iwapo utamuua mnyama huyo bila kupatiwa zindiko maalum waweza kutwa na mauzauza na mikosi mingi maishani mwako! Kwa maana hiyo hugangwa kuanzia mtu na vifaa vyote vya uwindaji kama mishale na bunduki.
Tena wawindaji baada ya zindiko huingia sehemu yoyote yenye wanyama wanaowawinda na kuwachagua wawatakao bila wanyama kuwaona au majangili kuonekana na askari wa wanyama pori! Kama ni kundi la tembo jangili atekwenda mpaka kwenye kundi la tembo na atakua anamchagua wa kumpiga kwa kumshika na wanyama hao hutulia tu.
Kwa maelezo niliyoyakusanya ni mara chache sana askari wa wanyama pori wakawaona majangili japo wakati mwingine huwa wametenganishwa na umbali mdogo sana wa hata mita ishirini tu! Inasemekana hii ndio sababu kubwa wanyama wetu wanaendelea kupungua kwa kuuwawa licha ya juhudi kubwa na rasilimali nyingi zinazotumika katika ulinzi wao.
Naomba kupewa darasa na uzoefu kutoka wakongwe wa tasnia hii kama Mshana Jr na wengineo kwamba kwa uzoefu wao hili jambo lina asilimia yoyote ya ukweli Na kama ni hivyo askari wetu nao waanze kutafuta "mafundi" wawagange ili waweze kutimiza vyema majukumu yao ya kupambana na majangili na kuokoa tembo wetu wanaotoweka kwa kasi ya ajabu?