Kuibuka na kufa kwa Merilyn Monroe

Nina

Ninazo Novel mbili za Marilyn Monroe, search Hilo Jina huko Facebook na Google utamwona,ni maarufu kuliko unavyofikiria
si kwamba simjui, namjua vizuri tu mkuu ila nachosema "amekuzwa sana" kwa lengo la kutengeneza fedha.

mfano ni hivyo tu tayari unazo novel zake mbili.. someone has make money out of her..
ndio wazungu walivyo sasa.

Ni kama ile picha ya monalisa pale ufaransa.
 
Sehemu ya 03

Monroe anasema kuna wakati alihisi kama alikuwa nje ya dunia halafu ghafla tu dunia inafunguliwa na kila mtu kumpokea. Ndiyo! Hivyo hujisikia kila mtu kwenye dunia hii. Inafika wakati unaona kabisa kama hauishi kwenye dunia hii.

Kuna watu wanakula raha, wanakula maisha lakini kila unapojiangalia, unaona kabisa unaishi kwenye dunia ya peke yako, yaani si hii dunia ambayo watu wanatumia mpaka milioni 50 kwa usiku mmoja tu kula bata.

Sasa kwa Monroe, ilifika kipindi akajiona ameingia upya duniani na kuishi maisha yake sasa. Amekuwa staa mkubwa lakini anakiri kwamba watu ndiyo wamempa ustaa huo ambao ulimfanya kuanza kutengeneza pesa nyingi huku akiwa na umri mdogo tu.

Kuna kitu Wazungu wanapenda sana kukisema ‘The sex symbol of the country’. Hii huwa kwenye kila nchi, kunakuwa na mwanamke mmoja ambaye huvutia kimapenzi (kingono) kuliko wanawake wengine maarufu. Miaka ile ya 2000, Tanzania tulikuwa na Ray C, nadhani mnakumbuka mpaka tukamuita kiuno bila mfupa. Sasa kwa Marekani, kwa miaka hiyo, mwanamke huyo alikuwa Monroe.

Kulikuwa na daktari mmoja aliyekuwa akiitwa Ralph Greenson. Huyu alikuwa daktari pekee wa saikolojia aliyekuwa akiongea sana na Monroe. Watu wote waliokuwa wakihitaji kuonana na daktari huyu ilikuwa ni lazima kwenda ofisini kwake lakini haikuwa hivyo kwa Monroe.

Kumbuka huyu alikuwa staa mkubwa mno Marekani, kitendo cha kuja kwako, tayari kungekuwa na usumbufu mkubwa sana kwa wengine, hivyo dokta akawa anakwenda nyumbani kwake kuzungumza naye.

Kwenye hilo, baada ya dokta huyo kufariki, aliacha maandiko yake ya kiofisi kuhusu kila mgonjwa aliyekuwa akizungumza naye, na kwenye maandiko kuhusu Monroe, aliweka wazi kwamba kila alipokuwa akizungumza naye, aliona ni maisha gani aliyokuwa amepitia kitambo yalivyokuwa yakimuumiza.

Wenzetu wanapokuwa wamefanikiwa, bado kuna maisha ya nyuma hubakia kuwa maumivu makali mno. Mfano mwanamke amebakwa, na hamfahamu mbakaji wake. Hata akija kufanikiwa na kuwa bilionea, bado suala hilo lingeendelea kumtafuna maisha yake yote mpaka anaingia kaburini kama ilivyo kwa Oprah Winfrey.

So kwa Monroe ilikuwa hivyo. Hakuishi sana na mama yake, hakuwa na pesa, na maisha yake yalikuwa choka mbaya na muda mwingi aliumwa yale magonjwa ya akili, hivyo akachukuliwa na kwenda kuishi kwenye kituo cha watoto yatima. Aliishi huko kwa miaka minne, baadaye akachukuliwa na mlezi mmoja na kuishi naye.

So dokta alipokuwa akiongea na Monroe alijua kabisa kitu pekee alichokuwa akihitaji msichana huyo kilikuwa ni familia. Alihitaji kupata familia ya kuishi naye.

Wakati mtoto wa dokta akifanya mahojiano, alisema kwamba kwa wagonjwa wote ambao baba yake alikuwa akifanya nao mazungumzo, hakuna hata mgonjwa mmoja aliyewahi kujiua, alishangaa kwa nini iwe kwa Monroe? (Hapa kuna swali, je, alijiua? Tutaona baadaye)

Kumbuka hapo juu nilikwambia kitu ambacho alikitamani sana Monroe ni familia, hakuwahi kuishi na familia hivyo dokta akamtambulisha kwa familia yake na akaanza kuishi nao kwa ukaribu, ile mnaitana dada na kaka.

Siku moja Monroe alimwambia binti wa dokta, Joan kwamba alipata mwanaume mpya, mzuri wa sura, anayeonekana kujali, si unajua wanawake wakiwa wanapiga stori kuhusu mwanaume fulani. Na alipoulizwa mwanaume huyo aliitwa nani, akajibu aliitwa GENERAL.

Hakutaka kumwambia jina lake, ila alimwambia cheo chake tu kwamba alikuwa General. Sasa hilo likaaanza kukisumbua kichwa cha Joan, General alikuwa nani kiasi cha kupendwa hivyo na Monroe?
Hapa acha nipige ngeli kidogo kwa hivi vyeo. General alikuwa mtu wa ndani mwa Justice Department, na hapo alimaanisha Attoney General, Robert Kennedy ambaye alikuwa mdogo wake rais wa Marekani kipindi hicho, John Kennedy.

Joan anasema kitu cha kwanza hakuwa akaiamini kama kweli alikuwa akizungumza na Monroe kuhusu wapenzi wao, na hata aliposema alikuwa akipendana na General, hakuwa akijua alikuwa akimzungumzia Robert ama rais.

Sasa hapa ndipo kulipoanza matatizo kwenye maisha yake. Hiyo ilikuwa ni mwaka 1961, yaani ni mwaka mmoja na miezi kadhaa kaba ya kifo chake.

Je, nini kiliendelea?
JamiiForums-2019035701.jpg
 
Haku"tetemesha kila mtu" bana, wazungu wanajua ku-hype vitu sana.. wanajua kuuza habari, wanajua kutengeneza mada. they can make business out of nothing,
apo vitaandikwa vitabu, zitachezwa movie, zitatengenezwa conspiracy theory nyingi ili watu wapige hela.

ni kweli alikua mzuri, na kipaji kidogo,
kama tu hawa akina wema na akina hamisa.

dont believe everything they told you.
Vip ulikua unaishi naye miaka hiyo uko kwao?maana ikisemwa kila mtu haimaanishi watu wote duniani.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom