Kuigiza Maisha kunavyowatesa watoto wa masikini vyuoni

Maisha yangu yachuo vitini vyangu vinahesabika haijawahi zidi elf kumi Hadi namaliza chuo


Sasa nashangaa nyie mnatoa copy unajaza madude yasio na kazi,kwani huwezi summerize?
Inategemeana unasoma nini? Uprint kazi? Hununui vitabu? Hufanyi Assignment?
 
Kuna nukuu moja ya mtunzi wa vitabu vya ziada Tanzania, Zist Kamili niliwahi kuisoma nikiwa kidato cha tatu.

Katika nukuu Ile Kamili alisema "wanadamu hatuwezi kukaa kwa amani muda wote kwakua kila mmoja anapambana kuwa bora zaidi ya mwenzake" mwisho wa kunukuu.

Katika nukuu hii nilipata kuelewa mambo mengi yanayotuzunguka wanadamu mfano mapambano ya kiuchumi ambapo kila siku watu hupigana vikumbo ili kupata pesa, ajira na fursa nyingine vya msingi ili kuwainua kiuchumi.

Sikuwahi kufikiria kuwa kauli hii ni pana na kubwa kiasi gani mpaka pale nilipoitafakari zaidi mara ilipokuja katika kumbukumbu.

Nukuu hii ilibamba zaidi pale nilipopata uzoefu wa maisha ya wanafunzi wa vyuo mbalimbali nchini namna ambavyo wanapambana kuwa bora baina yao.

Ingawaje mapambano yao sio ya namna Ile aliyo isema Kamili bali kwa mlengo mwingine wa kupambania ufahari.

Ni vigumu kuelewa kuwa ni kwa namna gani jamii inatambua maisha ya watoto wao pindi wanapowasili vyuoni kutoka nyumbani.

Kuna kisa cha mama mmoja ambaye ananisimulia kuhusu adha ya kulipa gharama mbalimbali za mtoto wake wa kike anaesoma katika chuo kikuu mojawapo katika jiji la Dar es salaam nchini Tanzania.

Mama huyo anasema licha ya mwanae kuwa na ufadhili wa mkopo wa elimu ya juu zaidi ya Asilimia 85 lakini bado hajapumzika kutuma fedha kwa mwanae.

Anasema licha ya mwanae huyo kupata fedha ya kujikimu kila baada ya Siku 60 kutoka bodi ya mikopo lakini bado amekuwa ombaomba kila kukicha.

"Mwanangu kila muda amekuwa mtu wa kunisumbua kuhusiana na fedha ya ada na matumizi chuoni, mfano mwaka jana alidai anataka shilingi laki 7 kwa ajili ya kumalizia kulipa ada na kulipia ziara za kimasomo" anasema mama huyo.

Anahoji fedha inayo tolewa na bodi ya mikopo huwa ina masharti gani katika matumizi yake na ina nafuu gani kwa walezi na wazazi nyumbani.

Kabla hajamaliza simulizi yake nakumbuka maisha ya wanachuo wengi wanapoanza masomo ambapo wengi wao huanza kuishi maisha ya hali ya juu sana ambayo sio sawa na hali yao ya kiuchumi "kufake".
Nakumbuka namna ambavyo wanachuo wengi huingia kwenye mkumbo wa kuigana matumizi pasipo kujua uchumi wa familia zao unalingana vipi.

Simulizi ya mzazi huyu inagusa hisia zangu naahidi kufanya upelelezi ili kujua nini sababu ya kile kinachomsibu mwanae kama ni ukubwa wa ada ya chuo, kupanda kwa gharama za maisha ama kuishi nje ya uhalisia.

Narejea simulizi nyingine niliyowahi kupewa na rafiki yangu mmoja wa chuo juu ya jamaa yake wa karibu ambaye baada ya kupata fedha ya kujikimu alitumia asilimia 80 ya fedha hiyo kununua runinga kubwa ya kutazamia filamu chumbani kwake huku akiwa anaandamwa na madeni ya hapa na pale ya kukopa.

Nikumbuka pia kisa cha yule mdada aliyetumia nusu ya pesa ya ada aliyopewa na wazazi wake kuandaa Sikukuu yake ya Kuzaliwa 'birthday" matokeo yake akakosa kufanya mtihani Kabisa kwa kutokamilisha ada.

Kufake maisha ni pigo kwa wanachuo wengi si wa kiume wala wakike msumeno umekata kotekote.
Kufake maisha ndiko kunawafanya wanachuo wengi wasikumbuke hata kurudi nyumbani kwao pindi kikizo inapowadia kwa kuhofia watarudi na hali gani na watatazamwa vipi pindi watakaporejea vyuoni.

Pia hali hii ndio inawafanya watoto wa maskini vyuoni kujiona wamemaliza yote hata kushindwa kusalimiana na ndugu zao waliotoka Kijiji kimoja pindi wanapokutana.

Kufake maisha ndiko kumewafanya wadada wengi waolewe pasipo kupenda baada ya kumaliza vyuo kwa kuhofia watarudi vipi nyumbani na kupokelewa kwa mtazamo chanya na walezi wao.

Peter Mwaihola

View attachment 2444552
Huwa unapenda kukaa na wamama na kuskiliza stori zao....
 
Maisha yangu yachuo vitini vyangu vinahesabika haijawahi zidi elf kumi Hadi namaliza chuo


Sasa nashangaa nyie mnatoa copy unajaza madude yasio na kazi,kwani huwezi summerize?
Maisha yangu ya chuo niliamua kuwa kiongozi na watu walizani napenda uwongozi bila kujua target yangu ilikuwa ni future baada ya uwongozi. Nilitengeneza connection na watu wa stationary baada ya kumaliza uwongozi mimi vitini ilikuwa Bure napewa, connection na waalimu ilikuwepo kwenye quiz huko hata nisipokuwepo nina uhakika wa marks kupata na kibaya zaidi assignment zaku print nilikuwa siifanyi, naenda kibandani nakuta wenzangu wamepeleka kazi zao mm nafanya kuchagua ya mtu nayemtaka napew na edit then na submit... kwanii kwasababu nilikuwa na connection za kuuwappatia kazi za ku print
 
Ni kweli haitoshi mwingine yupo nje ya chuo amekodi chumba analipa Kodi lkn Kuna Mambo wanayafanya yasikua na faida mfano kushindana mwenzake kisa anamiliki kitu Fulani na yeye anataka kumiliki wengi unakuta iPhone za 500k wakati maisha ya kwao ni kuungaunga.
Ndugu yangu pesa ya boom haitoshi kabisa wazee wengi wanapuuzia kuwasaidia watoto kisa eti wanapata boom! Fikiria TZS 520,000 KWA MIEZI MIWILI, Ale alale na kutoa copy kwa miezi miwili! (Siku 60).
 
Pia maisha ya mtaani ya gharama nyingi....wote tumeoitia huko Chuo ukisema Boom halitoshi hio Ni kauli ya kishua sana mtoto unayetoka uswazi life gumu huwezi sema 250,000 kwa mwezi haitoshi hio Ni nyodo na kudhihaki Mungu.

Yes kwa Standard za maisha haitoshi Sasa je wewe mtoto wa maskini una Standard za maisha tunaishi kwa basics ukitaka standard hata 700,000 kwa Mwezi haitoshi.

Hiyo pesa ya Boom ukiishi na bisics unakula vizuri unatoa Copy za notes zote na kusafiri na Pesa inatosha zaidi Wana wengi sasahivi tulionao mtaani na wanapata 100K kwa Mwezi now Wana realize pesa ilikuwa inatosha
Suala la photocopy sio page 1 ni 100 Kama umetype mwenyew kazi sema uvivu tu, Wala hauhitaji computer simu unaweza kutaype kazi Yako vizuri tu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom