Elections 2010 Kukatishwa Kwa Matangazo Jangwani: Tido Mhando Alonga

Kilichonifurahisha zaidi na wakubwa wa TBC kuonyeshwa na umma kuwa wamechoshwa na tabia yao ya kuegemea upande mmoja. TBC sio Polisi wala mahakama, kama mtu anatukana wengine TBC walipaswa kuendelea kuchukua shooting ili mikanda hiyo itumike baadaye kama ushahidiwa kimahakama. Kitendo cha kukatisha matangazo nidalili za kupokea maagizo kutoka upande mmoja.

Hata Todo Mhando leo ametambua kuwa "Heshima yake inashuka" ndio maana akaikimbilia kutoa taarifa za upande mmoja. Iweja ashindwe kubalance hiyo stori ya ukiukwaji wa makubaliano kwa kuwahoji viongozi wa CHADEMA walioingia nao makubaliano? LEO TBC MMECHEMSHA!!!!!!!
 
Mnasifia vulugu? Kuna njia nyingi nzuri za kuonesha kutoridhishwa na mwenendo ya TBC lakini sio vurugu.
Kuweni wastarabu kama CUF

Hah! hah! hah! Usinivunje mbavu mtoto wa mwenzio. CUF wastaarabu??
 
mwandishi au mtangazaji kupigwa ni DEMOKRASIA HURU.....SAFI NA YAFAA KUENDELEZWA NA VYAMA HIVI

Na kwa chombo cha habari cha umma kukata matangazo ya chama kingine kutokana na amri ya chama tawala ni demokrasia huru -- safi na yafaa kuendelezwa na chama hicho tawala!
 
Nilikuwa napata HARAMU na redbull mahala nikawa nakodolea macho tbsiii ghafla wakakata matangazo. pembeni yangu alikaa kanali mmoja mstaafu akabwatuka "HAWA JAMAA HAWAKULIPIA MATANGAZO YA MKUTANO WAO TBC NDO MAANA JAMAA WAMEKATA" nilikaa kimyaaa maana nilijua jioni hii nitapata unyeti wa suala lote na pia ufafanuzi kama matangazo ya kampeni live yanalipiwa and how much?
Ilishajulikana kuwa haya matangazo yamelipiwa na UNDP kwa kila chama kupata 4 hours(masaa 2 kufungua na 2 siku ya kuhitimisha) hivyo wala si hisani. Maana ingekuwa hisani wasingethubutu kuonekana Jangwani.
Tido siku zako za kukaa TBC zinahesabika.
 
Alichokifanya Tido ni funika kombe mwanaharamu apite,inavyoonekana lilikuwa lengo lao kukutisha matangazo ili Dr Slaa asisikike live.Nasema hivyokwa sababu kuu mbili.
1. Kwa kuwa mara walivyokata walitupa taarifa kuwa kuna hitilafu kidogo imetokea hii ya kuvunja sheria mbona hawakuisema kule Jangwani?
2.Kama kweli sababu ilikuwa ni kurusha madongo kwa kuwataja majina watu kwanini iwe kwa Marando ambaye alikuwa anaongea muda mfupi kabla ya Mbowe na Dr Slaa?mbona kamanda Lissu alimchana Kikwete live na matangazo yaliendelea?

Habari ndio hiyo..
 
Na kwa chombo cha habari cha umma kukata matangazo ya chama kingine kutokana na amri ya chama tawala ni demokrasia huru -- safi na yafaa kuendelezwa na chama hicho tawala!

Ahsante Mkuu -- polepole tutarudisha maadili. Mi nadhani serikali ya CCM ilitaka kupata sababu ya kui-label Chadema kwamba ni chama cha vurugu -- yaani wafuasi wa Chadema wapandwe hasira pale ili polisi wao watembeze virungu na mabomu ya machozi .
 
Hivi nani mwenye mamlaka ya kusema chama fulani kimekiuka sheria ya uchaguzi? Tido ni mmiliki,mhariri au mpiga picha kwenye hicho chombo cha habari? Nani mwenye mamlaka ya kuhariri hata kusitisha vipindi vya kituo cha tv? Nimeshindwa kuelewa Kabisa kuwa Tido ni mwenyekiti wa tume ya uchaguzi, mhariri wa kampeni za vyama vya siasa au mmiliki halali wa tbc! Mpaka anaweza kutoa amri kusitisha asichokipenda kuona kisirushwe!
 
