Kulinda Haki na Rasilimali za Taifa, Hata Kama Katiba ni Mbovu, Logic Itumike

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,547
41,060
Katiba yetu ya sasa, ni mbovu sana, na kwa kweli anayeshabikia kuwa hii katiba ya sasa iendelee, ni mnafiki, na adui mkubwa wa Taifa letu. Na anayechelewesha kupatikana kwa katiba mpya, ni shetani anayestahili kupigwa vuta kwa nguvu zote.

Katiba yetu, jambo la kwanza la msingi ni lazima itoe ulinzi wa raia na rasilimali za nchi, ilinde haki za raia na misingi ya demokrasia na uongozi bora.

Kwa mfano, tunajua kuwa kuna mambo tu machache ambayo ni ya Mwungano, lakini yapo mengi ambayo siyo ya Mwungano. Katiba ni vema ibainishe wazi ili mipaka ya mwungano wetu iwe bayana. Itamke kuwa mambo fulani kila upande unajitegemea na iwe marufuku upande mmoja kufanya maamuzi kwa mambo yasiyokuwa ya mwungano. Mathalani, itamke wazi kuwa ili mtu aweze kuteuliwa kwenye nafasi yoyote ile kwenye wuzara au taasisi isiyokuwa ya Mwungano ambayo ni ya Tanzania bara, lazima mhusika awe na uraia mmoja tu, uraia wa Tanzania.

Tujiulize, mathalani Bunge linapojadili bajeti ya Wizara ya fedha, Serikali za mitaa, utamaduni na michezo, Madini, Ujenzi, Nishati au Afya, mbunge wa Zanzibar anakuwepo Bungeni anafanya nini? Wabunge wa Zanzibar haki yao ya kushiriki Bunge ilistahili kuishia kwenye Wizara za Mwungano tu. Hili naamini ni jambo lililohitaji tu logic.

Tujiulize, hivi imekuwaje leo hii, Wizara ya Ujenzi na uchukuzi isiyo ya Mwungano, imewezekana vipi Waziri wake na Katibu wake wote wawe wa kutoka Zanzibar?

Rais Kikwete aliwahi kutamka wazi kuwa Zanzibar ni nchi tukiwa hapa nchini, lakini siyo nchi tukitoka nje ya Tanzania. Na alieleweka. Nje ya Tanzania, Zanzibar siyo nchi kwa sababu tunawakilishwa na Wizara moja ya Mwungano, wizara ya mambo ya nchi za nje.

Lakini kwa hapa ndani, Zanzibar ni nchi. Ina katiba yake, ina mipaka yake, ina wimbo wake wa Taifa, ina mahakama yake, na ina raia wake ambao wanaitwa Wazanzibari. Na hawa Wazanzibari, haki zao za kikatiba zimeirodheshwa kwenye katiba yao.

Kwa hiyo mzanzibari ana uraia pacha. Ana uraia wa Zanzibar, na uraia wa pili ni wa Tanzania. Kwa haki yake ya uraia wa Zanzibar, ana haki ya kugombea au kuteuliwa nafasi yoyote ya uongozi Zanzibar. Na kwa uraia wake wa pili wa Tanzania ana haki ya kuteuliwa kwenye nafasi yoyote ile kwenye masuala yale ya Mwungano. Sasa Mbarawa na katibu wake amewezaje kuwa kwenye nafasi za juu kabisa kwenye Wizara isiyo ya Muungano wakati yeye ni Mzanzibari?

Bandari zetu kama zitachukuliwa kwa kupitia mikataba hii ya kiinimacho, machozi ya Watanganyika yatakuwa kwa Wazanzibari maana ndio waliowezesha hilo kutokea.

Ni muhimu sana kwa sasa, mambo yote yasiyo ya kimwungano, maamuzi yake yafanywe na wananchi wa sehemu husika.

Kama Watanganyika hawana uwezo wa kuamua chochote kisicho cha muungano kwa Zanzibar, vivyo hivyo iwe kwa Wazanzibari kwa mambo ya Tanganyika.

Ucheleweshaji wa katiba mpya, katiba ambayo ingeyaweka mambo haya bayana, unaweza kuliangamiza Taifa, hasa upande wa Tanganyika, na mbeleni ikaja kuleta uhasama mkubwa baina ya pande mbili za Mwungano.

Hili ni angalizo.

Tuseme wote, BANDARI YETU ITAENDELEA KUWA YETU, NI URITHI WA WATU WETU.
 
Kuna mama mmoja anawadanganya watanzania 'eti watanzania hawathakiiii katibaaaaa wanataka maji foolish kabisa.Tungekuwa na katiba Bora hakuna MKATABA wa kihuniiiii ungepita.
 
Umeandika vizuri sana. Kuna hoja umeziweka zinapaswa kuibua mjadala ya kitaifa ili kuwe na muafaka mzuri
 
Katika uhalisia muungano wetu una walakini mkubwa hasa wa kimuundo na kiutendaji kwenye mifumo ya kiutawala. Kuna mipaka inayoacha alama nyingi za kuuliza. Na kwa bahati mbaya katiba yetu inatekelezwa kiubabaishaji sana kuhusu suala hili la muungano. Kuna upendeleo wa wazi wanapewa wazanzibari, sijui ni ili wasiuvunje muungano, na waendelee kubaki hivyo hivyo kwa shingo upande ama nini. Kinachoendelea kwa sasa hasa kwenye hili sakata la bandari kumeweka kwa uwazi madhaifu hayo ya muungano wetu.

Tunapotaka katiba mpya, lengo hasa ni kuondoa hii sintofahamu. Lakini cha ajabu linapokuja suala la maboresho ya muungano, ccm wanahodhi hilo suala zima, na kubaki na porojo za kumaliza kero za muungano, lakini hizo porojo hazijawahi kukata kiu ya wananchi wa pande zote mbili kuhusu kero za muungano. Huenda sakata hili la bandari likasaidia kuweka sawa kuhusu hatari ya huu muungano wa shuruti.
 
mbowe kapandikiza watu tabia za kichaga kung'ang'ania mashamba bila kuyaendeleza
Punguza utoto dogo kwenye nyuzi za heshima. Subiri huu utoto wako uupeleke kwenye nyuzi za wajinga wenzio. Hapa ndio unaona umeweza kupoteza watu kwenye hoja ya msingi.
 
ccm kumbuka tanganyika mnakoipeleka inakuja kuwa chini ya chama kitakuja kuwa chini ya nzanzibar na ccm itakufa.
pili mapinduzi mliyofanya nzanzibar yatakuja kutokea na huyu mama atakimbia nchi
 
Ukishakuwa na namba moja dhaifu hakuna kitakachoendelea cha maana na kibaya ni kwamba ukimkosoa utatafutwa chini kwa chini uje uache familia ikilia tu bila majibu
 
Tamaa na ulafi uliopitiliza ndio shida kubwa, sio kwamba wanaofanya maamuzi hayo hawawezi kufanya logical reasoning ama kutojua athari za maamuzi wanaofanya..
 
Back
Top Bottom