Kuhusu Rwanda na Tanzania: Tuweke rekodi sawa

Mara ya mwisho tunakutana hapa ulikimbia kwa kisingizio unaenda kulala kumbe ulikuwa unaenda kukusanya propaganda za kujaza server hapa. Ngoja nimalize majukumu ya jpili halafu nitarudi
Propaganda maana yake ni uongo, onyesha ni wapi katika hiyo post nimeandika uongo. Ukishindwa maana yake wewe ndio unapiga propaganda kuwa mimi napiga propaganda.
 
“This time, I think relations have become extremely warm and a new chapter is being opened, and there have been a tremendous amount of goodwill and assurances from both sides, and I think we are on a totally different trajectory in terms of relations between Tanzania and Rwanda,”said Mahiga.
sawa kabisa, "new chapter is being opened", maana yake kulikuwa na chapter mbovu iliyopita.
 
hapo sasa ndio ujuwe kuwa na jirani nuksi ni mbaya sana! yani FDLR inatumia vifaa vya FARDC na serikali ya DRC bado inawakenulia tu? ingawa chanzo ni kutoka Rwanda lakini hii habari imeripotiwa sana tu na maiti ndio kama unavyoziona kwenye picture!
Hivi kwa nini unapenda kuzungumza uongo ? James Kabarebe ni mjomba wake Hyporite Kanambe ( Joseph Kabila) ,pale alipo amewekwa na paka baada ya kumuua baba yake wa kufikia Laurenti Kabila sasa iweje aishambulie Rwanda? Acheni sarakasi zenu.
 
Kwa bahati mbaya ziara ya rais wa Tanzania mhe John Magufuli nchini Rwanda inapotoshwa sana hasa na mashabiki wa Rwanda/kagame humu mitandaoni mfano rejea: Wako wapi wale anti Kagame?.
Mhanga wa ziara hiyo amekuwa rais mstaafu Jakaya Kikwete, ambaye katika hali isiyo ya kawaida analaumiwa kwa ugomvi ambao kwa mtu yoyote makini ulishakwisha toka mwaka jana! Yafuatayo ni maoni yangu juu ya vitu muhimu ambavyo vinapotoshwa:

1. KUZOROTA UHUSIANO NI KOSA LA KIKWETE:

Ukisoma maoni ya wanazi mbalimbali wa Rwanda/Kagame, Tanzania inaonekana kuwa ndio iliyoikosea Rwanda. Suala hili sio kweli.

Jambo la kwanza lililozorotesha uhusiano wetu na Rwanda ni pale ambapo Tanzania iliamua kuungana na mataifa ya DRC na Afrika kusini kuwapiga waasi wa M23 kijeshi mwaka 2013. Maamuzi haya yalikuwa kinyume na mtazamo wa mataifa ya Kenya, Uganda na Rwanda ambao wakati huo walikuwa wakijiita COW (coalition of the willing), ambao wao walipendelea mazungumzo yasiyokuwa na tija yaendelee kati ya M23 na Uganda. Ni siri iliyokuwa wazi kuwa majeshi ya M23 yalikuwa ni vibaraka wa Rwanda. Hili limethibitishwa na ripoti ya umoja wa mataifa. Pia nchi za marekani na Uingereza zilisitisha misaada kwenda Rwanda kama adhabu (kama sisi tulivyokosa pesa za MCC) kutokana na nchi hizo kujiridhisha kuwa Rwanda ilikuwa nyuma ya M23, cha ajabu Rwanda haikuwahi kuzishutumu nchi hizi kama ambavyo ilimshutumu waziri Bernard Membe ambaye yeye alirejea taarifa hizo hizo za umoja wa mataifa.

Suala lingine lililoleta shida ni pale ambapo rais Kikwete, katika mkutano wa nchi za maziwa makuu, alishauri mazungumzo kati ya serikali na waasi wa nchi mbalimbali zenye vita ikiwapo Rwanda. (chanzo: KIKWETE Statement on Rwanda misquoted | The Rwandan). Ushauri huu ulipokelewa vizuri na nchi zote Uganda na DRC kasoro Rwanda. Hakukuwa na shida yoyote kama Rwanda wangepuuza ushauri wetu, lakini cha ajabu uongozi wa serikali ya Kagame ukalipuka kwa matusi na kashfa mbalimbali za kutuita interahamwe, uzushi kama kabila la mke wa Rais na mengineyo na mwishowe kwa rais Kagame binafsi kutishia kumpiga Kikwete. Hali hii ikapelekea Tanzania nayo kujibu mashambulizi kwa maneno mbalimbali.

