Kuigiza Maisha kunavyowatesa watoto wa masikini vyuoni

Pesa ya boom iliniwesha kuwa na getho ambalo mpaka namaliza chuo sikiweza kuliacha. Mana baada ya miaka mitatu geto lilikuwa na kila kitu mpka naanza kazi niliendelea kukaa pale geto mpaka nilipooa ndio nikahama. Sema nilikuwa najibana mnp mana ndo ela pekee niliokuwa naitegemea
 
Ndugu yangu pesa ya boom haitoshi kabisa wazee wengi wanapuuzia kuwasaidia watoto kisa eti wanapata boom! Fikiria TZS 520,000 KWA MIEZI MIWILI, Ale alale na kutoa copy kwa miezi miwili! (Siku 60).
Wakija huku mtaani ndio watajua kama inatosha au haitoshi, laki mbili na nusu haitoshi kwa mwezi hulipii umeme, hulipii maji, hulipii kodi kula tu na kutoa kopi? Kwanza hela ya stationery inajitegemea kama mtu alinywea bia hilo ni tatizo lake
 
Hiyo pesa nyingi sana kwa mtu mwenye budget nzuri. Mimi nimesoma bila mkopo nashangaa sana kuona watu wanasema hiyo pesa ni ndogo.

Hiyo pesa ukitunza vema, nusu yake inakutanata na ya mwezi unaofuata na unaweza kuvuka nayo semester moja ukaingia semester nyingine ukiwa nayo.

Kimsingi ni kama mleta uzi anavyosema shida ipo kwa wanafunzi mitazamo yao ni ya hovyo.

Ebu acha sound bana kwa bajeti ipi lbda utwambie
 
Mnawasema bure lakini Umri wao unawaruhusu kufanya anasa na starehe, ukivuka hiyo stage na ukayaendeleza hayo, sasa ndio ya kuonekana mtu mzima lakini hovyo,

Imagine vidato vyote ulikua boarding schools, leo booom upo chuo kikuu, uhuru kama wote hakuna mama, baba, mjomba wala shangazi wa kukuhoji unaishije, unapewa pesa ya kujikimu, unaishi zako hostel unajiamulia ule nini, uvae nini, nyie nyie kama hujapata muongozo imara hapo ndio unapotumbukia shimoni,

Yote kwa Yote Enjoy ujana wako haurudi nyuma huo.
 
Nina mdogo wangu wa kike anasoma chuo kimojawapo hapo mjini DSM, ana mkopo asilimia 100

Lakini juzi mwezi wa saba nilimkuta nyumbani kwa wazee analia njaa ,tukajichanga pale tukampatia pesa ya matumizi akarudi chuo

Mtoto hovyo sana yule.
 
Wakija huku mtaani ndio wayajua kama inatosha au haitoshi, laki mbili na nusu haitoshi kwa mwezi hulipii umeme, hulipii maji, hulipii kodi kula tu na kutoa kopi? Kwanza hela ya stationery inajitegemea kama mtu alinywea bia hilo ni tatizo lake
mtu anatamani hata apate elfu hamsini tu,alafu vikiwa chuo vinaleta nyodo na kuona kila mtu hajasoma ukipishana navyo njiani
 
Mnawaonea tu hawa watoto hata nyie mlipitia maisha ya anasa chuoni,si vizuri kujitoa ufahamu kuwasema madogo;kuna maisha binadamu lazima upitie na katika maisha kila umri una matukio yake ,kipindi cha utoto kuna matukio lazima utayafanya...kipindi cha balehe na ujana kuna matukio lazima ufanye wapo walioruka hayo matukio wamekuja kuyafanya ukubwani mwisho wa siku wanaonekana kituko.
Kijana kama pesa ipo kula vizuri,kunywa vizuri,lala vizuri,vaa vizuri pendeza fanya outing zote maana kuna muda ukifika hautoweza kuvifanya
 
Acheni mawazo ya kikoloni.

Waacheni watoto waishi wapendavyo maana mwisho wa siku wao ndio watalipa hilo deni la Heslb na sio nyinyi

Jifunzeni kuishi kulingana na wakati na mazingira yanayokuzunguka.
Ogopa sana hiyo kauli ya"kuishi upendavyo", hii dunia sio baba yako na sio mama yako, watu wanajifanya wanaijua sana wakati yenyewe haimzoei mtu wala haina urafiki na mtu. Ishini kwa akili, dunia haina huruma, tunatakiwa kuishi tuwezavyo, siyo tupendavo.

Vv
 
Sasa Kama hauna uwezo wa kula Piza kila siku,si bora ule zako miogo kuliko kulialia kua 520000 ni pesa ndogo sana! Ishiii kutokana na kipato chako ukilazimisha show off itaumia sana!!
Wanasema ndogo maana wana wa kumlilia,amalize chuo aje uraiani
pata kazi kwa mishahara hii ya kibongo,afu mwambie mwajiri wako kwamba pesa haitoshi usikie jibu lake
 
Acheni mawazo ya kikoloni.

Waacheni watoto waishi wapendavyo maana mwisho wa siku wao ndio watalipa hilo deni la Heslb na sio nyinyi

Jifunzeni kuishi kulingana na wakati na mazingira yanayokuzunguka.
Hii ni sawa na kujifariji kwamba tumia pesa ikuzoee,matokeo yake unakopa mpaka mikopo inakupeleka jera
unajikuta unalizoea gereza .
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom