Kukaa nyumba za bure ni umaskini tosha

Job Richard

JF-Expert Member
Feb 8, 2013
3,868
2,178
Katika maisha ukihitaji kusonga mbele usikubali kukaa nyumba ya bure.

Ukichunguza kwa umakini kuanzia wafanyakazi wote waliopewa nyumba za bure mpaka kustaafu kwao bado walikuwa wakiishi humo mwisho wanahamaki hana hata kiwanja.

Vijana wenzangu kama una nguvu zako usikubali kuishi nyumba ya bure. Wengine ndio wajingaaaa kabisa, anapewa nyumba na wakwe zake anakubali; huko ni kuolewa ukweni aiseeee!

Mwanaume kupambana chochote kianzie kwako, ni raha ukanunua uwanja kwa pesa ya jasho lako ukajenga mwenyewe.
 
Dah kwakweli hata mm nikipewa nyumba na babamkwe sidhani kama nitaishi kwa amani.
 
Sema wakati mwingine ukitumia akili vizuri, hii ni fursa yaani unajenga au kukuza biashara yako with 0 residence stress.
Unless kama hunywi pombe, zamani huku majeshini ilikua kila kitu bure..sikuhizi tangu JK apate mkopo wa zile nyumba ziko 2006 nadhani nchi nzima..unakatwa kwenye mshahara, unalipa bili zote..ni bora ukapange uraiani..Theres no free lunch in New York
 
Katika maisha ukihitaji kusonga mbele usikubali kukaa nyumba ya bure.

Ukichunguza kwa umakini kuanzia wafanyakazi wote waliopewa nyumba za bure mpaka kustaafu kwao bado walikuwa wakiishi humo mwisho wanahamaki hana hata kiwanja.

Vijana wenzangu kama una nguvu zako usikubali kuishi nyumba ya bure. Wengine ndio wajingaaaa kabisa, anapewa nyumba na wakwe zake anakubali; huko ni kuolewa ukweni aiseeee!

Mwanaume kupambana chochote kianzie kwako, ni raha ukanunua uwanja kwa pesa ya jasho lako ukajenga mwenyewe.
Mkuu umetoa ushauri mzuri, isipokuwa kuna mambo nadhani hauyafahamu kwa kina.

"Nyumba za bure" kwa taasisi nyingi kuziishi ni takwa la lazima na siyo chaguo ama hiyari!

Hapo ushauri uliotakiwa kuutoa kwa hao wanaoishi nyumba za bure, ni kuishi kwa aikili huku wakiwekeza akili zao kujenga nyumba zao.

Na kama ulivyoshauri wasibweteke na kujisahau!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom