Kukatika umeme hovyo hovyo Tanesco kuna agenda gani?

Quarterpin

JF-Expert Member
Mar 19, 2013
1,253
1,083
Jaman hii ni kero sasa naona TANESCO wana mpango wa kutuharibia vitu manake wanakata umeme kila wakati ukiwaka haliishi lisaa wanarudisha wanakata tena siku nzima.

Hivi kuna mgao usio rasmi au ndio watu wanakomoana kupitia vitalu vya gesi?
 
Wadau mimi nashindwa kuelewa! Huku kwetu maeneo ya Tegeta, Mbezi Beach, Makongo mpaka kupandisha huku juu Mbweni hadi Boko Bunju umeme unakatika kila siku kwa takribani masaa zaidi ya 7, tujuzane jamani mliopo maeneo mengine ya Dar hali ni kama hii au ni huku kwetu tu!?
 
Mwananyamala pia wanadai ni hivyo hivyo mkuu ndio bongo tuvumilie tu.
 
Aisee bongo hapaeleki huku umeme unakatika kila siku kuanzia saa tatu am wanarudisha saa mbili usiku au saa 10 jioni maeneo ya tegeta-chama.
 
Nadhani shirika linaelekea kushindwa kabisa kutoa huduma, kama yalivyokufa mashirika mengine ya umma. Huwa inaanza hivyo taratibu mwishowe itakuwa hakuna umeme kabisa.
 
Nadhani shirika linaelekea kushindwa kabisa kutoa huduma, kama yalivyokufa mashirika mengine ya umma. Huwa inaanza hivyo taratibu mwishowe itakuwa hakuna umeme kabisa
 
Na mwaka huu mvua zimenyesha sana tu je ikifika kiangazi sijui hali itakuwaje.
 
mimi mara nyingi nawaona wanabadilisha nguzo za umeme zilizochakaa maeneo ya sinza
 
Bunju wanakata mchana wanarudisha usiku........huu ni mgawo wa kimya kimya......lakini kama kawaida waandishi wetu wa habari wanasubiri kunukuu habari za warsha,makongamano na mikutano ya wanasiasa.........
 
Back
Top Bottom