King’asti
Platinum Member
- Nov 26, 2009
- 27,823
- 24,786
Baba, hujajua ni nini kilichokufikisha hapo ulipo? Umepata medali gani hadi sasa? Kuwasaidia ndugu sio tatizo, tatizo ni kuwalea kama mayai! Nawajengea mazingira ya kujitegemea, msaidie ndugu apate kazi aondoke. Aibu gani mtu anafukuzwa kazi ama anakufa familia nzima mnatafuta pa kutawanyikia? Mbona sie tumetoka kwako kila mtu anajitegemea hadi Cantalasia?
He! mwanangu ndivyo nilivyokufundisha hivyo, kutowajali ndugu zako wa damu na ndugu wa mumeo! mimi sijakufundisha tabia hiyo na najiuliza sijui umeipata wapi. wakati ule kabla sijakubinafsisha kwa mumeo si uliona jinsi nyumba yetu ilivyosheheni ndugu wa pande mbili wa mama yenu na ndugu zangu, kwani hujui hiyo ni mila yetu. sasa kwa nini uache mila?