Elections 2010 Kukatishwa Kwa Matangazo Jangwani: Tido Mhando Alonga

masasi

Member
Aug 3, 2010
48
0
ililkuwa kama zile sinema za akina rambo na waigizaji wengine,tbc kwa kile cha kulinda maslahi ya wakubwa wakaamua kukatiisha kurusha matangazo kwa sababu mabere marando alikuwa akifichua ufisadi wa kikwete,watu walishindwa kuzuia hasira zao na kuanza hata kmtupia makopo ya maji mtangazaji na kada wa chama marini hassan marini ambaye aliokolewa na vyombo vya usalama,
tbc eleweni kuwa watanzania si mabwege tena
 
Tiddo Muhando, anadai CHADEMA Walikiuka makubaliano ya Kutumia lugha ya Kistaarabu baada ya kuanza kukashfu watu binafsi . . .

Anadai walirudisha baada ya uongozi kuahidi marekebisho.

Leo katika Uzinduzi wa Kampeni ya CHADEMA; Marando alilonga kuwa ni Kikwete na Lowassa walimwomba Mkapa awapatie pesa ya Uchaguzi kitu kilichopelekea ufisadi wa EPA . . . . Matangazo yalikatishwa katika stage hiyo ya hotuba yake kabla ya kurudishwa dakika kadhaa baadaye

Tutasikia mengi . . .
 
Hebu ngoja niweke hivi; uhuru wa maoni ni pamoja na uhuru wa maoni ya kijinga. Uhuru wa maoni si lazima yawe maoni tunayoyataka sisi au tunayojisikia ni ya kutufurahisha. Uhuru wa maoni haupo ati kwa sababu lugha ni ya kistaarabu kwa hiyo ikitumika lugha isiyo ya kistaarabu basi kuna polisi (Tido) na wenzake ambao wanaamua kusema "hatutatiki kukusikiliza". Endapo mtu anasema kitu ambacho kinavuka uhuru huo yule anayesemwa anatakiwa kwenda mahakamani. TBC siyo msimamizi wa maoni hayo.

Lakini jingine ni kuwa madongo yaliyorushwa na JK na wenzake Jangwani dhidi ya wapinzani yalikuwa ni ya kistaarabu? Au ni ustaaarabu kuelekea CCM na siyo kwingine?

Lakini kubwa zaidi ni kuwa Watanznaia ni watu wazima na wana uwezo wa kusikiliza, kuamua na kukataa hoja za kijinga au kipuuzi. Hawahitaji serikali ikae kama nanny kuamua kusema "hili watanzania hawastahili kulisikia". Hakuna chochote ambacho kimetamkwa jangwani ambacho hakijawahi kluandikwa au kuzungumzwa na vyombo vya habari.

Jamani, kama demokrasia imewashinda wajaribu udikteta!
 
Kwani hayo ni matusi?
Kusema ukweli imekuwa si 'lugha ya kistaarabu' siku hizi?
Kwa hiyo wananchi wasielezwe ukweli kwa sababu unagusa watu binafsi?
 
Hebu ngoja niweke hivi; uhuru wa maoni ni pamoja na uhuru wa maoni ya kijinga. Uhuru wa maoni si lazima yawe maoni tunayoyataka sisi au tunayojisikia ni ya kutufurahisha. Uhuru wa maoni haupo ati kwa sababu lugha ni ya kistaarabu kwa hiyo ikitumika lugha isiyo ya kistaarabu basi kuna polisi (Tido) na wenzake ambao wanaamua kusema "hatutatiki kukusikiliza". Endapo mtu anasema kitu ambacho kinavuka uhuru huo yule anayesemwa anatakiwa kwenda mahakamani. TBC siyo msimamizi wa maoni hayo.

Lakini jingine ni kuwa madongo yaliyorushwa na JK na wenzake Jangwani dhidi ya wapinzani yalikuwa ni ya kistaarabu? Au ni ustaaarabu kuelekea CCM na siyo kwingine?

Lakini kubwa zaidi ni kuwa Watanznaia ni watu wazima na wana uwezo wa kusikiliza, kuamua na kukataa hoja za kijinga au kipuuzi. Hawahitaji serikali ikae kama nanny kuamua kusema "hili watanzania hawastahili kulisikia". Hakuna chochote ambacho kimetamkwa jangwani ambacho hakijawahi kluandikwa au kuzungumzwa na vyombo vya habari.

Jamani, kama demokrasia imewashinda wajaribu udikteta!

Well written!

Hakika sikuona mahali popote ambapo marando alimtukana mtu. Sana sana alisema anajua hawezi kumfanya kitu na kama wanaweza wampeleke mahakamani yeye ana ushahidi.

Ngoma inogile . . .
 
... siamini anachoongea huyu bwana mia kwa mia ... anasema yalitokea matusi ya nguoni na wakazimisha matangazo ...then wakarudisha... sasa wapi kulikuwa na matusi ya nguoni...?

Na kama sio mtangazaji Marine wa TBC ku@@@ makofi wasingerudisha ... matangazo...!!

Na inawezekana pia hii ni move iliyokuwa imeaandaliwa kuwahujumu CHADEMA kwani hapakuwa na umuhimu wowote wa kweli kukatisha matangazo na kukimbilia kuiponda CHADEMA kwenye taarifa ya habari...
 
Tido anadai kama wataendelea hivi, then siku za usoni watashindwa kufanya kazi . . .
 
Tido anadai kama wataendelea hivi, then siku za usoni watashindwa kufanya kazi . . .

Kwanini iwe ni CHADEMA tu siku ya kwanza ya kuzindua kampeni zake yote haya yatokeee? Kila mtu alikuwa anasikia ile kampeni...nini kilikuwa ni matusi ya kutishia kutokuwarusha tena CHADEMA hewani? Inaweza kumfanya mtu yeyote kudhani CHADEMA ianhujumiwa... from the day One...!!!
 
TIDO kwanu KBC ya mtukufu MOI iko mikononi mwa nani? Haya ndio kaseja alimwambia Maximo, unapita nitabaki maana mimi wa hapahapa
 
Poor TBC. Hii ni kuonyesha tu kuwa TBC ni kwa ajili ya CCM na si kwa vyama vyote
 
Tido amekuw3a kama si mtu aliyeishi na kufanya kazi Uingereza... Hivi ni yeye mwenye jukumu la kuwa polisi hao waongeaji au mapolisi wenyewe? Kwanza sijui nain alimpa kibali cha kazi maana hata Urai wake una utata! sijui ni mtanzania au ni mwingereza... kama hana kibalin cha kazi hebu arudi zake BBC FUL STOP...
 
Hii nayo ni hoja. Kama una data hebu anzisha thread mpya wadau wamchambue . . .
 
Hii nchi kazi kweli!!

Unaweza ukashindwa kuelewa kuwa yule Tido wa BBC na huyu wa TBC ni mtu mmoja.
 
Nilikuwa napata HARAMU na redbull mahala nikawa nakodolea macho tbsiii ghafla wakakata matangazo. pembeni yangu alikaa kanali mmoja mstaafu akabwatuka "HAWA JAMAA HAWAKULIPIA MATANGAZO YA MKUTANO WAO TBC NDO MAANA JAMAA WAMEKATA" nilikaa kimyaaa maana nilijua jioni hii nitapata unyeti wa suala lote na pia ufafanuzi kama matangazo ya kampeni live yanalipiwa and how much?
 
mwandishi au mtangazaji kupigwa ni DEMOKRASIA HURU.....SAFI NA YAFAA KUENDELEZWA NA VYAMA HIVI
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom