Kuhamisha wananchi: Serikali iache ubabaishaji

J.K.Rayhope

JF-Expert Member
Oct 26, 2011
316
31
Wanajf,

Naombeni msaada hata wa mawazo.

Serikali imetangaza kuwahamisha wakazi wa mabondeni kwa sababu tu ya mafuriko ya Dsm. Labda tu nieleze jambo moja, tayari asilimia kubwa ya nyumba hizi zina leseni za makazi na hata hati halali kutoka wizara ya ardhi, hivyo zinatambulika na zinalipa kodi zote. Leo nyumba nyingi sehemu mbalimbali kama Jangwani, Mchikichini, Kigogo, Kinondoni, n.k zimeandikwa namba kwa rangi nyekundu. Kuandikwa si tatizo, je nini kinafuatia? Nasikia kelele twende Mabwepande, kule ni bushi hakuna huduma muhimu.

Hivi mimi na wajukuu tukaishi kwenye mahema? Kiwanja ndio nyumba? Serikali leo imepata wapi polisi wa kulinda usalama wakati huu wa kuziandika namba na si wakati ule wanajenga? Leo mtu amestaafu, kiinua mgongo kajengea kibanda chake, umwambie nenda Mabwepande kwenye mahema!! Viwanja vimepatikana baada ya ajali?

Leo mtu atakula kiwanja au atajenga nyumba kwa kipato gani? Sina nia ya kupingana na serikali, ina nguvu lakini hapa ilipaswa kutumia nguvu wakati watu wanajenga. Acha, huna hatimiliki, kibali ni kwamba hata mahakama haina muda mchafu wa kusikiliza kesi hiyo. Sasa iweje umpe mtu hati, leo toka nenda kule.

Ni kwamba serikali iache ubabaishaji, YES iwe ya kweli, NO iwe ya kweli. Aliyewapa watu hawa leseni ni nani? Je wamevunja na kuiba hizi leseni za makazi? Nifanyeje?
 
Back
Top Bottom