Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,555
- 41,066
Kila mtu anajua kabisa kuwa hawa waliopo Bungeni, ni wahalifu, hawakuchaguliwa na wapiga kura. Je, ni halali wahalifu wa kupora haki za wananchi za kuwachagua wawakilishi wao kupitia boksi la kura, kufanya maamuzi juu ya rasilimali za Taifa?
Mwizi haachi asili yake. Hawa waliopo bungeni ni majizi ya haki za wananchi. Mtu mwizi tangu lini akafanya maamuzi ya kuzuia mali zisiibiwe. Mwizi anachotafuta ni faida binafsi. Na ndiyo maana tunasikia kuwa baadhi ya wabunge wamehongwa dola 50,000 na magari ya kifahari kuruhusu rasilimali ya Taifa kuibiwa. Hawana uchungu wowote kwa sababu asili yao ni kuiba, wamemsaidia mwizi mwenzao, na kama tuhuma hizo za hongo ni kweli, basi huyo mporaji amekwishawapa mgao wao in advance. Tulioibiwa mali yetu ni sisi wananchi tuliobakia na simanzi.
Wale mawakala wa wevi, wasitupotoshe. Ukweli kuhusiana na uporaji wa bandari ni kwamba:
1. MoU ilisainiwa na mkurugenzi wa bandari, ambaye ni mzanzibari, February 2022.
2. Mkataba ulisainiwa na waziri, ambaye ni mzanzibari, October 2022.
3. Utekelezaji wa mkataba ulianza miezi 3 tangu kusainiwa.
4. Kilichojadiliwa bungeni siyo MoU bali ni mkataba ambao tayari umekwishaanza kutekelezwa.
5. Mkataba uliosainiwa na Waziri baada ya kuridhiwa na Rais ni wa milele, hauna kikomo, wajibu wa Serikali ni kuhakikisha mwekezaji habughudhiwi na Serikali inashirikiana na mwekezaji kutengeneza mfumo wa ulinzi.
6. Siku 1 kabla ya Bunge kuridhia, wabunge hawa waovu walikaa kama kamati ya chama na kuelekezwa kuwa ni lazima waridhie mkataba kwa sababu utekelezaji wa mkataba umekwishaanza.
7. Wabunge waovu, hawakujali maslahi ya Tanganyika, wakaungana na Rais Mzanzibari, Waziri Mzanzibari, Katibu wa Wizara Mzanzibari na mkurugenzi wa Bandari Mzanzibari, kuuza bandari za Tanganyika.
Tafsiri ya Kilichoidhinishwa:
Waarabu watamiliki maeneo yote ya kuzunguka bandari na bandari yenyewe kwa muda usio na kikomo. Maana yake ni kwamba maeneo haya wamepewa waarabu kuwa ya kwao moja kwa moja, japo lugha iliyotumika siyo hiyo.
Ukweli kuhusu DP World:
1. Ni kampuni ya kimataifa katika uendeshaji shughuli za bandari.
2. Hakuna nchi yoyote iliyowahi kuipa Dp mkataba wa zaidi ya miaka 30. Maeneo mengi ina mkataba wa miaka 20.
3. Kuna baadhi ya nchi zilifuta mkataba na DP World baada ya kuthibitika DP kuwahonga wafanya maamuzi kwa upande wa Serikali ili wapitishe vipengere vya hovyo kwenye mkataba (kama ilivyofanyika hapa kwetu, kwa tetesi zilizopo).
4. Karibu kwenye nchi zote DP haijapewa kuendesha bandari Mama, bali bandari nyinginezo, sababu kubwa ni kuzui DP kuhatarisha usalama wa nchi. Maana ikitokea mgogoro kati ya mwendeshaji na nchi, na kusababisha shughuli za bandari kusimama, itasababisha economic crisis kwa nchi.
Kilichotakiwa:
1. DP haikustahili kupewa mkataba wa kuendesha bandari mama ya Dar, ingeanza na bandari ndogo kama vile ya Zanzibar au Mtwara. Zanzibar, ingekuwa ni mahali sahihi zaidi kwani Wazanzibari wameonekana kuwa ndiyo mainjinia wa kuitafuta hiyo DP. Ufanisi wa huko Zanzibar, ndio ungeiwezesha DP kupewa bandari nyingine au kufukuzwa, kama yalivyofanya baadhi ya mataifa.
2. Kwa kampuni yenye makandokando mengi kama hii, ilistahili kupewa mkataba wa miaka 10 tu kwenye bandari ya mwanzo ili kupima maadili na ufanisi wake.
SINTOFAHAMU:
Swali muhimu:
1. Hawa wabunge wevi wa haki za wananchi za kuwapata wawakilishi wao, ambao wameendeleza uovu wao kama vile tuhuma za rushwa dhidi yao zilivyo, wakatuingiza kwenye mkataba fedhuli, tuwafanye nini? Bado kuna mwaka mzima umebakia kabla ya uchaguzi, hapa katikati, si wanaweza kuendeleza uovu wao kwa kuuza mali nyingine za nchi?
2. Makamu wa pili wa Zanzibar ametamka wazi kuwa suala la bandari siyo la Mwungano, sasa imekuwaje Rais Samia amweke Mzanzibari kuwa waziri kwenye wizara isiyo ya mwungano? Imekuwaje Rais Samia amweke katibu mkuu mzanzibari kwenye Wizara isiyo ya mwungano? Ilikuwaje Rais Samia amweke mkurugenzi mkuu wa bandari mzanzibari? Je, hatuoni kuwa hii ni syndicate ambayo maandalizi yalianza muda mrefu kwa lengo hili chafu la kuipora rasilimali hii muhimu ya Tanganyika na kuigawa kwa Mwarabu? Hivi tunaweza kuamini kuwa hakukuwahi kuwa na watanganyika wenye uwezo wa kuisimamia bandari, na wizara nzima hii isiyo ya mwungano, mpaka tukakope watu kutoka Zanzibar?
Wazee wetu, bila ya bunduki, mizinga wala guruneti, walipambana na mwarabu, mjerumani na mwingereza, waliokuwa na kila aina silaha, kuetetea rasilimali na mamlaka yao. Japo ni kwa sadaka kubwa, ikiwa ni pamoja na maisha yao, mwishoni walishinda, ndiyo maana mpaka leo na sisi tunajiita ni Taifa. Huu ni urithi wa sadaka walizotoa mababu zetu. Sisi tunaacha nini kwa vizazi vijavyo kama hata vile walivyovipigania na kuvilinda babu zetu, leo tunavitoa wenyewe kwa mikataba ya hovyo kiasi hiki? Na hawa vibaraka wanaobariki mikataba hii ya hovyo, adhabu yao iwafaayo ni ipi?
Wawekezaji tunawakaribisha na wanahitajika, lakini mpangaji ni lazima ajulikane ni mpangaji, na mwenye mali lazima ajulikane kuwa ndiye. Siyo mpangaji apore au ampangie mwenye mali.
Mkataba huu wa kijuha, kamwe haukubaliki. Ule mfumo wa hovyo wa watawala kuwapangia wenye nchi namna ya kuwatawala wenye nchi, unamfanya Rais kufanya chochote apendacho na alichoamua, pamoja na kugawa hovyo rasilimali za nchi.
KATIBA ni lazima ipatikane. Kama watawala wanashupaza shingo kwa kuzuia upatikanaji wa katiba kwa hadaa nyingi mbalimbali, wajue kuna siku watafukuzwa na kuondolewa nje ya mfumo wa kikatiba. Kuna siku wananchi watachoka, na hapo ndipo watajutia kwa kuifanya nchi kutokuwa na katiba inayokubalika.