Hata hivyo ugomvi huu ulikuwa ni vita baridi, kwani mahusiano ya kibalozi bado yaliendelea pale pale, hakuna siku wananchi wa Tanzania au Rwanda nikiwamo mwandishi wa post hii walizuiwa au kurudishwa mpakani pale walipotaka kuvuka. Hakuna manyanyaso yoyote ambayo raia wa nchi zetu walizipata wakiwa wanaishi na kufanya kazi kihalali nchi nyingine. Hivyo ugomvi huu ulikuwa ni wa ngazi za kisiasa zaidi na haukufika chini kwa viwango vya wananchi kuonana maadui, isipokuwa labda kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa sababu zote kuu mbili za ugomvi wetu, hakuna uwezekano wowote kuwa rais Kikwete au nchi ya Tanzania ndio iliyokosea. Ni upotofu mkubwa kumlaumu Kikwete na Tanzania kutokana na ugomvi uliotokea. Uongozi wa rais Kagame wa Rwanda una historia iliyotukuka ya kugombana na nchi nyingi duniani kuliko nchi yoyote hapa Afrika labda na dunia kutokana na hulka yake ya kibabe. Mifano michache ni:
  • Kufukuzwa kwa ubalozi mzima wa Rwanda nchini Kenya mwaka 1996 kutokana na mauaji ya mpinzani/mkimbizi wa kisiasa Seth sendashonga yaliyofanywa na maafisa ubalozi huo
  • Kufukuzwa kwa ubalozi wa Rwanda nchini afrika kusini 2014 kutokana na majaribio ya mauaji ya mpinzani/mkimbizi wa kisiasa Gen Kayumba Nyamwasa.
  • Kufukuzwa kwa diplomat wa Rwanda Evode Mudaheranwa nchini Sweden 2012 kwa tuhuma za kufanya ujasusi dhidi ya wakimbizi wa kisiasa nchini humo.
  • Kufukuzwa kwa diplomats wa Rwanda nchini Burundi 2014 akiwamo Desire Nyaruhirira ambaye baada ya kutoroka inadaiwa nyumbani aliyokuwa anaishi kulikutwa silaha nzito za kijeshi na kiasi kikubwa cha fedha za kimarekani!
Pia kwa nyakati tofauti Rwanda chini ya rais Kagame imeshapambana kivita na Uganda nchini DRC, imeshapamba na DRC wenyewe, burundi etc, na kutokana na ripoti ya UN (rejea: Kutoka ripoti ya UN: Tanzania na Rwanda zilishapigana!) hata Tanzania kupitia M23! Ukiunganisha na kufukuzwa kwa mabalozi wake nchini Kenya, Rwanda chini ya Kagame inakuwa na historia ya kuwa imegombana na nchi zote za EAC! Kwa mifano hiyo michache (ipo mingine ya magomvi na nchi za ulaya na marekani) haiingii akilini kudai kuwa Kikwete/Tanzania ndie chanzo cha kuzorota kwa uhusiano wa nchi zetu mbili. Tulikuwa sahihi na bado tuko sahihi.

2. KURUDI KWA UHUSIANO KUNATOKANA NA ZIARA HII YA MAGUFULI:

Ukweli ni kuwa marais Paul kagame na Jakaya kikwete walikutana na kuzungumza hadharani kwa mara ya kwanza baada ya nchi zetu kupishana maneno kwenye mkutano wa 16 wa viongozi wa Afrika mashariki kwenye ukumbi wa KICC pale Nairobi mwezi februari mwaka 2015.

Wiki chache baadae mwezi march 2015 Kagame alikuja Tanzania na kushirikiana na rais Jakaya Kikwete kuzindua njia ya treni kutoka Dar e salaam kwenda rusumo/isaka mpakani mwa Tanzania na Rwanda. Kwa mara nyingine tena Paul Kagame akaja Tanzania mwezi November 2015 kuhudhuria uapishwaji wa rais John Magufuli.

Nashangaa kuona wapotoshaji wanaandika kuwa Magufuli kukubali mwaliko wa Rwanda ndio kumemaliza tofauti zilizokuwapo, pamoja na maneno mengine ya kutudunisha watanzania mbele ya Rwanda, kana kwamba Magufuli kaenda kuomba msamaha! Je kuja kwa Kagame nchini kwetu mara mbili, tena sio kusalimia bali kikazi hakukutosha kumaliza huo ugomvi na badala yake ni Magufuli ndio kamaliza ugomvi kwa kukubali mwaliko wa Kagame kwenda kutembea? Kwa nini Kagame alivyokuja hatukuambiwa kuwa kaja “kujifunza”, “anamkubali sana kikwete” na mengineyo?
kama kuna suala la msamaha kwa namna yoyote ile, ni Kagame ndie aliyeomba msamaha. Kwa tamaduni za kinyarwanda/kihima kutoa ng'ombe ni ishara ya kuomba amani na kuimarisha undugu, sio zawadi inayotolewa kiholela. Mara ya mwisho kwa kagame kutoa ng'ombe ilikuwa ni kurudisha uhusiano wake na rais Museveni na nchi ya uganda baada ya muda mrefu wa vita baridi kama ambayo tulikuwa nayo kati yetu na Rwanda. Bahati mbaya wenzetu wenye asili ya Rwanda humu JF wamekulia Dar es salaam hawaelewi the essence ya zawadi hii. Badala yake wanapiga propaganda zisizo na mashiko. Hata hapa nchini kwa tamaduni za makabila mbalimbali ukichukua mtoto wa mtu au 'mzigo' wa mtu unatozwa faini ya mifugo. Anayetoa mifugo ni yule mwenye makosa. :D

Anyway, ieleweke kuwa kuimarika kwa uhusiano wetu kwa sasa hakuna uhusiano wowote na nchi yetu kubadili msimamo wake juu ya masuala yote ambayo yalikuwa chanzo cha ugomvi wetu na Rwanda. Kwa bahati nzuri ni kuwa makundi ya M23 na FDLR yameondolewa nchini DRC (at least kwa upande wa vita), na hivyo hatuna sababu tena ya kupishana kauli. Lakini urafiki huu haumaanishi kuwa Tanzania itaungana na Rwanda/Kagame katika kila jambo, bado Tanzania ni ile ile isiyoyumbishwa kimsimamo.

Wenu katika ujenzi wa taifa, Jmali
Mhh!imekuchukua mda kweli,japo umerudia yaleyale kama kawaida hakuna jipya.
Cha msingi nikwamba Rwanda na Tanzania ninchi marafiki tofauti na mapenzi yenu.
Interahamwe zilichochea kwa sana ugomvi baina ya inchi hizi mbili, nimefuatilia sana kila supporter wako anajua lugha ya Kinyarwanda.
We predicted this before, kukataa big role ya Mheshimiwa Magufuli kurejesha uhusiano na Rwanda ni ujinga.
Just to remind you, Tanzania ,South Africa,Mozambique etc walipeleka majeshi DRC as par AU mandate na Rwanda ili kubaliana na uamuzi huu wa kutuma majeshi.
Hivyo kusema Rwanda haikufurahishwa na uamuzi wa Tanzania kutuma majeshi DRC ni kurudia propaganda zilezile mlizokuwa mnatumia kueneza chuki.
Propaganda zenu (interahamwe) ndizo ziliifanya JWTZ ku intervene na kutoa tangazo kuwalaani..
Nikwenye tangazo hilo mlikumbushwa kwamba hata silaha zilizokuwa zinatumiwa DRC kwenye mapigano zilikuwa zikipita Rwanda.
jMali unajulikana kama FDRL spokesman ,na uhusiano mzuri wa Rwanda na nchi yoyote ni mwiba kwako.
Ndio maana every bad news about Rwanda inakuwa posted na jMali.
 
Hapa najisomea kimya na kuwashangaa, sasa mbona yasiishe jameni, marais wamekubali kuungana na kufanya kazi pamoja, malumbano miaka yote hii ya nini. Kikwete keshakwenda zake Msoga, awamu ya sasa ni ya Magufuli, mbona tusiyaweke chini yote na kukubali kufanya kazi pamoja.
 
na ndoto za alinacha FDLR jMali ndio kwanza zinaanza! eti FDLR wameondolewa DRC? haya... RDF Repulses FDLR In Late Night Attack, One Dead - KT PRESS hebu kwanza tuachane na hao ndugu zako FDLR nianze nikupe za Mheshimiwa Raisi Magufuli! ninaimani hata yeye alijisikia yuko nyumbani, vijana wetu waliosomea Mlimani, Mzumbe, Sokoine walijimix na delegation ya Raisi Magufuli mpaka raha yani! Man... you have got to admire him! n'IMFURA pe! kwanza ile ongea yake tu na jinsi alivyo-livyo basi hapa Kigali tukajua tu KWELI zama za uongozi wa kinafiki kwenye hizi nchi zetu MASIKINI ushapitwa na wakati! sijui ni semeje lakini ndugu yangu jMali kama bado upo busy na zile plan zenu za kuisumbua Rwanda basi bora ungetafuta chaka jingine na sio kwa Mheshimiwa Magufuli! REFRESHING REFRESHING REFRESHING
Asa me nahisi kama hujailewa makala ya jamaa kama si kumuelewa jamaa mwnyewe, em pitia upya basi bro
 
Propaganda maana yake ni uongo, onyesha ni wapi katika hiyo post nimeandika uongo. Ukishindwa maana yake wewe ndio unapiga propaganda kuwa mimi napiga propaganda.
ndio ni UONGO MTUPU!
1) hakuna asiyejuwa jinsi report ilivyokuwa imejaa uzushi! je unakumbuka kwa nini huo msaada ulirudishwa? report ilikutwa imejaa upuuzi lakini wazungu iliwasaidia sana kumbuka kipindi kile walikuwa katika ECONOMIC CRISIS na ile report iliwasaidia sana kubana matumizi! lakini kwa nchi jirani au mtu kama KIKWETE/hiMEMBE ambao wana uwezo wa kupeleleza hali halisi au angalau kuuliza maswali kuhusiana na hiyo report iliyo jaa utumbo, hakuna majina wala mateka wa kijeshi au KITU CHOCHOTE CHENYE MSHIKO(kama ushahidi) unawezaje kulopoka hayo yote, kama sio kutafuta ukolofi na jirani! wacha tushukuru Mungu, unafiki umepitwa na wakati Ikulu baada ya ujio wa Mheshimiwa Magufuli.
2) labda ungetuambia ni kwa nini hizo Embassy ziliongeza zikafunguliwa?
3)ninachojuwa ni kwamba Rwanda, vita zote ilizo wahi pigana ni justified! hauwezi ukamkenulia The AGGRESSOR labda wewe!
4)nimekutumia hizo clip kusudi usije ukaleta sumu zako! kwa maneno yake mwenyewe Mheshimiwa Magufuli kasema kwa mda atakao maliza Rwanda anaamini atajifunza mengi! sasa we inakuuma hiyo?
5)FDLR imeondolewa Burundi/DRC? you must be joking...
 
Asa me nahisi kama hujailewa makala ya jamaa kama si kumuelewa jamaa mwnyewe, em pitia upya basi bro
hapana, ni UONGO MTUPU!
1) hakuna asiyejuwa jinsi report ilivyokuwa imejaa uzushi! je unakumbuka kwa nini huo msaada ulirudishwa? report ilikutwa imejaa upuuzi lakini wazungu iliwasaidia sana kumbuka kipindi kile walikuwa katika ECONOMIC CRISIS na ile report iliwasaidia sana kubana matumizi! lakini kwa nchi jirani au mtu kama KIKWETE/hiMEMBE ambao wana uwezo wa kupeleleza hali halisi au angalau kuuliza maswali kuhusiana na hiyo report iliyo jaa utumbo, hakuna majina wala mateka wa kijeshi au KITU CHOCHOTE CHENYE MSHIKO(kama ushahidi) unawezaje kulopoka hayo yote, kama sio kutafuta ukolofi na jirani! wacha tushukuru Mungu, unafiki umepitwa na wakati Ikulu baada ya ujio wa Mheshimiwa Magufuli.
2) labda ungetuambia ni kwa nini hizo Embassy ziliongeza zikafunguliwa?
3)ninachojuwa ni kwamba Rwanda, vita zote ilizo wahi pigana ni justified! hauwezi ukamkenulia The AGGRESSOR labda wewe!
4)nimekutumia hizo clip kusudi usije ukaleta sumu zako! kwa maneno yake mwenyewe Mheshimiwa Magufuli kasema kwa mda atakao maliza Rwanda anaamini atajifunza mengi! sasa we inakuuma hiyo?
5)FDLR imeondolewa Burundi? you must be joking...
 
Mhh!imekuchukua mda kweli,japo umerudia yaleyale kama kawaida hakuna jipya.
Cha msingi nikwamba Rwanda na Tanzania ninchi marafiki tofauti na mapenzi yenu.
Interahamwe zilichochea kwa sana ugomvi baina ya inchi hizi mbili, nimefuatilia sana kila supporter wako anajua lugha ya Kinyarwanda.
We predicted this before, kukataa big role ya Mheshimiwa Magufuli kurejesha uhusiano na Rwanda ni ujinga.
Just to remind you, Tanzania ,South Africa,Mozambique etc walipeleka majeshi DRC as par AU mandate na Rwanda ili kubaliana na uamuzi huu wa kutuma majeshi.
Hivyo kusema Rwanda haikufurahishwa na uamuzi wa Tanzania kutuma majeshi DRC ni kurudia propaganda zilezile mlizokuwa mnatumia kueneza chuki.
Propaganda zenu (interahamwe) ndizo ziliifanya JWTZ ku intervene na kutoa tangazo kuwalaani..
Nikwenye tangazo hilo mlikumbushwa kwamba hata silaha zilizokuwa zinatumiwa DRC kwenye mapigano zilikuwa zikipita Rwanda.
jMali unajulikana kama FDRL spokesman ,na uhusiano mzuri wa Rwanda na nchi yoyote ni mwiba kwako.
Ndio maana every bad news about Rwanda inakuwa posted na jMali.
1. Onyesha link yoyote ambayo mapenzi yangu yalikuwa kinyume na urafiki kati ya watu wa Rwanda na Tanzania. Ukiweza kuonyesha hilo naahidi kuhama JF! Najua huwezi kuthibitisha hilo kwa sababu kwenu nyie team kagame it's all or nothing. Criticism against Kagame maana yake kwenu ni chuki dhidi ya watutsi wote duniani!
2. Unachokisisitiza ndicho nilichokipinga, mbona hujibu hoja? Kagame kaja mara mbili TZ mwaka jana tu, na alishazungumza na kikwete wazi wazi Nairobi, ..Magufuli kwenda Rwanda imeboreshaje uhusiano zaidi ya safari za kagame Tanzania? Au unataka kusema Kagame alivyokuwa anakuja alikuwa amenuna?
Mheshimiwa Membe alikuwa anadanganya aliposema haya:
"Kwa kweli kikao kati ya Rais Kikwete na Rais Kagame kimeondoa majungu yote, kimekata fitina, uongo na maneno ya kuchombeza yaliyokuwa yakitawanywa na watu mbalimbali hapa nchini na hata kule Kigali,”. Ugomvi ulishakwisha siku nyingi ila nyinyi lazima kujisifia sifia tu bila mpango.
3. Rwanda haikukubaliana na TZ wala nchi yoyote kupeleka majeshi. Ilipendelea mazungumzo kati ya M23 na DRC yaendelee hilo liko wazi, hatuwezi kulumbana katika hilo surely! Objections za Rwanda na Uganda katika hilo ziko wazi. Are you really saying Rwanda did not object to our troops there at all? Na badala yake ilifurahia?
4 Umeshaanza kuniita Interahamwe:)...grow up kijana, anyway, tangazo pekee ninalolikumbuka lililotolewa na JWTZ wakati ule ni hili hapa:Home
Sasa nakupa changamoto ulete hilo tangazo lako hapa na lenyewe tulione! Usipolileta naomba niruhusiwe kukuita wewe ndio interahamwe.
5. Kuhusu hicho cheo cha spokesperson wa FDLR nadhani ni ile ile staili yenu ya kuchepusha mada pale mnapoishiwa na hoja. Wacha spokesperson, muanzilishi wa hiyo FDLR leo hii ni kiongozi wako wewe huko Rwanda! Hivyo hata kama ingekuwa kweli mimi ni FDLR, hujui kuwa unanitakia mema? Kiongozi wa FDLR kama mimi nikirudi Rwanda nitakula shavu kubwa kuliko wewe jeshi la cyberspace! Uongo?:D
 
Hapa najisomea kimya na kuwashangaa, sasa mbona yasiishe jameni, marais wamekubali kuungana na kufanya kazi pamoja, malumbano miaka yote hii ya nini. Kikwete keshakwenda zake Msoga, awamu ya sasa ni ya Magufuli, mbona tusiyaweke chini yote na kukubali kufanya kazi pamoja.
Mambo yalishaisha toka mwaka jana, Kikwete na Kagame walishaungana hapo kwenu Nairobi. Kagame kashakuja Tanzania twice including kuapishwa kwa Magufuli. Yote haya ni facts. Hawa rafiki zako wanatumia chance hii ya Magufuli kutembelea Rwanda kumtukana na kumdhalilisha Kikwete kwa sababu zao zinazojulikana na wote. Najaribu kuwarudisha kwenye mstari that's all.
 
ndio ni UONGO MTUPU!
1) hakuna asiyejuwa jinsi report ilivyokuwa imejaa uzushi! je unakumbuka kwa nini huo msaada ulirudishwa? report ilikutwa imejaa upuuzi lakini wazungu iliwasaidia sana kumbuka kipindi kile walikuwa katika ECONOMIC CRISIS na ile report iliwasaidia sana kubana matumizi! lakini kwa nchi jirani au mtu kama KIKWETE/hiMEMBE ambao wana uwezo wa kupeleleza hali halisi au angalau kuuliza maswali kuhusiana na hiyo report iliyo jaa utumbo, hakuna majina wala mateka wa kijeshi au KITU CHOCHOTE CHENYE MSHIKO(kama ushahidi) unawezaje kulopoka hayo yote, kama sio kutafuta ukolofi na jirani! wacha tushukuru Mungu, unafiki umepitwa na wakati Ikulu baada ya ujio wa Mheshimiwa Magufuli.
2) labda ungetuambia ni kwa nini hizo Embassy ziliongeza zikafunguliwa?
3)ninachojuwa ni kwamba Rwanda, vita zote ilizo wahi pigana ni justified! hauwezi ukamkenulia The AGGRESSOR labda wewe!
4)nimekutumia hizo clip kusudi usije ukaleta sumu zako! kwa maneno yake mwenyewe Mheshimiwa Magufuli kasema kwa mda atakao maliza Rwanda anaamini atajifunza mengi! sasa we inakuuma hiyo?
5)FDLR imeondolewa Burundi/DRC? you must be joking...

Unafiki ni kusisitiza kuwa hukumbuki Kagame alikuja TZ mara mbili mwaka jana! Mengine yote hayo ni nonsense!
 
1. Onyesha link yoyote ambayo mapenzi yangu yalikuwa kinyume na urafiki kati ya watu wa Rwanda na Tanzania. Ukiweza kuonyesha hilo naahidi kuhama JF! Najua huwezi kuthibitisha hilo kwa sababu kwenu nyie team kagame it's all or nothing. Criticism against Kagame maana yake kwenu ni chuki dhidi ya watutsi wote duniani!
2. Unachokisisitiza ndicho nilichokipinga, mbona hujibu hoja? Kagame kaja mara mbili TZ mwaka jana tu, na alishazungumza na kikwete wazi wazi Nairobi, ..Magufuli kwenda Rwanda imeboreshaje uhusiano zaidi ya safari za kagame Tanzania? Au unataka kusema Kagame alivyokuwa anakuja alikuwa amenuna?
Mheshimiwa Membe alikuwa anadanganya aliposema haya:
"Kwa kweli kikao kati ya Rais Kikwete na Rais Kagame kimeondoa majungu yote, kimekata fitina, uongo na maneno ya kuchombeza yaliyokuwa yakitawanywa na watu mbalimbali hapa nchini na hata kule Kigali,”. Ugomvi ulishakwisha siku nyingi ila nyinyi lazima kujisifia sifia tu bila mpango.
3. Rwanda haikukubaliana na TZ wala nchi yoyote kupeleka majeshi. Ilipendelea mazungumzo kati ya M23 na DRC yaendelee hilo liko wazi, hatuwezi kulumbana katika hilo surely! Objections za Rwanda na Uganda katika hilo ziko wazi. Are you really saying Rwanda did not object to our troops there at all? Na badala yake ilifurahia?
4 Umeshaanza kuniita Interahamwe:)...grow up kijana, anyway, tangazo pekee ninalolikumbuka lililotolewa na JWTZ wakati ule ni hili hapa:Home
Sasa nakupa changamoto ulete hilo tangazo lako hapa na lenyewe tulione! Usipolileta naomba niruhusiwe kukuita wewe ndio interahamwe.
5. Kuhusu hicho cheo cha spokesperson wa FDLR nadhani ni ile ile staili yenu ya kuchepusha mada pale mnapoishiwa na hoja. Wacha spokesperson, muanzilishi wa hiyo FDLR leo hii ni kiongozi wako wewe huko Rwanda! Hivyo hata kama ingekuwa kweli mimi ni FDLR, hujui kuwa unanitakia mema? Kiongozi wa FDLR kama mimi nikirudi Rwanda nitakula shavu kubwa kuliko wewe jeshi la cyberspace! Uongo?:D
Rwanda and DRC agree to AU military force
JWTZ LATOA ONYO KALI KWA VYOMBO VYA HABARI VINAVYOANDIKA HABARI ZA UONGO KUHUSU MZOZO WA DRC..!! | Habari kamili
Awe Kikwete,Kagame au Magufuli sisi tunachotaka ni uhusiano mzuri.
 
Interahamwe yupo katika mwezi mchanga! kama ulivyosema hiki kipindi cha maombolezo hawashikiki, damu za watu wasio na hatia zinawasumbua, out there in full force!
Kila siku nakuambia wewe banyamulenge, jufunze kujibu hoja kwa hoja. Usiwe unajibu hoja kwa matusi!
 
Wewe interahamwe nobody is taking you serious na hamna cha kuchangia...just go away
 
Kwa bahati mbaya ziara ya rais wa Tanzania mhe John Magufuli nchini Rwanda inapotoshwa sana hasa na mashabiki wa Rwanda/kagame humu mitandaoni mfano rejea: Wako wapi wale anti Kagame?.
Mhanga wa ziara hiyo amekuwa rais mstaafu Jakaya Kikwete, ambaye katika hali isiyo ya kawaida analaumiwa kwa ugomvi ambao kwa mtu yoyote makini ulishakwisha toka mwaka jana! Yafuatayo ni maoni yangu juu ya vitu muhimu ambavyo vinapotoshwa:

1. KUZOROTA UHUSIANO NI KOSA LA KIKWETE:

Ukisoma maoni ya wanazi mbalimbali wa Rwanda/Kagame, Tanzania inaonekana kuwa ndio iliyoikosea Rwanda. Suala hili sio kweli.

Jambo la kwanza lililozorotesha uhusiano wetu na Rwanda ni pale ambapo Tanzania iliamua kuungana na mataifa ya DRC na Afrika kusini kuwapiga waasi wa M23 kijeshi mwaka 2013. Maamuzi haya yalikuwa kinyume na mtazamo wa mataifa ya Kenya, Uganda na Rwanda ambao wakati huo walikuwa wakijiita COW (coalition of the willing), ambao wao walipendelea mazungumzo yasiyokuwa na tija yaendelee kati ya M23 na Uganda. Ni siri iliyokuwa wazi kuwa majeshi ya M23 yalikuwa ni vibaraka wa Rwanda. Hili limethibitishwa na ripoti ya umoja wa mataifa. Pia nchi za marekani na Uingereza zilisitisha misaada kwenda Rwanda kama adhabu (kama sisi tulivyokosa pesa za MCC) kutokana na nchi hizo kujiridhisha kuwa Rwanda ilikuwa nyuma ya M23, cha ajabu Rwanda haikuwahi kuzishutumu nchi hizi kama ambavyo ilimshutumu waziri Bernard Membe ambaye yeye alirejea taarifa hizo hizo za umoja wa mataifa.

Suala lingine lililoleta shida ni pale ambapo rais Kikwete, katika mkutano wa nchi za maziwa makuu, alishauri mazungumzo kati ya serikali na waasi wa nchi mbalimbali zenye vita ikiwapo Rwanda. (chanzo: KIKWETE Statement on Rwanda misquoted | The Rwandan). Ushauri huu ulipokelewa vizuri na nchi zote Uganda na DRC kasoro Rwanda. Hakukuwa na shida yoyote kama Rwanda wangepuuza ushauri wetu, lakini cha ajabu uongozi wa serikali ya Kagame ukalipuka kwa matusi na kashfa mbalimbali za kutuita interahamwe, uzushi kama kabila la mke wa Rais na mengineyo na mwishowe kwa rais Kagame binafsi kutishia kumpiga Kikwete. Hali hii ikapelekea Tanzania nayo kujibu mashambulizi kwa maneno mbalimbali.

Hata hivyo ugomvi huu ulikuwa ni vita baridi, kwani mahusiano ya kibalozi bado yaliendelea pale pale, hakuna siku wananchi wa Tanzania au Rwanda nikiwamo mwandishi wa post hii walizuiwa au kurudishwa mpakani pale walipotaka kuvuka. Hakuna manyanyaso yoyote ambayo raia wa nchi zetu walizipata wakiwa wanaishi na kufanya kazi kihalali nchi nyingine. Hivyo ugomvi huu ulikuwa ni wa ngazi za kisiasa zaidi na haukufika chini kwa viwango vya wananchi kuonana maadui, isipokuwa labda kwenye mitandao ya kijamii.

Kwa sababu zote kuu mbili za ugomvi wetu, hakuna uwezekano wowote kuwa rais Kikwete au nchi ya Tanzania ndio iliyokosea. Ni upotofu mkubwa kumlaumu Kikwete na Tanzania kutokana na ugomvi uliotokea. Uongozi wa rais Kagame wa Rwanda una historia iliyotukuka ya kugombana na nchi nyingi duniani kuliko nchi yoyote hapa Afrika labda na dunia kutokana na hulka yake ya kibabe. Mifano michache ni:
  • Kufukuzwa kwa ubalozi mzima wa Rwanda nchini Kenya mwaka 1996 kutokana na mauaji ya mpinzani/mkimbizi wa kisiasa Seth sendashonga yaliyofanywa na maafisa ubalozi huo
  • Kufukuzwa kwa ubalozi wa Rwanda nchini afrika kusini 2014 kutokana na majaribio ya mauaji ya mpinzani/mkimbizi wa kisiasa Gen Kayumba Nyamwasa.
  • Kufukuzwa kwa diplomat wa Rwanda Evode Mudaheranwa nchini Sweden 2012 kwa tuhuma za kufanya ujasusi dhidi ya wakimbizi wa kisiasa nchini humo.
  • Kufukuzwa kwa diplomats wa Rwanda nchini Burundi 2014 akiwamo Desire Nyaruhirira ambaye baada ya kutoroka inadaiwa nyumbani aliyokuwa anaishi kulikutwa silaha nzito za kijeshi na kiasi kikubwa cha fedha za kimarekani!
Pia kwa nyakati tofauti Rwanda chini ya rais Kagame imeshapambana kivita na Uganda nchini DRC, imeshapamba na DRC wenyewe, burundi etc, na kutokana na ripoti ya UN (rejea: Kutoka ripoti ya UN: Tanzania na Rwanda zilishapigana!) hata Tanzania kupitia M23! Ukiunganisha na kufukuzwa kwa mabalozi wake nchini Kenya, Rwanda chini ya Kagame inakuwa na historia ya kuwa imegombana na nchi zote za EAC! Kwa mifano hiyo michache (ipo mingine ya magomvi na nchi za ulaya na marekani) haiingii akilini kudai kuwa Kikwete/Tanzania ndie chanzo cha kuzorota kwa uhusiano wa nchi zetu mbili. Tulikuwa sahihi na bado tuko sahihi.