Hadi sasa hujui utawala wa CCM ni kama ule wa kambare? Kila mmoja ana masharubu. Inawezekana amri ya kusitisha matangazo ilitoka kwa Katibu Mkuu wa CCM wa Mkoa wa Dar -- yule Kihiyo nimesahau jina lake!
 
sio mda wote watu hupewa amri! Kujipendekeza kunatuponza sana! Unaweza kuta hata waliositisha matangazo walifanya hivyo ndio wakampigia tigo Ah sorry! tido nae ndio akawapa directives! Mimi hata nisingeuliza kama tido angekaa kimya bila kuzungumzia maana tulishaambiwa ni mitambo ambayo haipo tayari hata kwa fimbo kuendelea kuipokea sauti ya marando! Tido kaharibu kuongea kwamba chadema wamekiuka taratibu za uchaguzi na makubaliano! Nikawa najiuliza tido ni nani hasa kwenye tume yetu ya uchaguzi! Ukomo wa Mamlaka ya tido kwenye habari zinazorushwa na tbc ni upi?
 
Binafsi sioni kama ni utaarabu kuanza kubutuana kwenye kampeni, kwani amekuwa mwizi, mbona wezi wa epa, rada, richmund wanajulikana na ndo wanatuongezea umaskini, nyie mnaojifanya mna hasira na uchungu si muwafuate muwabutue. mnachofanya ni sawa na serikali ya ccm kupambana na rushwa kwa kupeleka mahakamani wanaochukua shilingi elfu kumi na hata kuwanyima dhamana wakati mramba, chenge, lowasa, sumaye n.k wanapeta.
Nasema nyie chadema na wenye hasira kawapigine hao magwiji maana mnakutana nao mabarabarani na kwingineko, ACHENI HIZO HUO NI UOGA
 
Tido amejidhihirisha kwamba yeye ni mbumbumbu hata wa fani ya uandishi na utangazaji. Kama ushahidi wa tuhuma hizo UPO, na Marando anao, akisema hayo kuna kosa gani?

Ustaarabu anaoutaka ni CCM waendelee kukwiba kama walivyofanya kukwapua pesa za serikali kutengenezea mabango ya JK kwa kuitumia kampuni ya MEDIAPIX? Habari hizo ziliripotiwa MwanaHalisi, mpaka leo Salva hajatoa jibu.

Ustaaraby my ass!
 
mwandishi au mtangazaji kupigwa ni DEMOKRASIA HURU.....SAFI NA YAFAA KUENDELEZWA NA VYAMA HIVI
Sijui njia sahihi ni ipi maana wakiendelea hivyo huoni sikumoja mtu ataumia...?, hivi hakuna sheri ya kukishitaki chombo cha habari cha serikali maana hii ya kupiga...
 
mwandishi au mtangazaji kupigwa ni DEMOKRASIA HURU.....SAFI NA YAFAA KUENDELEZWA NA VYAMA HIVI

We dogo Mahesabu ondoa hiyo picha ya JKN. Unamwaibisha tu kwa upupu wako hapa jamvini.

JKN was a great thinker. You are truly a great sinker!
 
Marin asipoangalia iko siku atatolewa ngeu na kupata ulemavu wa maisha! Ushabiki kwa CCM mbele ya walalahoi wenye uchungu na nchi yao ni KOSA LA JINAI! Adhabu yake ni papo kwa papo! Natumai amejifunza! Mwingine wa kupewa onyo ni Jane Shirima! Shaaban Kissu asipoangalia, naye ataadhibiwa hivyo hivyo!

Hawa watu wanautafuta Ukuu wa Mikoa na Ukuu wa Wilaya kwa nguvu zote. Kwenye Serikali ya Slaa vyeo hivyo HAVIPO! Hahahaha! Wajiandae KULOSTI!
 
Tido anadai kama wataendelea hivi, then siku za usoni watashindwa kufanya kazi . . .

Hapo ndio watanzania watawafundisha TBC kufanya kazi kwa kufuata maadili. Waulize tabia ya fire kwenda kwenye tukio la moto bila maji imeishia wapi siku hizi
 
I said it earlier naona TBC imetimiza kuleta distraction (https://www.jamiiforums.com/uchaguzi-tanzania-2010/70938-uzinduzi-chadema-be-aware.html)

Kitu kimoja ambacho hawa apologists wa CCM wanashindwa kuelewa ni kwamba wanapofanya hizi mbinu za kitoto toto wanakuwa wanazidi kuitangaza CHADEMA. And the other thing from the meadia point ofv view ni kwamba jk na watu wake wameshawaonwa..a sana kwenye TV pple need see some new faces and new talk points.
 
Hapo ndio watanzania watawafundisha TBC kufanya kazi kwa kufuata maadili. Waulize tabia ya fire kwenda kwenye tukio la moto bila maji imeishia wapi siku hizi

Mpambalyoto kuna uwezekano wa kuondoa hilo panga kwenye Avatar yako? linaogopesha kukujibu si unajuwa sisi ni watu wa amani TZ.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom