kulikua na ulazima wa kumteua mwandosya?

KIM KARDASH

JF-Expert Member
Sep 21, 2011
5,139
1,139
Hivi kulikua na sababu yeyote ya msingi jk kumteua mzee mwandosya kuwa waziri wakati ni wazi kabisa inaonyesha hali yake kiafya bado haijatengemaa sawasawa??

Je watanzania tutegemee mchango gani kutoka kwa mzee wetu huyu mtaalam aliyebobea kwenye masuala mazima ya mazingira ambae dunia imekua ikimtumia kwenye masuala hayo kipindi alipokua na afya nzuri?

Pichani chini:Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na Waziri asie na Wizara Maalum Profesa Mark Mwandosya wakati alipomtembelea nyumbani kwake, Kunduchi jijini Dar es salaam kumjulia hali May 7, 2012.

IMG_0348xx.JPG

JK awahitaji kina MWA la sivyo wataenda Chadema kama wimbi lilivyo sasa.
mtandao wa Mwa ni kubwa mno kulipoteza.
 
Kuugua sio kwamba hatapona. Huyu ndo nguzo ya ccm ktk mkoa wa mbeya. Kuto mjumuisha katika baraza la mawaziri lingekuwa pigo kwa ccm katika mikoa ya ukanda huo. Hajapewa wizara specific kwani bado hajawa fit ki afya ila lazima jina lake liwemo kwenye baraza kwa manufaa ya ccm.
 
Kwa hiyo unataka kubagua wagonjwa? Mbona anaweza kuperform kabisa huyo.
 
linganisha na kazi alizolifanyia taifa hata kabla ya kupata uwaziri kisha utajua kwamba Jk alikuwa sahihi kumpa wizara hiyo.

Usifikiri Rais anatoa fursa hiyo kwa kila kiongozi ni fursa idimu kupewa na nadra sana kukutana nayo ni viongozi wangapi wamepishana na fursa hii.
 
Mwandosya amejitahidi sana kupishana na orodha ya mafisadi ya Chadema ni dalili njema kwa kiongozi kushinda tuhuma za wapinzani.
 
Hivi kulikua na sababu yeyote ya msingi jk kumteua mzee mwandosya kuwa waziri wakati ni wazi kabisa inaonyesha hali yake kiafya bado haijatengemaa sawasawa??

Je watanzania tutegemee mchango gani kutoka kwa mzee wetu huyu mtaalam aliyebobea kwenye masuala mazima ya mazingira ambae dunia imekua ikimtumia kwenye masuala hayo kipindi alipokua na afya nzuri?

Pichani chini:Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na Waziri asie na Wizara Maalum Profesa Mark Mwandosya wakati alipomtembelea nyumbani kwake, Kunduchi jijini Dar es salaam kumjulia hali May 7, 2012.

IMG_0348xx.JPG

Halafu tunasema Tanzania ni nchi masikini ambayo haina umeme wa uhakika, haiwezi kuwalipa madaktari vizuri na haiwezi kuwalipa walimu lakini inaweza kumpa mtu uwaziri bila yule mtu kufanya kazi yeyote. Watanzania ni wa pole sana!!!
 
linganisha na kazi alizolifanyia taifa hata kabla ya kupata uwaziri kisha utajua kwamba Jk alikuwa sahihi kumpa wizara hiyo.

Usifikiri Rais anatoa fursa hiyo kwa kila kiongozi ni fursa idimu kupewa na nadra sana kukutana nayo ni viongozi wangapi wamepishana na fursa hii.

Kweli mkuu, JK yuko makini sana ndio maana hadi kina VIck Kamata, Betty Mkwasa wanapata nyazifa...
 
Kwa kweli mwandosya amechoka, hiyo "sumu" waliyompa ni kiboko...
 
