Kulikoni mkuu mpya wa Mkoa wa Shinyanga kuhamishwa mapema hivi?

kwa hapa ndo mh dk jk ananiacha hoi,amekaa takriban mwaka tka aanze awam ya pili,hv kama kwl kwa mda huo wote alishindwa kujua hyu aende wapi yule wapi??hv si watalipwa hela ya transfer??inauma sana tena sana,na mungu yupo anatuona wote ss wanyonge na mackin

Mkuu wa mkoa lindi aliishakaribishwa na sherehe kubwa ilifanyika oceanic hotel na millions were spent kwa ajili ya kumkaribisha tu. Aliishaenda na kukutana na watendaji kwenye wilaya na kutembelea projects chache. Sasa hivi watu ofisini kwa Ras wanalalamika kuhusu matumizi makubwa mapya yanayowasubiri hali hamna fungu lake. Hii ndo nchi ya Kikwete! Sometimes huwa najiuliza sisi watz ndio kiongozi wetu tuliyemchagua atuongoze kizembe hivi? Kweli hatuna akili.
 
Huyo mh. Mwananzila alikuwepo Shy wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya uhuru pale kwenye viwanja vya Shycom.Mimi nilikuwepo na nilipata nafasi ya kupeana nae mikono, kwa hiyo nina uhakika alikuwepo Shinyanga. Kahamishwa lini tena?
Au kuna kitu kavurunda tena?
 
Tanzania Tanzania nakulilia, Yaani mkuu wa kaya kawapanga wanae kwenye vyumba kumbe kakosea kawageuza tena kabla hata hakujakucha!!!!!! Mkwe le na team yake ta TISS ni wababaishaji
 
JK na uteuzi wake wa kufikirika anaweza siku moja kumteua hata mtu aliyekwisha KUFARIKI katika nafasi na kuja kushtuka wakati wa kumuapisha.Rahisi asiyekuwa makini ni mzigo kwa Taifa kama Umasikini,maradhi na ujinga.
 
Wakiongozwa na Mganga njaa wa habari SALVA RWEYEMAMU

Haya ni yale yale ya Mkurugenzi wa wilaya na Ngorongoro kuitwa ili akabidhiwe gari la wagonjwa la Longido. Ikulu imejaa watu wanaofikiri kama wauza vitumbua wa Kinondoni Mosco
 
wanajf naomba kufahamishwa kidogo kama kuna mtu anafahamu; hivi mkuu wa mkoa wa shinyanga aliyeteuliwa hivi karibuni anaitwa nani?

kumbe jibu unalo unataka kutuingiza chaka??tule makasa
hilo ndiojibu sahihi
 
RCs.JPG


Elimu%2Bni%2Bmacho.JPG


Shule ya kijijini kwake huyu Ludo hiyo hapo juu.


Wednesday, 4 August 2010


WAZITO WALIO ANGUSHWA KURA ZA MAONI CCM


Mpenzi mdau wa maarifa blog, tunapenda kukujulisha kuwa kama ulikuwa hujawafahamu 'wazito' waliongushwa katika kura za maoni CCM ni kama walivyo orodheshwa hapa chini, kama unamfahamu mwingine zaidi basi usisite kutuhabarisha ili tuongeze kwenye orodha yetu!