2. KURUDI KWA UHUSIANO KUNATOKANA NA ZIARA HII YA MAGUFULI:

Ukweli ni kuwa marais Paul kagame na Jakaya kikwete walikutana na kuzungumza hadharani kwa mara ya kwanza baada ya nchi zetu kupishana maneno kwenye mkutano wa 16 wa viongozi wa Afrika mashariki kwenye ukumbi wa KICC pale Nairobi mwezi februari mwaka 2015.

Wiki chache baadae mwezi march 2015 Kagame alikuja Tanzania na kushirikiana na rais Jakaya Kikwete kuzindua njia ya treni kutoka Dar e salaam kwenda rusumo/isaka mpakani mwa Tanzania na Rwanda. Kwa mara nyingine tena Paul Kagame akaja Tanzania mwezi November 2015 kuhudhuria uapishwaji wa rais John Magufuli.

Nashangaa kuona wapotoshaji wanaandika kuwa Magufuli kukubali mwaliko wa Rwanda ndio kumemaliza tofauti zilizokuwapo, pamoja na maneno mengine ya kutudunisha watanzania mbele ya Rwanda, kana kwamba Magufuli kaenda kuomba msamaha! Je kuja kwa Kagame nchini kwetu mara mbili, tena sio kusalimia bali kikazi hakukutosha kumaliza huo ugomvi na badala yake ni Magufuli ndio kamaliza ugomvi kwa kukubali mwaliko wa Kagame kwenda kutembea? Kwa nini Kagame alivyokuja hatukuambiwa kuwa kaja “kujifunza”, “anamkubali sana kikwete” na mengineyo?
kama kuna suala la msamaha kwa namna yoyote ile, ni Kagame ndie aliyeomba msamaha. Kwa tamaduni za kinyarwanda/kihima kutoa ng'ombe ni ishara ya kuomba amani na kuimarisha undugu, sio zawadi inayotolewa kiholela. Mara ya mwisho kwa kagame kutoa ng'ombe ilikuwa ni kurudisha uhusiano wake na rais Museveni na nchi ya uganda baada ya muda mrefu wa vita baridi kama ambayo tulikuwa nayo kati yetu na Rwanda. Bahati mbaya wenzetu wenye asili ya Rwanda humu JF wamekulia Dar es salaam hawaelewi the essence ya zawadi hii. Badala yake wanapiga propaganda zisizo na mashiko. Hata hapa nchini kwa tamaduni za makabila mbalimbali ukichukua mtoto wa mtu au 'mzigo' wa mtu unatozwa faini ya mifugo. Anayetoa mifugo ni yule mwenye makosa. :D

Anyway, ieleweke kuwa kuimarika kwa uhusiano wetu kwa sasa hakuna uhusiano wowote na nchi yetu kubadili msimamo wake juu ya masuala yote ambayo yalikuwa chanzo cha ugomvi wetu na Rwanda. Kwa bahati nzuri ni kuwa makundi ya M23 na FDLR yameondolewa nchini DRC (at least kwa upande wa vita), na hivyo hatuna sababu tena ya kupishana kauli. Lakini urafiki huu haumaanishi kuwa Tanzania itaungana na Rwanda/Kagame katika kila jambo, bado Tanzania ni ile ile isiyoyumbishwa kimsimamo.

Wenu katika ujenzi wa taifa, Jmali
Aisee upo kaa Activist !! Sijajua kama ni mchambuzi rasmi wa mambo ya siasa au n MTU tu na Weredi wako!! Gud I like this proved evidence against our fellow who are trying to get clean for their own misery!! Nasisi kauli yetu ni moja..
We have done nothing wrong in this !! And we are perceived as a threat in this diplomatic relationship!! We are not a threat in this and we don't apologize ,we never did and never will
 
na ndoto za alinacha FDLR jMali ndio kwanza zinaanza! eti FDLR wameondolewa DRC? haya... RDF Repulses FDLR In Late Night Attack, One Dead - KT PRESS hebu kwanza tuachane na hao ndugu zako FDLR nianze nikupe za Mheshimiwa Raisi Magufuli! ninaimani hata yeye alijisikia yuko nyumbani, vijana wetu waliosomea Mlimani, Mzumbe, Sokoine walijimix na delegation ya Raisi Magufuli mpaka raha yani! Man... you have got to admire him! n'IMFURA pe! kwanza ile ongea yake tu na jinsi alivyo-livyo basi hapa Kigali tukajua tu KWELI zama za uongozi wa kinafiki kwenye hizi nchi zetu MASIKINI ushapitwa na wakati! sijui ni semeje lakini ndugu yangu jMali kama bado upo busy na zile plan zenu za kuisumbua Rwanda basi bora ungetafuta chaka jingine na sio kwa Mheshimiwa Magufuli! REFRESHING REFRESHING REFRESHING
Kumbe nyie watu ni wakorofi!! Nilikua nasikiaga tu aisee Sijui kabila gan kati ya Yale mawili
 
Back
Top Bottom