Kuugua sio kwamba hatapona. Huyu ndo nguzo ya ccm ktk mkoa wa mbeya. Kuto mjumuisha katika baraza la mawaziri lingekuwa pigo kwa ccm katika mikoa ya ukanda huo. Hajapewa wizara specific kwani bado hajawa fit ki afya ila lazima jina lake liwemo kwenye baraza kwa manufaa ya ccm.

Lakini tunaomlipa ni sisi walipa kodi
 
ni bora hata Rais kumtetea na kumueka mwandosya kuliko alivokua anawatetea akina ngeleja na majambazi wenzie...
 
linganisha na kazi alizolifanyia taifa hata kabla ya kupata uwaziri kisha utajua kwamba Jk alikuwa sahihi kumpa wizara hiyo.

Usifikiri Rais anatoa fursa hiyo kwa kila kiongozi ni fursa idimu kupewa na nadra sana kukutana nayo ni viongozi wangapi wamepishana na fursa hii.

wewe acha ushabiki,jk hana cha kupoteza mleta mada kama humjamuelewa lengo lake ni kuonyesha matumizi mabaya ya serikali,mwandosya kwa kuteuliwa tu ataliowa mshahara na malupu lupu kama mawaziri wengine,sasa kwanini tumlipe mgonjwa mapesa hayo?kwanini tusimlipie matibabu tu then yeye abaki nyumbani ashughulike na afya yake kwanza mpaka itakapoengemaa?kulikua na haraka gani ya kumchagua kabisa?
 
Jk hana huruma na fedha za walipa kodi,na ndiyo sababu anazifuja atakavyo.
 
wewe acha ushabiki,jk hana cha kupoteza mleta mada kama humjamuelewa lengo lake ni kuonyesha matumizi mabaya ya serikali,mwandosya kwa kuteuliwa tu ataliowa mshahara na malupu lupu kama mawaziri wengine,sasa kwanini tumlipe mgonjwa mapesa hayo?kwanini tusimlipie matibabu tu then yeye abaki nyumbani ashughulike na afya yake kwanza mpaka itakapoengemaa?kulikua na haraka gani ya kumchagua kabisa?

Elimu ni nzuri sana, ukikosa elimu unakuwa kama mtumwa wa milele. Hivi katika mawazo yako unafikiri Rais anateua watumishi au Mawaziri ili kukuridhisha wewe na familia yako? Tambua kuwa kabla ya Ujeuzi Rais anashauriana na jopo la watu wenye heshima sana na Elimu ya kutosha na kupata ushauri wa kina.

Rais hawezi kukusikiliza wewe unayefikiria wajomba zako na binamu zako ndiyo wateuliwe. Nchi huendeshwa kwa umakini sana na ndivyo Rais anafanya, sio kusikiliza mawazo potofu kama yako.

Prof. Mwandosya ni mtu muhimu sana katika nchi hii, duniani na Chama cha Mapinduzi, hivyo lazima Serikali iendelee kumtumia kwa faida ya Watanzania wote na siyo kwa faida ya Wajomba zako.

Tatizo lako hujui hata mahusiano mema kazini, ukimwajiri Housegirl nyumbani kwako, alafu ghafya huyo binti akaanza kuumwa, usifikilie kumfukuza kazi kwa vile tu hawezi kukupikia kande kwa wakati huo na huku ukiwaza gharama za kumtibu. Kwanza fikiria kumtibu ili arudi katika hali yake ya kawaida alafu endelea kumtumia.

Ingekuwa nchi hii inaendeshwa na wajinga kama nyinyi pangechimbika kwani immediately ukisikia Waziri, Katibu, Mhasibu, Tarishi, Mfagizi wa choo katika Ofisi za Serikali anaumwa wewe ungekuwa ni kuulizia faili lake ili kumsimamisha kazi mpaka atakapopona au akichelewa kupona unamfukuza kazi.

Big up JK, Prof. Mwandosya nchi hii bado inamwitaji usisikilize hawa walevi.
 
Back
Top Bottom