1. John Malecela (Mtera)


2. Joseph Mungai (Mufindi Kaskazini)

3. Raphael Mwalyosi (Ludewa)

4. Jackson Makweta (Njombe Kaskazini)

5. Monica Mbega (Iringa Mjini)

6. Yono Kevela (Njombe Magharibi)

7. Felix Mrema (Arusha Mjini)

8. Prof Philemon Sarungi (Rorya)

9. Dk James Wanyancha (Serengeti)

10. Ramadhan Maneno (Chalinze)

11. John Shibuda (Maswa)

12. Bujiku Sakila (Kwimba)

13. Mudhihir Mudhihir (Mchinga)

14. Tatu Ntimizi (Igalula)

15. Said Nkumba (Sikonge)

16. Siraju Kaboyonga (Tabora Mjini)

17. James Nsekela (Tabora Kaskazini)

18. Jackob Shibiliti (Misungwi)

19. Joel Bendera (Korogwe Mjini)

20. Samuel Chitalilo (Buchosa)

21. James Musalika (Nyang'hwale)

22. Ernest Mabina (Geita)

23. Charles Mlingwa (Shinyanga Mjini)

24. Kilontsi Mporogomyi (Kasulu Magharibi)

25. Manju Msambya (Kigoma Kusini)

26. Juma Ngasongwa (Ulanga Magharibi)

27. Suleiman Sadiq Murad (Mvomero)

28. Mwichoum Msomi (Kigamboni)

29. Felix Kijiko (Muhambwe)

30. Ruth Msafiri (Muleba Kaskazini)

31. Pascal Degera (Kondoa Kusini)

32. Zainab Gama (Kibaha Mjini)

33. Prof Idriss Mtulia (Kibiti)

34. Ibrahim Msabaha (Kibaha Vijijini)

35. Joseph Mungai (Mufindi Kaskazini)

36. Benito Malangalila (Mufindi Kusini)

37. Esterina Kilasi (Mbarali)

38. Guido Sigonda (Songwe)

39. Nazir Karamagi (Bukoba Vijijini)

40. Mgana Msindai (Iramba Mashariki)

41. Ludovick Mwananzila (Kalambo)

42. Clemence Lyamba (Mikumi)

43. Damas Paschal Nakei ( Babati Vijijni)

44. Charles Kajege (Mwibara)

45. Bakari Mwapachu (Tanga Mjini)

46. Diodorus Kamala (Nkenge)

47. Suleiman Kumchaya (Lulindi)

48. Wilson Masilingi (Muleba Kusini)

49. Shamsa Mwangunga (Ubungo)

50. Raphael Chegeni (Busega)

51. Juma Kilimbah (Iramba Mashariki)

52. Aloyce Kimaro (Vunjo)

53. Mohamed Sinani (Mtwara Vijijini)

54. Raynald Mrope (Masasi)

55. Freethan Banyikwa (Ngara)

56. Ponsian Nyami (Nkasi)

57. Elisa Mollel (Arumeru Magharibi)

58. Dunstan Mkapa (Nanyumbu)

59.Mwantumu Mahiza (Mkinga)

60. Mhandisi Laws Mhina (Korogwe Vijijini)

61. Mohamed Rished (Pangani)

SOURCE: MAARIFA BLOG: WAZITO WALIO ANGUSHWA KURA ZA MAONI CCM


HOJA YANGU:

Hao waheshimiwa wa CCM waliopigwa chini kwenye mchujo wa chama chao hapo mwaka jana, ndio tuseme;

1. Ni nani kati yao ambaye yuko wapi hivi sasa na anafanya nini?

2. Yupi aliyeshindwa kihalali na yupi kwa mizengwe?

3. Ni wangapi kati yao katulizwa na ofisi tunazolipia kupitia kodi zetu na kuna ustahili gani MAKAPI WA KISIASA kupata uteuzi wa kiserikali?

Nawashilisha hoja.
 
Hapana, si bure huyu bwana kaibiwa tu password yake wala si yule Mwita25 tindikali ya Igunga yule.

This tips off how rudderless JK government is.

The man seems to have been crapulous or under the weather when he announced the appointments! Needless to say, previous experience has proved that life can be possible even in the absence of Regional Commissioners.
 
Hakika mkuu Najua aliteuliwa Mwananzila ila Mwananzila si mkuu tena wa mkoa wa Shinyanga. Nilikuwa na maana ya kuileta hii habari kinyumenyume ili tuijadili baada ya kujiuliza kwa makini. Sikutegemea mtu ategemee mtu kama mimi nisiwe najua uteuzi uliofanyika na ulivyofanyika. Sikutegemea mtu aniambie nika google as if I am a layman and not a gteat thinker. Hapa dhima yangu ilikuwa kutaka kujua kama wanaJF wenzangu wanajua kuwa kumetokea kubadilishana vituo kwa wakuu hao wa mikoa.[/
 
Mkuu wa mkoa lindi aliishakaribishwa na sherehe kubwa ilifanyika oceanic hotel na millions were spent kwa ajili ya kumkaribisha tu. Aliishaenda na kukutana na watendaji kwenye wilaya na kutembelea projects chache. Sasa hivi watu ofisini kwa Ras wanalalamika kuhusu matumizi makubwa mapya yanayowasubiri hali hamna fungu lake. Hii ndo nchi ya Kikwete! Sometimes huwa najiuliza sisi watz ndio kiongozi wetu tuliyemchagua atuongoze kizembe hivi? Kweli hatuna akili.

Nyie msokuwa na akili wakati wa kuchagua ndio mliotuponza!
 
Takribani mwezi mmoja baada ya Rais Jakaya Kikwete kuteua wakuu wa mikoa wapya, akiwamo Ludovick Mwananzila, aliyeteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, sasa amehamishiwa mkoa wa Lindi.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Ally Nassoro Rufunga, amehamishiwa Mkoa wa Shinyanga.
Rais Kikwete aliwateua wakuu wapya wa mikoa Septemba 14, mwaka huu na kuwaapisha Septemba 16, mwaka huu Ikulu jijini Dar es Salaam.
Msemaji wa Ofisi wa Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), Khalist Luanda, alithibitisha uhamisho wa wakuu hao wa mikoa.

ADAIWA KUKATALIWA SHINYANGA
Habari kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, zinaeleza kuwa uhamisho huo unadaiwa kufanyika, baada ya wananchi wa Mkoa wa Shinyanga, hasa wafugaji kutomkubali Mwananzila.
Mwananzila anadaiwa kuwanyanyasa wafugaji wa Kisukuma alipokuwa mbunge, mkoani Rukwa mwaka 2005-2010.

Habari zinasema kuwa Mwananzila na Rufunga walikuwa katika makabidhiano ya ofisi yaliyofanyika katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa Shinyanga jana.
Makabidhiano hayo yalishuhudiwa na wakuu wa wilaya, wakurugenzi wa halmashauri, viongozi mbalimbali wa serikali, vyama vya siasa, vyombo vya ulinzi na usalama na waandishi wa habari wa Mkoa wa Shinyanga.

Habari zaidi kutoka ofisi hiyo zilizothibitishwa na baadhi ya maofisa waandamizi, zinaeleza kuwa uhamisho huo uliofanyika kimyakimya, unatokana na Mwananzila kuwa mstari wa mbele kusimamia uhamishaji wa wafugaji wa kabila la Kisukuma mkoani Rukwa.
Mwananzila anadaiwa kutekeleza suala hilo katika zoezi la kuwaondoa wafugaji mwaka 2008 hadi mwanzoni mwa mwaka 2009) akiwa Mbunge wa Jimbo la Kalambo, mkoani Rukwa.

“Unajua Mwananzila akiwa mbunge wa jimbo la Kalambo, mkoani Rukwa, alisimamia kidete kuwaondoa wafugaji wa kabila la Kisukuma waliohamia Sumbawanga kwa madai kuwa wanaharibu mazingira,” alisema ofisa Mwandamizi wa serikali, ambaye hakupenda jina lake liandikwe gazetini. Aliongeza: “Katika zoezi hilo, wengi wao waliteswa walinyang’anywa mifugo yao na kuchomewa nyumba zao hasa katika Kata ya Matai na Sopa.”

Kwa mujibu wa habari hizo, baada ya Mwananzila kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, wafugaji wengi kutoka katika wilaya za Maswa, Kishapu, Bariadi, Shinyanga Vijijini na Meatu walipinga uteuzi wake.
Walipinga uteuzi wake kwa madai kwamba, hakustahili kuwaongoza kwa vile alisababisha mateso, manyanyaso na dhuluma dhidi yao.
“Mara baada ya Rais Kikwete kumteua Mwananzila kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, wafugaji wengi kutoka katika wilaya za mkoa huo, walipinga vikali,” alisema ofisa mwingine mwandamizi kutoka ofisi ya mkuu wa mkoa.

Aliongeza: “Walimtuhumu kuwa mwaka 2008 huko Sumbawanga, ndiye aliyeongoza mateso, manyanyaso na dhuluma dhidi yao pamoja na watumishi wa serikali, wakiwamo askari polisi, usalama wa taifa na watendaji wa kata na vijiji.”

Wakizungumzia uhamisho huo, baadhi ya wananchi wa mkoa huo walisema Rais Kikwete hakupaswa kumhamisha mkuu huyo wa mkoa, bali alipaswa kusitisha uteuzi wake kutokana na kuongoza mateso dhidi ya wafugaji wa kabila la Kisukuma waliohamia mkoani Rukwa.
“Rais Kikwete hakupaswa kumhamisha RC Mwanazila. Angesitisha uteuzi wake. Kwani mateso tuliyoyapata kipindi kile na hata wengine kupoteza maisha na mali zao, ni vitendo vya kusikitisha. Havikupaswa kufanywa na kiongozi kwa Watanzania wenzake,” alisema Luzerenga Lufuta.
Aliongeza: “Mimi ni miongoni mwa waathirika katika zoezi hilo. Nilikuwa maeneo ya Matai. Nimepoteza mifugo yangu zaidi ya ng’ombe 2,000. Hata ushahidi wa mkanda wa video ninao. Na huyo Mwananzila alikuwa Mbunge. Ndiye alisimamia kidete suala hili.”

Walisema asingeweza kuongoza mkoa huo, kwani walio wengi mara baada ya uteuzi wake, walikumbushwa machungu waliyoyapata na wengi wao walikuwa wakisimuliwa jinsi walivyokuwa wakinyang’anywa mifugo yao na kuuzwa kwa bei ya chini ili walipie faini serikalini na kuachwa maskini hadi sasa.
“Asingeweza kuongoza mkoa huu, kwani uteuzi wake ulitukumbusha machungu mengi. Wengi tulinyang’anywa mifugo na kuuzwa kwa bei ya chini na viongozi wa serikali. Na wao ndio walikuwa wakiuziana na fedha zilizopatikana ziliingizwa halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga kwa madai ya faini. Na sisi tuliachwa maskini hadi sasa,” alisema Seni Jidamabi.

MWANANZILA: NI UHAMISHO WA KAWAIDA
Hata hivyo, Mwananzila alisema uhamisho huo ni wa kawaida.
Aliwashukuru wananchi wa mkoa wa Shinyanga kwa kipindi kifupi alichofanya kazi na kuwataka kumpatia ushirikiano mkuu mpya wa mkoa.

KAULI YA MRITHI WAKE
Naye Rufunga aliwaahidi wananchi wa mkoa huo kuwa ataongoza kwa kufuata misingi iliyopo katika katiba ya nchi.
Alisema milango ya ofisi yake itakuwa wazi kwa mwananchi yeyote, hivyo akawaomba wampe ushirikiano ili kuleta maendeleo mkoani humo.

TAMISEMI: NI KUBORESHA UTENDAJI WA KAZI
Naye Msemaji wa Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi), Luanda, licha ya kuthibitisha uhamisho wa wakuu hao wa mikoa, alisema umefanywa kwa lengo la kuboresha utendaji kazi.
“Kilichofanyika ni mabadiliko ya vituo viwili vya kazi za wakuu wa mikoa. Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mwananzila amehamishiwa Mkoa wa Lindi,” alisema Luanda.

Alipotakiwa na NIPASHE kueleza sababu za uhamisho huo, Luanda alisema: “Ni katika kuboresha utendaji kazi. Hakuna sababu nyingine yoyote.”
Mwaka 2006 serikali mkoani Rukwa, ilianzisha zoezi la kuwaondoa wafugaji wa kabila la Kisukuma kwa madai kuwa wanaharibu mazingira kwa kuwa na idadi kubwa ya mifugo kuliko uwezo wake.
Hata hivyo, zoezi hilo lililalamikiwa na wabunge kutoka mikoa ya wafugaji ya Shinyanga, Mwanza, Arusha na Manyara kwa kile kilichoelezwa kuwa liligubikwa na vitendo vingi vya ukiukwaji wa haki za binadamu.
Kutokana na malalamiko hayo, serikali ililazimika kusitisha zoezi hilo.

Operesheni ya kuhamisha wafugaji kwenye maeneo ambayo hawaruhusiwi, hasa maeneo oevu, ilitangazwa na Rais Kikwete wakati akizundua Bunge Desemba 30, 2005.
Rais Kikwete alitangaza kwamba maamuzi machungu ya kuokoa mazingira yangetangazwa na Makamu wake, Dk. Ali Mohamed Shein, Aprili mosi mwaka 2006, maamuzi ambayo yalisaidia kuwaondoa wafugaji kwenye vyanzo vya maji, kama eneo la Ihefu mkaoni Mbeya.
 
kwa hapa ndo mh dk jk ananiacha hoi,amekaa takriban mwaka tka aanze awam ya pili,hv kama kwl kwa mda huo wote alishindwa kujua hyu aende wapi yule wapi??hv si watalipwa hela ya transfer??inauma sana tena sana,na mungu yupo anatuona wote ss wanyonge na mackin

Andika sentesi kamili acha mammbo ya facebook na kwenye sms
 
Unaambiwa siku nyingine uwe una google!! Watu wanaamini kila kitu kinapatikana kwenye google!! Hii ni Tanzania, leo unasimamishwa kazi kesho unarudishwa kwa mamlaka aliyopewa anayekuridisha lakini kabla hujakaa sawasawa inakuja mamlaka nyingine inakurudisha likizo!!

Hili ndo tatizo letu kubwa, nimependa mchango wako
ingawa walio wengi sidhani kama wanaelewa unamaanisha nini...
 
Back
Top Bottom