Kufungwa kwa Jukwaa la DINI

Invisible

Robot
Feb 11, 2006
9,075
7,878
Wakuu,

Nasikitika kutangaza kufungwa kwa Jukwaa la Dini.

Malalamiko dhidi ya jukwaa hili yamekuwa mengi na moderators hawataweza kuvumilia kero zinazotokana na malalamiko haya.

Ukweli ni kwamba malalamiko yote yako sahihi na pia LILIKUWA NA MATATIZO ambayo dawa yake ni kulipitia upya na kuchukua hatua muhimu kwa manufaa ya wote wanaolitumia.

Izingatiwe kuwa, sheria zitazingatiwa katika kulipitia upya na lugha yoyote itakayoonekana kuwa CHAFU ama kejeli zisizo za lazima zitafutiliwa mbali na wahusika watafahamishwa.

Baada ya kulipitia jukwaa hili, litakuwa public na litakuwa chini ya uangalizi wangu na moderators wengine wawili wapya watakaotambulishwa kwenu.

Nasikitika kwa usumbufu utakaojitokeza kwa YEYOTE. Ni hatua ambayo kwa sasa haikwepeki na ni LAZIMA iwe ilivyo sasa.

Ahsanteni
 
Kila la kheri mkuu.
 
Ahsante,

Katika kulipitia jukwaa hili nitashirikiana kwa karibu na wafuatao:

X-PASTER na MaxShimba

Nawaomba ushirikiano wakuu

You can't be serious Mr. Invisible....yaani MaxShimba unamweka kuwa modereta wa jukwaa la dini?
 
Hahaha,

Hapana, ni ushauri pale ninapoona maandiko ninayo-suspect kuwa ya kichochezi na endapo yataletwa public hayataleta maana nyingine.

Ahsante
 
Invisible,
Kweli likiondolea jukwaa hili tutaweza hilo la siasa kila siku? mhhhhhh
haya Bwana. Mimi nalalamikia lile la mambo ya kikubwa nalo lishughulikiwe tafadhali. Ila naomba kwanza maoni ya mazee K********
 
...I hope hawatakuja huku 'kuchafua' hali ya hewa na malumbano yao :(
 
Wanaelewa na naamini wengi wana busara kubwa, watatupa muda wa kujipanga kuliweka Jukwaa sawa.

Mkuu Mchukia Fisadi,
Mambo ya Kikubwa sijapata lawama hata kidogo... Kama linakusumbua basi mkuu wacha nikuondoshee access haraka kabla hujakosa exit door!
 
Ahsante,

Katika kulipitia jukwaa hili nitashirikiana kwa karibu na wafuatao:

X-PASTER na MaxShimba

Nawaomba ushirikiano wakuu

Unakaribishwa Mkuu Invisible any time.

Max Shimba, A Bondservant of Jesus Christ, KING OF KINGS.
 
Shukrani bro kwa pendekezo lako, na pia ni heshima kubwa sana kwangu.. mie ambaye ni mwanafunzi tu katika ulimwengu huu wenye mahalifa mengi

Ila kabla ya mimi binafsi kuamua kutumia haki yangu ya msingi ya kukubali ama kukataa pendekezo lako, naomba ufanye jambo moja kwanza.

Tafadhali sana sana, taka au tafuta ushauri wa wanachama. Ninavyosema wanachama najumuisha na wale ambao hawa kuwahi kuwa na access na jukwaa la dini ambao nadhani idadi yao ni kubwa kuliko sisi ambao tulikuwa na access kule.

La kama itaonekana kuwa haiwezekani, basi utupatie sababu ambazo wewe binafsi umeona ni muwafaka kwa nini umetoa maamuzi hayo mazito ya kunipendekeza mimi niwe mmojawapo wa hao viranja watakao kusaidia wewe.

Natanguliza shukrani zangu za dhati.

X-Paster
 
Unakaribishwa Mkuu Invisible any time.

Max Shimba, A Bondservant of Jesus Christ, KING OF KINGS.
Ahsante mkuu
Shukrani bro kwa pendekezo lako, na pia ni heshima kubwa sana kwangu...
Wewe ni mwalimu wa wengi, mmojawapo mimi.

Usitie shaka, nitakachofanya ni kuongea nanyi pembeni... Nimewafikiria ninyi wawili kwa kuanzia lakini mkihitaji wengine wawili toka pande mbili naweza kuwaongezea.

Nitawapa namna ya kufanya na nitawaombea kabla hamjaanza hiyo kazi. Naamini tunaweza kushirikiana kufanya kitu kikubwa zaidi ya kile mnachokiona kule.

Kwanza, tutatengeneza kitabu kimoja cha kumbukumbu na kitakuwa katika PDF format, kitahusisha topic zote kule (behind the scene) kisha tutatoa kingine kilichokuwa reviewed (movie yenyewe) kisha tutawakabidhi wadau Jukwaa lao likiwa liko pruned na likiwa na sheria zake ambapo huenda baada ya kazi ile mtakuwa na cha kuongea tofauti na sasa.

Ninaomba tuwasiliane via PM kujua nini kifanyike na kivipi.

Najua kazi yenyewe ni ngumu lakini kwa kuwashirikisha ninyi wawili naamini itakuwa rahisi na itakuwa na baraka zote.

Wasalaam
 
Babu uwa unakwenda kwenye jukwa la dini? huko sijawahi kuingia wala kwenye jukwaa la mambo ya kikubwa lol.

Jukwaa la dini huwaga naenda kwa nadra sana. Kuna mtu alisema Pundit alilikimbia baada ya kunyweshwa juisi ya pilipili so ikabidi niingie nione kukoje. Defininitely not my cup o tea

Mbona nakuona huko sasa hivi?

Heheheheheee...sasa babu unadai chemba huingii wakati roboti anakuona...Lol
 
Ahsante mkuu

Wewe ni mwalimu wa wengi, mmojawapo mimi.

Usitie shaka, nitakachofanya ni kuongea nanyi pembeni... Nimewafikiria ninyi wawili kwa kuanzia lakini mkihitaji wengine wawili toka pande mbili naweza kuwaongezea.

Nitawapa namna ya kufanya na nitawaombea kabla hamjaanza hiyo kazi. Naamini tunaweza kushirikiana kufanya kitu kikubwa zaidi ya kile mnachokiona kule.

Kwanza, tutatengeneza kitabu kimoja cha kumbukumbu na kitakuwa katika PDF format, kitahusisha topic zote kule (behind the scene) kisha tutatoa kingine kilichokuwa reviewed (movie yenyewe) kisha tutawakabidhi wadau Jukwaa lao likiwa liko pruned na likiwa na sheria zake ambapo huenda baada ya kazi ile mtakuwa na cha kuongea tofauti na sasa.

Ninaomba tuwasiliane via PM kujua nini kifanyike na kivipi.

Najua kazi yenyewe ni ngumu lakini kwa kuwashirikisha ninyi wawili naamini itakuwa rahisi na itakuwa na baraka zote.

Wasalaam

Sawa sawa nimekuelewa.
Tupo pamoja Insha'Allah.
 
Back
Top Bottom